Skip to main content

Posts

Showing posts from May 18, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Serikali Kuendelea Kuboresha Vituo vya Maarifa Nchini

Na, Mwandishi wetu - Pwani SERIKALI kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) imeeleza dhamira yake ya kuendelea kuboresha Vituo vya Maarifa nchini, hususan vile vinavyotoa huduma kwa madereva wa malori ya masafa marefu kuhusu masuala ya VVU na UKIMWI. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Dkt. Jim Yonazi mapema mwanzoni mwa wiki mara baada ya kutembelea na kukagua Vituo vya Maarifa vinavyotoa huduma za VVU na UKIMWI kwa madereva wa malori ya masafa marefu vilivyopo eneo la Kurasini  katika wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam na Mdaula mkoa wa Pwani ambayo Vituo hivyo vipo chini ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS). Dkt. Yonazi amesema Serikali, kupitia Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), ina jukumu la kusogeza huduma muhimu za VVU na UKIMWI karibu na wananchi. “Vituo hivi vina mchango mkubwa katika kuwafikia madereva wa masafa marefu ambao mara nyingi hukaa safarini kwa muda mrefu. Serikali itaendelea kuviboresha hususan...

Mwili wa Baharia Mtanzania Aliyefariki Uae Wawasili Nchini

Mwili wa Baharia Mtanzania, Bw. Mchama Maregesi Mongu, aliyefariki dunia akiwa kazini nchini Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), umewasili nchini Mei 18, 2026 kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam. Mwili huo ulipokelewa na viongozi wa Serikali, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu waliokuwepo uwanjani hapo. Baharia Mongu alifariki dunia Mei 3, 2026 baada meli ya kuvuta ya VOLANS (tug boat) aliyokuwa akifanya kazi kushambuliwa kwa bomu katika Mlango wa Bahari wa Hormuz ilipokuwa safarini kutoka UAE kuelekea Oman.  Akizungumza baada ya kupokea mwili huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Nahodha Mussa Mandia, ameishukuru Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia Konseli Kuu ya Tanzania - Dubai kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na kufanikisha taratibu zilizowezesha kuurejeshwa ngumbani nwa mwili wa marehemu Mongu. Nahodha Mandia pia ametoa rai kwa wamiliki wa vyombo vya...

Wizara ya Ulinzi na Jkt Yaliomba Bunge kuidhinisha Trillioni 4.2 kuimarisha Ulinzi na Teknolojia

SERIKALI kupitia Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa imesema itaendelea kuimarisha ulinzi na usalama wa Taifa kwa kuongeza uwekezaji katika zana za kisasa za kijeshi, teknolojia, mafunzo ya wanajeshi pamoja na upanuzi wa miundombinu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ili kuwapa vijana wengi zaidi mafunzo ya kijeshi na stadi za kazi. Kauli hiyo imetolewa na Dkt. Rhimo Nyansaho wakati akiwasilisha Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa mwaka wa fedha 2026/27 leo Mei 19, 2026 Bungeni Jijini Dodoma. Amesema katika mwaka wa fedha 2026/27, Wizara imepanga kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Mpango wa Nne wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano, Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030 (SDGs), pamoja na Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025. Katika bajeti hiyo, Serikali inatarajia kutumia jumla ya Shilingi trilioni 4.28 kwa matumizi ya kawaida na maendeleo, ambapo Shilingi trilioni 3.85 zimetengwa kwa matumizi ya kawaida huku zaidi y...

Dkt.Nyansaho:Hali ya Ulinzi na Usalama Mipakani ni Swari

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho amesema Tanzania imeendelea kuwa salama huku vyombo vya ulinzi na usalama vikiongeza nguvu katika kulinda mipaka ya nchi dhidi ya changamoto mbalimbali za kiusalama zinazojitokeza ndani na nje ya mipaka. Akiwasilisha Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa leo Mei 19, 2026 Bungeni jijini Dodoma, Dkt. Nyansaho amesema katika mwaka wa fedha 2026/2027 hali ya ulinzi na usalama katika mipaka yote ya Tanzania imeendelea kuwa shwari licha ya kuwepo kwa changamoto kadhaa ikiwemo uharibifu wa alama za mipaka, uchakavu wa barabara za ulinzi pamoja na migogoro ya ndani katika baadhi ya nchi jirani. Amesema mipaka ya Tanzania yenye urefu wa kilomita 5,923.41 inayojumuisha nchi kavu, anga na eneo la maji imeendelea kulindwa kwa umakini mkubwa kupitia operesheni, doria na ushirikiano wa karibu kati ya JWTZ na vyombo vingine vya usalama. Katika taarifa hiyo, Waziri huyo amesema mpaka wa Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia y...

Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jkt Mei 19-2026

 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho, akisalimiana na viongozi Mbalimbali Mara baada ya kuwasili Bungeni leo Mei 19, 2026 kwa ajili ya kuwasilisha Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa kwa mwaka wa fedha 2026/27.  Wasilisho hilo linatarajiwa kueleza vipaumbele vya wizara, utekelezaji wa shughuli mbalimbali za ulinzi na usalama pamoja na mipango ya maendeleo kwa mwaka wa Fedha 2026/2027 Viongozi ambao anasalimiana nao pichani ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt Faraji Kasidi Mnyepe Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jenerali Jacob Mkunda pamoja na viongozi wengine waandamizi.

Vyama Sita Vya Ukombozi Kusini Mwa Afrika Vyaanza Mafunzo Kibaha

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (Bara), Ndugu Stephen Wasira, amefungua rasmi mafunzo kwa vyama sita rafiki vya ukombozi kutoka kusini mwa Afrika. Mafunzo hayo yamefanyika leo, Mei 18, 2025, katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Leadership School, Kibaha Mkoa wa Pwani Vyama vinavyoshiriki ni Chama Cha Mapinduzi (CCM), ZANU-PF, African National Congress (ANC), SWAPO, FRELIMO, na MPLA.  Mafunzo haya yanalenga kuwajengea makada kutoka vyama hivyo sita uwezo wa kiuongozi, usimamizi, na kuendeleza tunu za harakati za ukombozi kusini mwa Afrika. #CCM #ZANUPF #ANC #SWAPO #FRELIMO #MPLA #Leadership #AfricanLiberationMovements #MwalimuNyerereLeadershipSchool ───

Vyama Sita vya Ukombozi Kusini Mwa Afrika Vyaanza Mafunzo Kibaha

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (Bara), Ndugu Stephen Wasira, amefungua rasmi mafunzo kwa vyama sita rafiki vya ukombozi kutoka kusini mwa Afrika. Mafunzo hayo yamefanyika leo, Mei 18, 2025, katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Leadership School, Kibaha Mkoa wa Pwani Vyama vinavyoshiriki ni Chama Cha Mapinduzi (CCM), ZANU-PF, African National Congress (ANC), SWAPO, FRELIMO, na MPLA.  Mafunzo haya yanalenga kuwajengea makada kutoka vyama hivyo sita uwezo wa kiuongozi, usimamizi, na kuendeleza tunu za harakati za ukombozi kusini mwa Afrika.