Skip to main content

Posts

Showing posts from December 11, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Ujenzi wa Jengo la Kituo Cha Mafunzo ya Kuongeza Thamani Madini ya Vito Waanza Jijini Arusha

■ Ni mkakati wa kuhakikisha madini vito yanaongezewa thamani nchini. ■Ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais.Dkt. Samia katika kuendeleza mnyororo wa madini thamani. ■Waziri Mavunde amtaka mkandarasi kuongeza nguvukazi kukamilisha mradi kwa wakati. ▪️Atoa siku 7 kwa Katibu Mkuu kukutana na wakandarasi,TGC na Taasisi za serikali kwa ajili ya upatikanaji vibali muhimu vya kuendeleza ujenzi. *Arusha* Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amemtaka mkandarasi wa ujenzi wa kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) kukamilisha ujenzi wa majengo ya kituo cha mafunzo ya Uongezaji thamani madini ya vito kwa kuongeza nguvukazi na kufanya kazi kwa masaa 24 ili kukamilisha ujenzi wa jengo kwa muda mfupi. Waziri Mavunde ameyasema hayo leo Desemba 12, 2025 mkoani Arusha wakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa kituo hicho ulioanza ujenzi rasmi ambapo katika maelekezo yake amemtaka mkandarasi kuzingatia ujenzi bora wenye kukidhi vigezo vilivyoainishwa kwenye mkataba. Waziri Mavunde amefafanua kuwa, Serikali...

Waziri Ulega Atoa Agizo Kwa Kampuni ya Ujenzi ya Jasco ya Jijini Mwanza

 Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, ameutaka mkandarasi Jassie and Company (JASCO) kuhakikisha ujenzi wa Daraja la Mkuyuni unakamilika na kukabidhiwa ifikapo Januari 15, 2026, ili kupunguza adha wanayoipata wananchi hususan katika kipindi cha mvua. Ulega ametoa maelekezo hayo leo, Desemba 11, 2025, mkoani Mwanza wakati wa ziara maalum ya kukagua maendeleo ya mradi huo. Ziara hiyo imefanyika kufuatia agizo la Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, aliyemtaka Waziri kufika eneo hilo kubaini sababu za kuchelewa kwa utekelezaji wa ujenzi. Waziri Ulega amesema Serikali haitavumilia ucheleweshaji unaowaathiri wananchi na kusisitiza mkandarasi kuongeza kasi kuhakikisha daraja linakamilika kwa viwango vinavyostahili.

Askofu Mwamakula Amwaga Siri Kuhusu Jenista Mhagama

   *Ameandika Askofu Mwamakula* 🙏🙏🙏 Usilolijua Kuhusu Jenista Mhagama! Nusu ya pili ya mwaka 2023 ilikuwa na joto la aina yake katika siasa za Tanzania. Fenomena ijulikanayo kama Boniface Anyisile Mwabukusi ilianza kuchomoza na kung'ara katika siasa za Tanzania kupitia sakata la Mkataba wa Bandari. Mwabukusi, Dkt. Slaa na Mdude waliwekwa kizuizini kule Mbeya baada ya IGP kutangaza kuwa kuna watu walitaka kuipindua serikali ya Rais Samia. Askofu Mwamakula alijikuta akiwa katikati ya utetezi wa watu hao. Walitamkiwa makosa ya uhaini, lakini ghafla wakaachiwa wakiwa polisi bila ya kufikishwa mahakamani. Alphonce Lusako Mwamwile na mawakili wenzake walifungua kesi ya kupinga mkataba huo. Mwabukusi na wenzake wakawa mawakili wao. Lakini kesi ilitupwa mahakamani kwa kile kilichoelezwa na jaji kuwa mahakama haikuwa na mamlaka ya kuingilia mamlaka ya Bunge. Mwabukusi na wenzake kadhaa wakahamishia mapambano nje kwa kutangaza maandamano. Mwabukusi alianza kusakwa kama 'dhahabu ya Ch...

Usilolijua Kuhusu Jenista Mhagama!

 *Ameandika Askofu Mwamakula* 🙏🙏🙏 Usilolijua Kuhusu Jenista Mhagama! Nusu ya pili ya mwaka 2023 ilikuwa na joto la aina yake katika siasa za Tanzania. Fenomena ijulikanayo kama Boniface Anyisile Mwabukusi ilianza kuchomoza na kung'ara katika siasa za Tanzania kupitia sakata la Mkataba wa Bandari. Mwabukusi, Dkt. Slaa na Mdude waliwekwa kizuizini kule Mbeya baada ya IGP kutangaza kuwa kuna watu walitaka kuipindua serikali ya Rais Samia. Askofu Mwamakula alijikuta akiwa katikati ya utetezi wa watu hao. Walitamkiwa makosa ya uhaini, lakini ghafla wakaachiwa wakiwa polisi bila ya kufikishwa mahakamani. Alphonce Lusako Mwamwile na mawakili wenzake walifungua kesi ya kupinga mkataba huo. Mwabukusi na wenzake wakawa mawakili wao. Lakini kesi ilitupwa mahakamani kwa kile kilichoelezwa na jaji kuwa mahakama haikuwa na mamlaka ya kuingilia mamlaka ya Bunge. Mwabukusi na wenzake kadhaa wakahamishia mapambano nje kwa kutangaza maandamano. Mwabukusi alianza kusakwa kama 'dhahabu ya Chuny...

Makamu wa Rais Dkt Nchimbi amlilia Mhagama

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema Taifa limepata pengo kuondokewa na aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma, Jenista Mhagama ambaye alikuwa kiongozi aliyeheshimika na kutumikia nchi katika majukumu mbalimbali ya kitaifa. Makamu wa Rais amesema hayo wakati akitoa salamu za rambirambi alipowasili kuhani msiba nyumbani kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, marehemu Jenista Mhagama eneo la Itega Jijini Dodoma. Amesema ripoti Mhagama licha ya kuwa mbunge wa Jimbo la Peramiho, lakini pia alitoa mchango wake katika Chama Cha Mapinduzi na maendeleo ya Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla. Makamu wa Rais ametoa pole kwa familia na waombolezaji na kuwaombea watoto wa marehemu na ndugu wa karibu, Mungu awape ujasiri wa kukubali jambo hilo na kutambua ni njia ya watu wote.

Waziri Gwajima ashiriki mkutano wa wanawake, Amani na Usalama ( WPS ) nchini Tunisia

 ASISITIZA USHIRIKIANO KUIMARISHA USAWA WA KIJINSIA* Na WMJJWM – Tunisia Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, ameshiriki Mkutano wa 6 wa Ngazi ya Juu kuhusu Masuala ya Wanawake, Amani na Usalama (WPS) uliofanyika tarehe 9–10 Desemba 2025 katika Chuo cha Kimataifa cha Diplomasia, jijini Tunis nchini Tunisia. Akizungumza katika mkutano huo, Dkt. Gwajima ameupongeza Umoja wa Afrika kupitia Ofisi ya Mjumbe Maalum wa AU wa Masuala ya Wanawake, Amani na Usalama, pamoja na Serikali ya Tunisia kwa kuandaa mkutano huo muhimu wenye mstakabali wa Wanawake. Akiwasilisha mchango wake katika mjadala wa jopo la wataalamu, Dkt. Gwajima amesema kasi ya ukuaji wa teknolojia na akili mnemba imekuwa na manufaa pale inapowezesha jamii kuelimishwa kuhusu madhara ya ukatili wa kijinsia, sambamba na kusambaza ujumbe wa kukataa vitendo hivyo. Dkt. Gwajima pia ameeleza mafanikio makubwa yaliyofikiwa na Tanzania, ikiwemo kuzinduliwa kwa Mpango wa Taifa ...

Serikali ya Rais Samia yafanikisha ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam - Tawi la Bukoba

Makamu wa Rais Balozi Nchimbi kuweka Jiwe la Msingi Wiki kesho Jumatatu Disemba 15, 2025._ Licha ya Mkoa wa Kagera kusifika kwa usomi lakini hadi muda huu hakuna Chuo Kikuu, ni mwaka jana 2024 Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ilianza kujenga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Tawi la Bukoba kwa gharama ya Bilioni 13.1. Ujenzi unaendelea vyema ukiwa zaidi ya asilimia 78. Chuo hiki kinajengwa kwenye Kijiji cha Itawa, Kata ya Karabagaine Halmashauri ya Wilaya Bukoba Vijijini ili kuwezesha sasa vijana na wananchi wapate elimu ya juu ndani ya Kagera. Makamu wa Rais wa Tanzania Balozi Emmanuel Nchimbi wiki ijayo Jumatatu 15/12/2025 kuanzia Saa 1 asubuhi ataweka Jiwe la Msingi kwenye Ujenzi wa Chuo hicho. Serikali ya Rais Samia imedhamiria kufanya mageuzi ya maendeleo na ndiyo maana miradi mikubwa kama hii ya Vyuo Vikuu vinajengwa hadi pembezoni kabisa katika nchi ili kuwafikia Watanzania wengi zaidi.  Wananchi wote wanakaribishwa kwenye tukio hili muhimu kwenye mkoa.