Skip to main content

Posts

Showing posts from December 28, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Kadogosa Aadhimisha Misa Maalumu Kuliombea Taifa na Kumuombearais Samia Suluhu Hassan

Mbunge Wa Jimbo La Bariadi Vijijini Mh. Masanja Kungu Kadogosa Mapema Leo Amefanya Misa Maalum Ya Kumuombea Rasi Dkt. Samia Suluhu Hassan, Kuliombea Taifa Na Kumuombea Marehemu Baba Yake Mzee Daudi Kungu Kadogosa Tukio Lililofanyika Nyumbani Kwake Kijijini Mwakibuga, Mkoani Simiyu. Katika Dua Hii, Maombi Maalum Yamefanyika Kusisitiza Misingi Ya Kulinda Amani, Umoja Na Mshikamano Wa Kitaifa. Dua Hiyo Imehudhuriwa Na Viongozi Mbalimbali Wa Serikali Akiwemo Mkuu Wa Mkoa Wa Simiyu, Viongozi Wa Madhehebu Ya Katoliki - Zaidi Ya Mapadri 10, Waislam Wakiongozwa Na Sheikh Wa Mkoa Wa Simiyu, Walutherani, Madiwani Wa Vyama Mbalimbali Vya Siasa Na Maelfu Ya Wakazi Wa Mkoa Wa Simiyu.

Rc Batilda, Mwanafa Wakoshwa na 'hale Festival'

📍WAHIMIZA ENZI ZA TX MOSHI WILLIAM KUTUMIKA KUIBUA VIPAJI NA MASHAKA MHANDO, Korogwe MKUU wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian, amemwagia sifa mwandaaji wa tamasha la 'Hale Festival', Dkt. Hassan Abbas, huku akibainisha kuwa jukwaa hilo ni daraja imara la kuibua na kuendeleza vipaji vya muziki na soka mkoani humo. Akizungumza katika usiku wa kipekee wa kumkumbuka gwiji la muziki wa dansi nchini, marehemu TX Moshi William, uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Hale Lounge, Balozi Batilda alisema tamasha hilo ni mfano wa kuigwa katika kuenzi tunu za sanaa. "Sisi kama mkoa tumejifunza kupitia wazo hili zuri la Hale Festival. Kupitia tamasha hili, tunaweza kupata akina TX Moshi William wengi zaidi. Hongera sana Dkt. Abbas kwa maono haya," alisema Mkuu wa Mkoa. Katika kilele cha tamasha hilo, mwanzilishi wa Hale Festival, Dkt. Hassan Abbas, alitoa Tuzo ya Heshima (Lifetime Achievement Award) kwa marehemu TX Moshi William, kutokana na mchango wake uli...