MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa ameshuhudia wanachama 24 wa vyama vya CUF na ACT-Wazalendo wakirejea CCM ndani ya siku mbili. Mheshimiwa Majaliwa alishuhudia wanachama hao wakikabidhi kadi zao kwa Katibu wa CCM wa Wilaya ya Ruangwa, Bw. Abbas Mkwenda (Agosti 23 na 24, 2024) wakati akizungumza na wakazi wa vijiji vya Mtondo (Kata ya Nambilanje) na Namikulo (Kata ya Chunyu), wilayani Ruangwa, Lindi ambako alifanya ziara ya jimboni kwake. Katika kijiji cha Mtondo, wanachama tisa wa CUF walirejesha kadi zao wakiongozwa na Mzee Bakari Abdallah Nanyambo ambaye alikuwa Mwenyekiti wa CUF Kata ya Nambilanje. Wengine ni Abdallah Ally Manjawila, Bakari Ally Nyanga, Bakari Abdallah Nampota, Mwanahawa Abdallah Komaje, Zaituni Omary Mitachi, Mwanahawa Rashid Chomwingo, Somoe Omary Mkupete na Amina Musa Pachela. Katika kijiji cha Namikulo, wanachama watano wa ACT-Wazalendo walikabidhi kadi zao wakiongozwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT Kata ya C...