Skip to main content

Posts

Showing posts from June 7, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

TAKUKURU YAFICHUA MRADI WA SHULE ULIOKWAMBA KWASABABU YA NeST

 NA MASHAKA MHANDO, Tanga TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Tanga, imefichua kukwama kwa miaka miwili kwa mradi wa madarasa na vyoo katika Shule ya Sekondari Chongoleani Jijini Tanga. Mradi huo wa thamani ya Sh. 93,816,506, ulishindwa kuanza utekelezaji tangu fedha zilipotolewa Machi 4, 2024 kutokana na kasoro kubwa za kiutawala na mfumo wa manunuzi wa halmashauri ya Jiji la Tanga. Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Tanga, Ramadhani Ndwata, aliwaambia waandishi wa Habari ofisini kwake Leo Juni 8 2026 wakati wa kutoa taarifa ya utendaji wa robo ya kwanza ya mwaka (Januari–Machi, 2026), ambapo alisema uingiliaji kati wa taasisi hiyo umeokoa hasara ya jumla ya Sh. 116,216,506 katika sekta ya elimu.  Uchunguzi wa TAKUKURU ulibaini kuwa, makadirio ya bei ya vifaa vya ujenzi wa madarasa hayo mawili yalikuwa chini ya bei halisi ya soko, hali iliyosababisha mfumo wa manunuzi wa kielektroniki wa Serikali (*NeST*) kukataa zabuni zote na kukwamisha maendeleo ya wanafunzi ...

SERIKALI YAINGIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO NA DIT KUIMARISHA USIMAMIZI WA MAAFA

 Na, mwandishi wetu – Dar es Salaam SERIKALI kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) imeingia Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) na Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) yenye lengo la kuimarisha usimamizi wa maafa nchini kwa kutumia sayansi, teknolojia na ubunifu. Akizungumza mapema hii leo (08 Juni, 2026) katika hafla ya utiaji saini wa makubaliano hayo Katibu Mkuu wa ofisi hiyo, Dkt. Jim Yonazi, amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kujenga mifumo madhubuti ya kiutendaji inayoongozwa na maarifa, sayansi na teknolojia ikiwemo matumizi ya Akili Unde (AI) katika kukabiliana na maafa. Amesema makubaliano hayo yanatekeleza pia mapendekezo ya Mkutano wa Nane wa Umoja wa Mataifa wa Jukwaa la Dunia la Upunguzaji wa Vihatarishi vya Maafa uliofanyika Geneva, Uswisi, mwezi Juni 2025, na yanaashiria mabadiliko ya kimkakati katika namna Serikali inavyoshughulikia changa...

BENKI YA AZANIA YATANGAZA GAWIO LA SHILINGI 98.62 KWA KILA HISA

 Benki ya Azania imeidhinisha gawio la jumla ya shilingi bilioni 18.36 katika Mkutano Mkuu wa 33 wa Wanahisa (AGM) uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro. Gawio hilo la shilingi 98.62 kwa kila hisa linawakilisha asilimia 30 ya faida baada ya kodi ya shilingi bilioni 61.4 ambayo Benki ilipata katika mwaka wa fedha ulioishia Desemba 2025, ikionesha dhamira ya Benki ya Azania kuendelea kutoa thamani endelevu kwa wanahisa wake na kujenga msingi imara wa ukuaji kwa miaka ijayo. Mkutano huo uliwakutanisha Wanahisa, Wajumbe wa bodi, menejimenti, Wadhibiti pamoja na wadau mbalimbali kujadili utendaji wa Benki na mwelekeo wake wa kimkakati, jambo linaloendelea kuonesha imani kubwa ya wawekezaji katika mustakabali wa taasisi hiyo. Akizungumza baada ya mkutano huo, Eng.Julius B. Ndyamukama - Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Azania alisema kuwa uamuzi wa kutoa gawio hilo unaakisi uimara wa kifedha wa Benki pamoja na dhamira yake ya kuendelea kuongeza thamani kw...

KIOO LIMITED YATOA MSAADA WA VIFAA VYA MILIONI 150 KWA SHULE MKURANGA

 Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya KIOO Limited imetoa misaada mbalimbali kwa shule za Msingi na Sekondari Mkuranga Mkoa wa Pwani zinazofikia shilingi milioni 150 kwa mwaka jana kama sehemu ya mpango wake wa kusaidia jamii wa (Cooperate Social Responsibility (CSR). Mwishoni mwa wiki kampuni hiyo ilikabidhi mashine za kurudufia karatasi na kompyuta kwa shule za sekondari za Msorwa na Malela zilizoko Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani zenye thamani y ash milioni nane. Vifaa hivyo vilikabidhiwa mwishoni mwa wiki na Mshauri wa Masuala ya Usalama, Afya na Mazingira wa Kioo Limited, Richard Msumule, wakati wa hafla iliyohudhuriwa na Ofisa Elimu Msingi wa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, Jessy Mpangala. Akizungumza mara baada ya kutoa msaada huo, Richard Msumule alisema katika mpango wake wa CSR, Kioo Limited imekuwa ikikarabati madarasa, ofisi za walimu na kujenga visima vya maji. Alisema kampuni hiyo imekuwa ikiwajengea miradi ya nishati safi ya gesi, majiko ya gesi, kuwanunulia kompyuta na ...

MAKUBALIANO MANANE YA KIMKAKATI: RAMANI MPYA YA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI KATI YA TANZANIA NA URUSI YAFUNULIWA

 Na Mwandishi Wetu, TBN, Dar es salaam Mikataba na hati za makubaliano manane (8) zilizosainiwa kati ya Tanzania na Urusi, ndizo zilizoweka msingi mkuu wa ushirikiano mpya wa kiuchumi, kijamii na kiteknolojia unaotarajiwa kupandisha hadhi ya nchi hizi mbili.  Makubaliano haya makubwa, ambayo ni matunda ya moja kwa moja ya ziara ya kihistoria ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini Urusi, yanajenga daraja imara la maendeleo katika sekta tisa za kipaumbele: kilimo, elimu, nishati, madini, viwanda, utalii, usafirishaji, uchumi wa kidijiti, pamoja na biashara na uwekezaji. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, ameanika hadharani undani wa makubaliano hayo manane yanayobeba mustakabali wa nchi: Kutoka Diplomasia ya Lugha Hadi Mapinduzi ya Afya na Elimu ya Juu Katika makubaliano ya kwanza, Tanzania na Urusi zimeamua kutumia lugha kama silaha ya kidiplomasia. Kupitia hati ya ushirikiano kati ya Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) na Chuo Kikuu cha M...

DAKIKA TATU ZA DHAHABU ZA RAIS SAMIA URUSI ZAFUNGUA MILANGO YA SHILINGI TRILIONI 5

 Na Mwandishi Wetu, TBN, Dar es salaam Ziara ya kihistoria ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini Urusi imeendelea kuzaa matunda makubwa baada ya Serikali kutangaza kuwa kampuni kubwa za nchi hiyo zimeonesha nia thabiti ya kuwekeza kiasi cha Dola za Marekani bilioni mbili (sawa na Shilingi za Kitanzania trilioni tano) ndani ya miaka mitatu ijayo.  Uwekezaji huu mkubwa unalenga kimkakati sekta tano kuu za kipaumbele, huku ukichangiwa kwa kiasi kikubwa na ushawishi wa kipekee wa Rais Samia kiuchumi. Akitolea ufafanuzi mafanikio hayo, Mkurugenzi wa Biashara ya Kimataifa na Diplomasia ya Uchumi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi John Ulanga, alifichua siri ya mafanikio hayo kuwa ni "dakika tatu za dhahabu" alizopewa Rais Samia kuzungumza katika Jukwaa la Uchumi la Kimataifa la Petersburg nchini Urusi.  Kupitia ubunifu na maono yake makubwa, Rais alitumia muda huo mfupi kwa umahiri mkubwa kutangaza fursa za Tanzania, hatua iliyoziteka akili za miamba ya biashara nchini Urusi na...

JINSI ZIARA YA RAIS SAMIA NCHINI URUSI ILIVYOTEKA FIKIRA ZA KIDIPLOMASIA DUNIANI

 Na Mwandishi Wetu, TBN, Dar es salaam Katika ulimwengu wa diplomasia ya kimataifa, kuna matukio yanayobadilisha mwelekeo wa upepo wa kiuchumi, na ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini Urusi imeandikwa kama mojawapo ya matukio hayo.  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, amebainisha kuwa safari hiyo ya kihistoria kuanzia Juni 3 hadi 5, mwaka huu, imeleta "mtikisiko chanya" kote duniani, ikionyesha nafasi ya kipekee ya Tanzania kama lango kuu la bara la Afrika. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Balozi Kombo alifafanua kuwa mshtuko huu wa kidiplomasia unatokana na ukweli kwamba, hakuna nchi nyingine ya Afrika iliyowahi kufanya ziara ya kimkakati ya namna hiyo nchini Urusi katika muktadha wa sasa. "Dunia nzima ina watu bilioni 7.5; Urusi anafanya biashara na watu bilioni 6. Ni bilioni 1.5 tu ndio waliomwekea vikwazo. Katika kutanua uchumi wake Afrika, Urusi inaiangalia Tanzania kama kiungo muhimu za...

MV LIEMBA SETS RECORDS FOR DMG AS FIRST CLASS SHIP BUILDER IN AFRICA

By Staff Writer  The _Forbes Africa_ ha has recognised Dar es Salaam Merchant Group (DMG) as Tanzania's class one shipbuilding capability which redefines 'made in Tanzania'. *A key reason for the recognition was DMG’s successful reconstruction of MV Liemba - the world’s oldest operating passenger ship at 115+ years* - a project that proved Tanzania can restore and operate heritage vessels to modern safety and performance standards. However, the _Forbes Africa_ dedicated pages 20-21 of its June/July 2026 “Africa’s New Blueprint for Growth: Tanzania” edition to DMG wasn’t just celebrating a company. It was announcing a shift. Tanzania had entered the Class One shipbuilding league - a club previously held by only two countries in Africa. The feature titled _“Tanzania’s Class One Shipbuilding Capability”_ profiles DMG as a homegrown, multi-sector conglomerate delivering multi-million-dollar contracts while managing national maritime strategy. The numbers alone demand attention:...