Skip to main content

Posts

Showing posts from August 12, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Polisi Kagera Yawashikilia Watu Watano

Na Angela Sebastian -Bukoba  Jeshi la polisi mkoani Kagera linawashikilia watu watano baada ya kukutwa na mashine 12 zinazotumika kwenye boti za kuvulia samaki na pikipiki sita ambazo wanadai ni mali za wizi ambazo ziliibiwa sehemu mbalimbali mkoani humo. Kamanda wa jeshi hilo Blasius Chatanda alieleza hayo jana wakati akiongea na vyombo mbalimbali vya habari katika viwanja vya ofisi za jeshi hilo mkoa mjini Bukoba, ambapo alisema waliweza kukamata vifaa hivyo kutokana na operesheni saka waalifu iliyofanyika ndani ya ziwa victoria na maeneo yote ya mkoa huo. "Operesheni ilinza mwezi Juni  mpaka Agosti 11 mwaka huu ambapo tulianzia ziwa victoria  baada ya kupata taatifa ya uwepo wa wizi wa mashine zinazotumika kwa ajiliya kuvua samaki (Engene bort) kutoka kwa baadhi ya wananchi hususani wavuvi ambapo tumezikamatia mikoa ya Bariadi na Mara ambapo wamo walioiba na wanunuzi wa mali hizo za wizi"alieleza kamanda. Wakati huo huo jeshi hilo linaendelea na ufuatiliaji wa tukio la...

Waziri Kombo Kushiriki Mkutano wa Mawaziri wa SADC, HARARE

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amewasili Harare, Zimbabwe kushiriki Mkutano wa Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika tarehe 13 na 14 Agosti, 2024 Mkutano huo wa Mawaziri ni sehemu ya mikutano ya awali kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano wa 44 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya hiyo utakaofanyika tarehe 17 Agosti, 2024 nchini Zimbabwe. Mkutano wa Mawaziri ulitanguliwa na kikao cha Makatibu Wakuu wa SADC kilichofanyika tarehe 8 hadi 11 Agosti, 2024 nchini humo ambacho kilijadili na kufanya maandalizi ya nyaraka mbalimbali zitakazo pokelewa na kujadiliwa na mkutano huo wa Mawaziri. Baada ya kuwasili nchini Zimbabwe, Mhe. Kombo amepokelewa na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe. Balozi IGP (RTD) Simon Sirro na kufanya kikao na ujumbe wa Tanzania unaoshiriki katika mikutano ya maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC. Mawaziri wengine watakaos...

Viongozi wa Kata na Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii Wapatiwa Elimu ya Kujikinga na Maradhi Mtambuka

NA WAF, Kilimanjaro Viongozi wa Kata na Wahudumu wa afya ngazi ya jamii, wapatao 170 wamepatiwa elimu ya kujikinga na maradhi ili  kuisaidia jamii kuepukana na maradhi mtambuka na kuwa na afya njema. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel Agosti 11, 2024 wakati wa  mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi hao mkoani Kilimanjaro. Dkt. Mollel amesema kuwa  ni muhimu kwa viongozi wa kata na wahudumu wa afya ngazi ya jamii kushirikiana ili kuhakikisha usalama wa afya za wananchi kwenye maeneo yao zinaimarika. Awali akifungua mafunzo hayo Naibu Waziri Ofisi ya Waziri mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe Ummy Nderiananga amewaasa viongozi na watumishi hao kuibua kwa Pamoja ikiwa kuna wagonjwa waliofichwa ndani ama walemavu kwani wote wanahaki ya kupata huduma za afya. “Viongozi wa Kata na wahudumu wa afya ngazi ya jamii mna jukumu la kuwaibua watu  waliofichwa, ili wapate msaada”. Amesema Mhe. Nderiananga. Kwa Upande wake mkurugenzi wa operesheni na programu kuto...

Serikali Yapunguza Rufaa za Matibabu Nje ya Nchi Kwa Asilimia 97

Serikali kupitia wizara ya afya imepunguza rufaa za nje ya nchi kwa asilimia 97 ikiwa ni matokeo ya uwekezaji uliofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan. Hayo yamesemwa Agosti 11, 2024 Mkoani Kilimanjaro na Naibu waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel wakati wa mafunzo kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii na viogozi wa kata 170 katika kukabiliana na magonjwa mbalimbali. Aidha Dkt. Mollel amesema kuwa Serikali imewekeza teknolojia ya kisasa katika Hospitali zote nchini ikiwa ni kutekeleza uboreshaji wa huduma za afya kwa jamii ili kila mwananchi apate huduma bora za afya. "Tumepunguza rufaa za nje kwa asilimia 97, wanaokwenda nje kwa ajili ya matibabu ni asilimia 3 huu ni uwekezaji mkubwa uliofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais Wetu ameleta hospitali nzuri na vifaa tiba vya kutosha ili kuleta huduma bora kwa wananchi". Amesema Dkt Mollel.

Ujenzi wa Daraja la Magufuli Wafikia Asilimia 90 ya Utekelezaji

Mwonekano wa Ujenzi wa Daraja la  John Pombe Magufuli (Kigongo - Busisi) Kilometa 3.2 linalojengwa kuunganisha Barabara Kuu ya Usagara - Sengerema - Geita kupita Ziwa Victoria Mkoani Mwanza na ujenzi wa barabara unganishi ya Kilometa 1.66 utekelezaji unaendelea na upo asilimia 90. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya  Ujenzi Kupitia mtandao wa X zamani uliokua unajulikana kama (twitter) inaeleza kuwa mradi huo unagharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania kwa shilingi Bilioni 716.3 zikijumuisha Malipo ya Mkandarasi, Mhandisi Mshauri wa usimamizi wa mradi, Fidia na Usanifu.         (Picha Kwa Hisani ya Wizara ya Ujenzi)