Skip to main content

Posts

Showing posts from November 13, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

TUME YA HAKI ZA BINADAMU YAWEKA WAZI MSIMAMO WAKE KUHUSU KESI YA LISSU

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imesema hatua kuu za kiutaratibu katika kesi iliyokuwa ikimkabili Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Tundu Lissu zilifanyika kwa kuzingatia mfumo wa sheria za mwenendo wa makosa ya jinai, huku ikisisitiza kuwa uzingatiaji wa taratibu hizo pekee hauondoi wajibu wa kulinda haki za msingi za binadamu. Katika tamko lake la Novemba 13, 2026, kuhusu masuala ya haki za binadamu na utawala bora yaliyojitokeza katika kesi hiyo THBUB imeeleza kuwa tathmini yake ilibaini hatua kuu za kesi zilizothibitishwa na kumbukumbu ilizozichunguza zilifuata mfumo wa kisheria uliowekwa. THBUB imeeleza imesisitiza kuwa kufuata taratibu za kukamatwa, kufikishwa mahakamani na kusikilizwa kwa kesi hakutoshi peke yake kuthibitisha kuwa haki zote za binadamu zililindwa kikamilifu. Tume imetaja umuhimu wa kuhakikisha mtuhumiwa anapata msaada wa kisheria, muda na mazingira ya kutosha kuandaa utetezi, nyaraka muhimu za kesi na nafasi ya kuwauliza maswali mashahidi. Katika eneo...

RAIS SAMIA AWASILI DAR ES SAAM AKITOKEA NCHINI UTURUKI

  Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam, wakati akitokea Antalya nchini Uturuki na kupokewa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mhe. Deogratius Ndejembi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tarehe 13 Novemba, 2026. Akiwa Jijini Antalya, Mhe. Rais Dkt. Samia alishiriki katika Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP31), pamoja na mikutano ya pembezoni ya Ngazi za Juu kuhusu masuala ya Nishati Safi ya Kupikia. Aidha, tarehe 12 Novemba, 2026, Mhe. Rais Dkt. Samia alikutana na kuzungumza na Mhe. Recep Tayyip ErdoÄŸan, Rais wa Jamhuri ya Uturuki.