MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, amewataka wakazi wa Kambi ya Samaria iliyopo Hombolo kulinda na kutunza miundombinu ya huduma za kijamii iliyojengwa kupitia mradi wenye thamani ya shilingi milioni 69.9, ili iweze kudumu na kuendelea kuwanufaisha kwa miaka mingi ijayo. Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi miradi ya maji, umeme na majiko banifu iliyotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhe. Senyamule alisema jukumu la kutunza miundombinu hiyo sasa liko mikononi mwa wanufaika. "Miradi hii imewekwa na inahitaji kutunzwa. Tumeshawekewa umeme, kazi ya kutunza balbu ni yetu, si ya REA tena. Tumewekewa maji karibu na makazi yetu, kazi ya kutunza koki ni yetu, si ya STAMICO tena. Ilindeni na kuitunza miundombinu yote mlioletewa kwa sababu thamani yetu ni kuitunza," alisema. Aidha, aliwahimiza wakazi wa kambi hiyo kutumia huduma hizo kujiongezea kipato kupitia shughuli za uzalishaji, hususan ki...
Marato tv - Sauti ya Jamii