WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema ndani ya wiki moja, Serikali itachukua hatua ya kuhakikisha bei ya saruji inakuwa himilivu kwa wananchi, baada ya kubaini malalamiko ya kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Simiyu. Ametoa kauli hiyo jana (Jumanne, Septemba 15, 2026) wakati akizungumza na wananchi wa Bariadi Mjini, mkoani Simiyu katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya CCM Saba Saba. “Serikali tumeliona hilo. Serikali sikivu tumesikia hilo. Nimewatuma wataalamu ndani ya wiki moja wawe wameshapata ufumbuzi. Tutatoa tamko la njia ya kushusha bei ya saruji ili kila Mtanzania aweze kumudu. Katika baadhi ya maeneo bei ya saruji imefikia zaidi ya sh. 26,000 na katika baadhi ya mikoa ya mipakani imefikia sh. 32,000,” amesema na kusisitiza kuwa Serikali inataka wananchi waweze kumudu gharama za ujenzi wa nyumba na miradi mingine ya maendeleo. Kuhusu zao la pamba, Waziri Mkuu amesema ameielekeza Wizara ya Kilimo ikutane na wadau wa pam...
Marato tv - Sauti ya Jamii