Skip to main content

Posts

Showing posts from August 12, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Samia achangisha mabilioni ya fedha kwa ajili ya kampeni za CCM

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan akiongoza viongozi, wanachama, wapenzi, wakereketwa wa CCM na Watanzania wapenda maendeleo katika harambee ya kuchangisha fedha, iliyolenga kukusanya kiasi cha shilingi Bilioni 100 kwa ajili ya kampeni za CCM za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025,hafla hiyo inaendelea katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar Es Salaam.

Watanzania Tusikubali Uchaguzi Utugawe - Dkt. Biteko

📌 Asema Kuna Maisha baada ya Uchaguzi  ðŸ“Œ Amwakilisha Rais Samia,miaka 40 Kanisa Anglikana Dayosisi ya Kagera 📌 Rais Samia achangia Tsh. Milioni 50 Ujenzi wa Kanisa Dayosisi ya Kagera 📌 Anglikana Waishukuru Serikali, washirika wa maendeleo Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka Watanzania kuwapima wagombea wa nafasi mbalimbali  katika Uchaguzi Mkuu ujao na kuchagua kwa haki ifikapo tarehe 29 Oktoba 2025 (mwaka huu) na katu wasikubali Uchaguzi uwagawe. Dkt. Biteko amesema hayo Agosti 12, 2025 wakati akimwakilisha Mheshimiwa Rais katika Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 40 ya Kuzaliwa kwa Dayosisi ya Kagera iliyofanyika katika Viwanja vya Kanisa Kuu Yohana Mbatizaji - Murgwanza, Ngara. Amesema kuwa watanzania wanayo haki ya kuwapima wagombea kwa matendo yao na hatimaye kutenda haki kwa kufanya uchaguzi wao kwa njia ya demokrasia huku akisisitiza umuhimu wa kuzingatia kampeni za kistaarabu na kuj...

Ukombozi wa kiuchumi ni safari ndefu, SADC yakumbushwa

Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) zimekumbushwa kuwa ukombozi wa kiuchumi ni safari ndefu na ili kuifikia nchi hizo zinahitaji  mtangamano wenye nguvu na usioyumbishwa katika utekelezaji wa malengo waliyojiwekea.  Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara za Kimataifa wa Zimbabwe, Prof. Amon Murwira kabla ya kukabidhi uenyekiti wa Baraza la Mawaziri la SADC kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Madagascar, Mhe. Rasata Rafaravavitafika jijini Antananarivo Agosti 12, 2025. Katika Kikao hicho cha Baraza la Mawaziri, Tanzania inawakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo na moja ya agenda inayojadiliwa ni maandalizi ya Mkutano wa 45 wa Wakuu wa Nchi wa SADC uliopangwa kufanyika Agosti 17, 2025. Prof. Murwira amesema safari yoyote haikosi changamoto na kutumia jukwaa hilo kuwatahadharisha washiriki wa Mkutano huo kuwa,  changamoto zisiwe sababu za kutofikiwa kwa malengo mazuri yaliyoanzisha SADC. ...