Skip to main content

Posts

Showing posts from February 2, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Magari 150 ya Zimamoto yanunuliwa Na Kusambazwa Nchi Nzima: Bashugwa

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amesema kuwa Serikali inaendelea kuliimarisha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kulipatia vitendea kazi ambapo sasa inatekeleza mradi wa ununuzi vifaa mbalimbali vya kuzima moto na uokoaji pamoja na magari 150 ya kuzima moto na uokoaji. Bashungwa ameeleza hayo tarehe 03 Februari 2025 wakati akijibu swali la Mbunge wa Ngorongoro, Emmanuel Shangai aliyetaka kujua Je, lini Serikali itanunua gari la Zimamoto Wilaya ya Ngorongoro. “Kwa sasa Serikali inatekeleza mradi wa ununuzi vifaa mbalimbali vya kuzima moto na uokoaji pamoja na magari 150 ya kuzima moto na uokoaji” amesema Bashungwa Amesema pindi magari 150 ya kuzima moto na uokoaji yatakapofika nchini, yatakayosambazwa nchi nzima ikiwemo Wilaya ya Ngorongoro.  Aidha,  amesema Serikali inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan imeshaliwezesha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kununua magari 12 ya kisasa ambapo moja wapo lilitumiaka kuzima moto katika jengo gorofa la TRA Kariako...

Mahakama Kuu Kanda ya Musoma imesema Kwa Sasa imepunguza Mgogoro Mingi ya Ardhi

 Na Ada Ouko, Musoma. MAHAKAMA kuu kanda ya Musoma mkoani Mara imefanikiwa kupunguza ucheleweshwaji wa mashauri yanayotokana na migogoro ya ardhi kwa kufuata sheria na utaratibu unaosimamiwa na mabaraza ya ardhi na nyumba nchini. Hayo yamebainishwa february mosi mwaka huu 2025 na Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo Fahamu Mtulya, mara baada ya kumaliza kikao chake cha majumuisho na wadau mbalmbali wa sheria waliokuwa wakitoa elimu kwa jamii ikiwa ni moja kuelekea kumaliza wiki ya sheria wilayani hapa. "Suala hili tumeligundua tangu mwaka jana 2024, na tukumbuke kuna msemo wa kisheria ambao unajulikana kwa wengi unaosema haki ikichelewa ni kama haki iliyonyimwa".amesema . Amesema katika Halmashauri ya Musoma kuna mwenyekiti wa baraza la nyumba na ardhi mmoja sambamba na wilaya za Serengeti na Tarime hali inayopelekea gharama ya kuwalipa na kugharamia ujio endapo amri ya Mahakama kama haitaki Mwenyekiti wa Baraza la Musoma kusikiliza shauri hilo tena, na kwamba bajeti mara nyingi h...

Balozi Dkt Nchimbi Afika Ubalozi Wa Tanzania Nchini Ethiopia

 KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia, mjini Addis Ababa, alipotembelea ofisini hapo wakati wa ziara yake ya kikazi nchini humo. Kulia kwa Balozi Nchimbi ni Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Mhe. Innocent Eugene Shiyo na kushoto kwake ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) - Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ndugu Rabia Abdalla Hamid.

Jwtz imesema Licha ya Kupoteza Askari Wawili Nchini Drc,Vikundi Vyote Vya Jwtz Vipo Salama na Imara

Dkt. Masika aridhishwa Utekelezaji Mradi wa Membe

 📍 *NIRC Dodoma*   Mwenyekiti Bodi ya Uongozi Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Dkt. Richard Masika ameeleza kuridhishwa kwake utekelezaji miradi ya Umwagiliaji ikiwemo mradi wa ujenzi bwawa la Umwagiliaji la Membe lililopo wilayani Chamwino mkoani Dodoma.   Dkt. Masika ametoa kauli hiyo mara baada ya kufanya ziara katika bwawa hilo ambapo kwa sasa ujenzi wake umefikia asilimia 86 ya utekelezaji wa mradi. Aidha Dkt. Masika ametoa wito kwa wakulima ambao ni wanufaika wa mradi huo kutoa ushirikiano kwa wataalamu wanaotekeleza mradi wakati wa ujenzi na mara baada ya  kukamilika kwake ili kuhakikisha unaleta tija inayokusudiwa.   Sanjari na hayo Dkt. Masika ameielekeza Tume kuhakikisha katika utekelezaji wa mradi huo  unazingatia muda pamoja na thamani ya Dedham.   Akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Mkurugenzi Idara ya Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini Dkt. Consolatha Kapinga amekiri kupokea maelekezo ya Mwenyekiti hu...

Serikali na Bunge Zaipongeza Benki ya Azania

 WAZIRI mkuu Kassim Majaliwa na bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania,wameipongeza Azania benki kwa mchango wake mkubwa katika jamii hasa kwa kukubali kudhamini tamasha la Bunge bonanza linalofanyika ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan za kupambana na magonjwa yasioambukiza. Wa kwanza kutoa pongezi hizo ni wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembea mwendo wa kilometa tatu na kushuhudia michezo mbalimbali,waziri mkuu Kassim Majaliwa,amesema kuwa benki ya Azania imeonyesha kwa vitendo kuunga mkono juhudi za Rais Samia kwa kukubali kudhamini bonanza hilo kubwa. Amesema uamuzi wa benki ya Azania kudhamini bunge kufanya bonanza hilo kubwa imeonesha wazi upendo wa benki hiyo wa kujali afya za watanzania na kwamba kufanya hivyo ni kuunga mkono juhudi za Rais Samia katika mapambano ya magonjwa hayo yasio ambukiza. Amesema kuwa azania benki ni moja ya taasisi kubwa ya fedha nchini na imekuwa ikijitokeza kudhamini michezo mbalimbali h...