Skip to main content

Posts

Showing posts from November 10, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Makusanyo ya Madini Simiyu Yavuka Malengo, Yafikia Zaidi ya Asilimia 103

📍Simiyu AFISA Madini Mkazi wa Mkoa wa Simiyu, Mayigi Makolobela, amesema mkoa huo umeendelea kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato yatokanayo na Sekta ya Madini, ambapo makusanyo ya robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2025/2026 yamevuka malengo kwa kufikia zaidi ya asilimia 103 ya lengo lililowekwa kwa kipindi husika. Akizungumza mkoani Simiyu, Makolobela amesema kwa mwaka wa fedha uliopita, ofisi yake ilipewa lengo la kukusanya Shilingi bilioni 4, lakini walifanikiwa kukusanya zaidi ya Shilingi bilioni 4.5.  “Kwa mwaka huu wa fedha tumewekewa lengo la kukusanya Shilingi bilioni 4.76, na hadi kufikia robo ya kwanza tayari tumekusanya zaidi ya Shilingi bilioni 1.23, sawa na asilimia 103 ya lengo la robo mwaka,” amesema Makolobela. Ameongeza kuwa tangu kuanza kwa Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, makusanyo ya madini kupitia wachimbaji wadogo mkoani humo yamefikia zaidi ya Shilingi bilioni 17, hatua inayodhihirisha ukuaji na uimara wa sekta hiyo katika Mko...

Taju Yalaani Vikali Vurugu katika Kuhatarisha Amani

 Taasisi ya Tanzania Jumuishi (TAJU) imelaani vikali vitendo vya baadhi ya watu waliosababisha vurugu na kuharibu mali pamoja na kuikosesha amani jamii ya watu wenye ulemavu nchini. Hayo amebaisha mapema hii leo novemba 10, 2025, jijini Dar es salaam, Katibu wa Taasisi hiyo ya Tanzania Jumuishi (TAJU), Innocent Gabriel Siriwa, katika mkutano wa taasisi hiyo na vyombo vya habari  ambapo pia imevikumbusha vyama vya siasa na viongozi wa dini kutumia nafasi zao vizuri ili kulinda na kuhubiri amani nchini.  Aidha, Innocent  amesema (TAJU) Inapinga vikali  wote wanaounga mkono kwa kusema kuwa kudai haki kwa njia ya amani hakuwezi kufanikisha upatikanaji wa haki huku ikiwataka watanzania kufuta mtazamo huwo kwani hauna tija na ni wa wakati wa ukoloni Pia, amesema ili kulinda amani ya taifa la tanzania inapaswa watanzania kuacha kuiga mataifa madogo yanayofanya vurugu bila ufumbuzi wa matatizo ya kama Madagascar ikiwa pamoja na kutumia mitandao kuchagua mema na kuacha m...

SENDIGA AZINDUA MRADI WA USAMBAZAJI NA UUZAJI WA MAJIKO BANIFU KWA BEI YA RUZUKU MANYARA* .

📌 *Majiko banifu 7,914 kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku* .   📌 *Jiko moja kuuzwa kwa bei ya ruzuku ya TZS 11,200* . 📍 *MANYARA*  Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mheshimiwa Queen Sendiga, leo Novemba 10, 2025 amezindua rasmi mradi wa kutuma na kutuma ujumbe kwa bei ya ruzuku mkoani Manyara. Uzinduzi huu ni sehemu ya mkakati wa kutafuta mkakati wa kitaifa wa kufikia na matumizi ya matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia. Aidha,uzinduzi huu umefanyika katika Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Manyara iliyopo wilaya ya Babati, ambapo jumla ya majiko banifu 7,914 yatauzwa na kusambazwa kwa bei ya ruzuku ya kiasi cha TZS 11,200 ambayo ni sawa na aslimia 80 ya ruzuku ya TZS 56,000 ambayo ni bei ya awali ya jiko. Sauti wakati wa Mheshimiwa, Mheshimiwa Sendiga amesema mpango huo umelenga kusaidia wananchi wote, hususani wa kipato cha chini, wanapata fursa ya kutumia nishati safi na salama ya kupikia kwa gharama nafuu. Aidha, amewaagiza Wakuu wa Wilaya yote mkoani Manyara ni kwa makini zo...

Waratibu wa Kitaifa wa Nchi za Jumuiya ya Ukanda wa Maziwa Makuu - Icglr Wakutana Jijini Kinshasa

Mkutano wa 20 wa Kawaida wa Waratibu wa Kitaifa wa Nchi za Jumuiya ya Ukanda wa Maziwa Makuu  (ICGLR) umefanyika tarehe 10 Novemba, 2025 jijini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo - DRC. Mkutano huo ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa 19 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje  (RIMC) pamoja na Wakuu wa Nchi na Serikali (SUMMIT) wa Jumuiya hiyo iliyopangwa kufanyika Novemba 13 na 15, 2025 mtawalia. Mkutano huo umefunguliwa na Waziri wa Ushirikiano wa Kikanda wa DRC, Mhe. Floribert Anzuluni Isiloketshi ambapo pamoja na masuala mengine, amewasihi waratibu hao kutumia mkutano huo kuja na mapendekezo yatakayoboresha utendaji kazi wa Sekretarieti ya Maziwa Makuu ili iweze kutekeleza kwa ufanisi zaidi majukumu yake ya msingi, ikiwemo kuleta amani, usalama na maendeleo katika nchi 12 Wanachama wa Jumuiya hiyo. Tanzania ikiwa moja ya nchi waasisi wa ICGL, inashiriki mkutano huo kikamilifu ambapo Mratibu wa Kitaifa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Afrika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na...

Engineer Lwamo Urges Staff to Embrace Regular Exercise for Better Health at Work

Dodoma The Executive Secretary of the Mining Commission, Engineer Ramadhani Lwamo, has called on Commission employees to adopt a culture of regular physical exercise as a key measure to prevent chronic diseases and the spread of HIV/AIDS in the workplace. Engineer Lwamo made the remarks while opening a two-day peer educator training organized by the Mining Commission in Dodoma, aimed at raising awareness among staff on HIV, AIDS, and non-communicable diseases (NCDs). He emphasized that good physical and mental health is essential for productivity and effective performance, noting that many health challenges today stem from unhealthy lifestyles, poor eating habits, lack of exercise, and risky sexual behaviors. “A healthy body and mind are the foundation of effective performance. Each of us has a responsibility to protect ourselves and lead a healthy lifestyle,” said Engineer Lwamo. He further underscored the importance of integrating workplace health strategies into annual institutional...

Mhandisi Lwamo: Mazoezi ni Kinga ya Afya Kazini

Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo, amewataka watumishi wa Tume kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi ya mwili mara kwa mara na kuepuka tabia zinazoweza kusababisha magonjwa sugu na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU). Mhandisi Lwamo ametoa wito huo Novemba 10, 2025, wakati akifungua mafunzo ya waelimisha rika wa Tume ya Madini yanayofanyika jijini Dodoma. Amesema lengo la mafunzo hayo ni kuongeza uelewa miongoni mwa watumishi kuhusu VVU, Ukimwi na magonjwa yasiyoambukiza, ili kulinda afya zao na kuboresha ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku. “Afya bora ya mwili na akili ni nguzo muhimu ya utendaji kazi wenye tija. Magonjwa mengi tunayokabiliana nayo leo yanatokana na mitindo ya maisha, ulaji usio sahihi, kutofanya mazoezi na tabia hatarishi za ngono. Ni jukumu letu kila mmoja kuhakikisha tunajilinda na kuishi kwa afya,” amesema Mhandisi Lwamo. Aidha, amesisitiza umuhimu wa waajiri kujumuisha mikakati ya afya kazini kwenye mipango ya kila mwaka...