DODOMA: Programu ya Mifumo Himilivu ya Chakula Nchini (TFSRP-P4R) imeanza kuleta matokeo chanya kwa wakulima wadogo nchini Tanzania, baada ya kuongeza uzalishaji wa zao la mpunga kutoka wastani wa tani mbili hadi kufikia tani nane kwa ekari, kufuatia ukarabati na uboreshaji wa miundombinu ya umwagiliaji. Mafanikio hayo yamebainishwa wakati wa kikao cha tathmini ya utekelezaji wa programu hiyo kilichofanyika katika Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), jijini Dodoma, chini ya uongozi wa Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo, Bw. Raymond Mndolwa. Kikao hicho kimewakutanisha wadau wa maendeleo wanaoshirikiana katika utekelezaji wa programu hiyo, wakiwemo wawakilishi wa Benki ya Dunia (WB), Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Kilimo (IFAD) na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Japan (JICA). Kupitia programu hiyo, jumla ya skimu 84 za umwagiliaji nchini zimeingizwa katika mfumo rasmi wa usimamizi na matunzo shirikishi, unaowezesha wakulima wadogo kushiriki moja kwa moja katika ...
Marato tv - Sauti ya Jamii