Skip to main content

Posts

Showing posts from February 28, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Wanawake ni nguzo muhimu kulea kizazi chenye maadili-DC Itunda

📍Awataka viongozi wa dini kuhubiri Umoja na mshikamano *NA MWANDISHI WETU, MBEYA* MKUU wa Wilaya ya Mbeya, *Mhe. Solomon Itunda*, ametoa wito kwa viongozi wa dini na jamii kwa ujumla kuimarisha vita dhidi ya mmomonyoko wa maadili, huku akisisitiza kuwa wanawake ni nguzo muhimu katika kulea kizazi chenye nidhamu na uzalendo nchini. Mhe. Itunda ametoa kauli hiyo Jumamosi, Februari 28, 2026, alipomwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, *Mhe. Beno Malisa*, katika ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la Wanawake wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) lililofanyika katika ukumbi wa VETA jijini Mbeya. Akihutubia washiriki wa kongamano hilo waliotoka katika mikoa zaidi ya 13 nchini, DC Itunda alisema Serikali ya Awamu ya Sita inatambua mchango wa kipekee wa wanawake katika kulinda misingi ya amani, maadili na hofu ya Mungu, mambo ambayo ni chemchemi ya ustawi wa Taifa. "Wanawake ni nguzo ya Taifa. Serikali inaendelea kuthamini ushirikiano na taasisi za kidini katika kukuza maadili na kuchochea maen...

Jasi Yatikisa Same

- Wachimbaji Waanzisha Mfuko wa Ukarabati wa Mazingira - Wakusanya Shilingi Bilioni 2.6 kwa Miaka Miwili 📍Same SHUGHULI za uchimbaji wa madini ya Jasi katika vijiji vya Ruvu Jiungeni na Makanya, wilayani Same mkoani Kilimanjaro, zimeendelea kushika kasi huku wachimbaji wadogo wenye leseni zaidi ya 200 wakiungana kuimarisha uzalishaji na usimamizi wa rasilimali hiyo muhimu kwa viwanda vya saruji na bidhaa nyingine za viwandani. Wachimbaji hao wameanzisha chama chao kwa lengo la kusimamia maslahi na kuratibu uendeshaji wa shughuli za uchimbaji, hatua inayotajwa kuongeza tija, uwajibikaji na mchango wa sekta hiyo kwa wanachama pamoja na jamii inayowazunguka. Katika kipindi cha takribani mwaka mmoja, wamefanikiwa kuweka mifumo ya pamoja ya usimamizi na udhibiti wa mapato. Akizungumza wilayani humo, Mhandisi Abel Madaha, Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Kilimanjaro anayesimamia wilaya za Same, Mwanga, Hai, Rombo, Siha na Moshi, amesema pamoja na fursa za kiuchumi zinazotokana na madini ...

Waziri Mkuu Ashiriki Mazishi ya Kardinali Pengo, Dar es Salaam

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Februari 28, 2026 ameshiriki mazishi ya Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Marehemu Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, yaliyofanyika katika Kanisa la Hija ya Bikira Maria – Pugu, jijini Dar es Salaam. Mazishi hayo yameongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi na kuhudhuriwa na viongozi wengine wa Serikali pamoja na viongozi wa dini mbalimbali.

Msimu wa Tatu wa Bunge Marathon yaja Kivingine

Msimu wa tatu wa Bunge Marathon umezinduliwa leo februari 27, 2027 katika Ofisi Ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam ambapo mwaka huu mbio hizo zinatarajiwa kufanyika Aprili 18 2026 Jijini Dodoma. Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mwenyekiti wa Maadalizi ya mbio hizo Mhe. Festo Sanga amesema mbio hizo ambazo zinaandaliwa kwa mara tatu, zinatarajiwa kuwakutanisha wanariadha zaidi ya 5,000 kutoka ndani na je ya Tanzania.  Amesema Lengo la kuendeleza mbio hizi ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita za kupambana na magonjwa yasiyoambukiza kwa kuimarisha afya kupitia michezo. Akizungumzia zawadi za washindi Mheshimiwa Sanga amesema zawadi katika msimu huu wa tatu zimeboreshwa zaidi ambapo kwenye nusu marathon yaani kilometa 21, mshindi wa kwanza atajinyakulia Milioni 6, mshindi wa pili atapata Milioni 3 na mshindi wa tatu akiambulia Milioni 1.5. Kwa upande wa kilomita 10, mshindi wa kwanza atazawadiwa shilingi milioni 3, mshindi wa pili Shilingi milioni 2, na mshindi wa ta...

Tume yakutana na mmiliki Mabasi ya Esther

Na Festo Polea DAR ES SALAAM:  TUME ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, Leo Februari 28 imekutana na mmiliki wa mabasi ya Esther, Joseph Didas.  Mahojiano hayo ya Tume na Didas yamefanyika katika Ofisi za Tume hiyo zilizopo Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini hapa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Tume kukusanya taarifa, maoni na ushauri kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa sasa, wastaafu. Katika mkutano huo wa Tume na Didas yamejadiliwa kwa kina namna matukio ya uvunjifu wa amani yalivyoanza, athari zake kwa wananchi, mali zao na miundombinu, pamoja na ushauri na mapendekezo ya namna ya kudhibiti na kuzuia matukio kama hayo yasijirudie siku zijazo. Hivi karibuni Mamlaka ya Uteuzi imeiongezea Tume muda wa siku arobaini na mbili (42) kuanzia tarehe 20 Februari, 2026 ili Tume iweze kukamilisha uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani ya wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa tarehe 29 Oktoba, 2025 na kuitak...

Rais Dkt Samia Azungumza na Katibu Mkuu wa EAC Ikulu Dar es Saalam

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) anayemaliza muda wake, Bi. Veronica Nduva, tarehe 28 Februari, 2026 Ikulu, Jijini Dar es Salaam. Pamoja na masuala mengine, Katibu Mkuu ambaye anamaliza muda wake alimshukuru Mheshimiwa Rais na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi chote cha kuhudumu kama Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo.

Mwekezaji Kiwanda cha Kuchakata Taka Amwaga Shukrani zake Kwa Serikali

 Na Angela Sebastian; Bukoba MKURUGENZI wa kiwanda cha kuchakata taka za plastiki pamoja na mifuko cha Waste Plastic Enterprises kilichopo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera Justin Nsabi ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuwaunga mkono, kuwapa moyo na kutambua umuhimu wao wa kutunza na kuhifadhi mazingira kwa kukusanya taka na kuzibadilisha kuwa fursa ya ajira kwa wananchi wa Bukoba. Nsabi ametoa shukrani hizo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Festo Dugange alipotembelea kiwanda hicho na kukagua shughuli za uhifadhi wa mazingira zinazofanywa kiwandani hapo na kujionea akina mama na vijana zaidi ya 250 wakiendea na ukusanayaji uchambuzi na uchakataji wa taka ikiwa ni njia ya kijiingizia kipato na kutunza mazingira. "Tunaishukuru Serikali ya Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kutuunga mkono pindi tunapohitaji msaada wa Serikali hari iliyochochea maendeleo ya kiwanda hiki ambacho kimekuwa chachu ya kuzalisha ajira kwa wanawake na vijana" "Wanaof...