Na: Mwandishi Wetu, Pangani Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Bara, Mussa Mwakitinya, anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi wa mashindano ya mpira wa miguu wilayani Pangani yaliyopewa jina la Aweso Vijana Cup Aprili 4, 2026, katika uwanja wa mpira, Kata ya Mwera. Mashindano hayo yamelenga kuongeza fursa ya ajira kwa vijana kupitia michezo, kuepuka magonjwa yasiyoambukiza, kujenga mahusiano na afya bora, huku Mbunge wa Jimbo la Pangani na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, akiyafadhili mashindano hayo yaliyoandaliwa na Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM wilaya ya Pangani. Pambano la uzinduzi litahusisha timu kutoka Kata za Mwera na Tungamaa. Akizungumza ofisini kwake Aprili 3, 2026, Katibu wa UVCCM wilaya ya Pangani, Nasri Mkalipa, amesema vijana wajiandae kikamilifu kushiriki mashindano hayo muhimu. "Mbunge wetu Jumaa Aweso anawajali na kuwapenda vijana ndiyo maana amefadhili mashindano haya kwani siku hizi michezo sio burudani pekee lakini ni ajira pia, hivyo...
Marato tv - Sauti ya Jamii