Skip to main content

Posts

Showing posts from March 10, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Samia Akutana na Kufanya Mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Unicef

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Akutana na kufanya Mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto (UNICEF) Bi. Catherine Russell, leo tarehe 11 Machi, 2025, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma. Katika mazungumzo yao, Rais Dkt. Samia ameishukuru UNICEF kwa mchango wake katika masuala mbalimbali ikiwemo afya, elimu na lishe kwa watoto pamoja na afya ya msingi.

“Tunataka Kuwa Champion Wa Dira Ya Taifa Ya Maendeleo Ya 2050” – Mwanasheria Mkuu Wa Serikali

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari amesema kuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeshiriki kikamilifu katika kutoa maoni katika utengenezaji na uandaaji wa *Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050* ili kuhakikisha kuwa Dira hiyo inaakisi masuala yote ya Sekta ya Sheria. Mwanasheria Mkuu wa Serikali amezungumza hayo katika mahojiano maalumu na Vyombo vya Habari yaliyofanyika Ofisini kwake, Mtumba Jijini Dodoma, tarehe 10 Machi, 2025. Aidha, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameeleza kuwa Ofisi yake imejipanga kuhakikisha kwamba mambo yote yanayoihusu Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali yanatekelezwa ipasavyo ili kuweza kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya 2050.  *“Sisi kama Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali tutahakikisha kwamba tunaoanisha vizuri Sheria zetu tulizonazo na kule tunakotaka kwenda, ni lazima tuwe na legal framework ya kutufikisha.”* Amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesisitiza suala la kufanya maboresho katika Sheria mb...

Dodoma Jiji Kinara Wa Matumizi ya Teknolojia Kwenye Elimu-mbunge Mavunde

  ▪️Agawa Kompyuta na Printa kwa Shule zote za Sekondari za Jiji la Dodoma ▪️Azindua maabara ya Kisasa ya Kompyuta ▪️Matumizi ya Teknolojia yaongeza ufaulu ▪️Rais Samia apongezwa kwa kuboresha miundombinu ya Elimu *Dodoma* Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde leo amekabidhi Kompyuta 50 na Printa 50 kwa Shule za Sekondari za serikali za Dodoma Jiji pamoja na maabara ya kisasa ya Kompyuta kwa Shule ya Sekondari Viwandani na kuahidi kuifanya Dodoma kuwa kinara kwenye matumizi ya teknolojia kwenye kufundishia. Mavunde ameyasema hayo leo katika hafla ya kukabidhi vifaa hivyo iliyofanyika Shule ya Sekondari Viwandani. “Tunaipongeza serikali chini ya uongozi wa Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa maboresho makubwa ya miundombinu kwenye sekta ya elimu Jijini Dodoma ambapo kwa mwaka huu wa fedha zimetengwa Tsh 16 bilioni. Kompyuta hizi na Printa natumai zitachochea ufaulu na kuwajengea uwezo wanafunzi wetu. Katika Kompyuta hizi tumeweka mitihani yote ya kitaifa kuanzia mwaka 19...

Serikali Imethibitisha Kuwepo Kwa Gonjwa Hili Hatari Nchini

 Waziri wa Afya Jenista Mhagama, amethibitisha kuwepo kwa wagonjwa wawili wa ugonjwa wa Mpox nchini baada ya uchunguzi wa kimaabara kufanyika.  Wagonjwa hao waligundulika kuwa na dalili za ugonjwa huo, ikiwemo vipele usoni, mikononi, na miguuni, pamoja na homa, maumivu ya kichwa na misuli. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wizara ya afya Machi 10,2025 ni kuwa wagonjwa hao walitambuliwa baada ya sampuli zao kuchunguzwa katika maabara ya Taifa. Mmoja wa wagonjwa hao ni dereva wa magari ya mizigo aliyekuwa safarini kuelekea Dar es Salaam. Taarifa hiyo imeeleza kuwa Mpox ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyopatikana kwa wanyama jamii ya nyani na huweza kuambukizwa kwa binadamu kupitia kugusana moja kwa moja na mnyama au mtu mwenye maambukizi.  Serikali imewahakikishia wananchi kuwa imejipanga kudhibiti ugonjwa huo kwa kutumia mikakati madhubuti ya ufuatiliaji, upimaji, na utoaji wa elimu ya afya Wizara ya Afya imewasihi wananchi kuepuka kugusana na watu wenye dalili...

Mwenyekiti wa Ccm Taifa Dkt Samia, Aongoza Kikao cha Nec Jijini Dodoma

  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), leo tarehe 10 Machi 2025, jijini Dodoma.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Akutana na Balozi wa India Nchini

  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa India hapa nchini Mhe. Bishwadip Dey ofisini kwake Msalato Jijini Dodoma leo tarehe 10 Machi 2025. Katika mazungumzo yao Jenerali Mkunda amempongeza Balozi Bishwadib Dey kwa kazi nzuri anayoifanya hapa nchini hususani kudumisha ushirikiano baina ya JWTZ na Jeshi la India katika nyanja ya Mafunzo, Mazoezi, na kubadirishana uzoefu wa kijeshi. Aidha Mkuu wa Majsshi amemwomba Mhe Balozi kuendelea kudumisha ushirikiano baina ya Majeshi haya mawili ili kutoa fursa kubadilishana uzoefu katika nyanja mbalimbali za Kijeshi. Naye Balozi Bishwadib Dey ambaye alifika Ofisini kwa Mkuu wa Majeshi kwa ziara ya kikazi, amelishukuru JWTZ kwa ushirikiano uliopo baina ya Majeshi ya nchi hizi mbili na kuahidi kuendeleza ushirikiano uliopo katika mafunzo, mazoezi na kubadirishana uzoefu wa Kijeshi. Uhusiano uliopo baina ya Majeshi haya mawili ni muendelezowa mahusiano ya muda mrefu baina ya Tanz...

Makamu Mwenyekiti wa Chadema Zanzibar Aongoza Kikao Cha Kamati Kuu

  Kikao cha kamati kuu kikiongozwa na Makamu Mwenyekiti Zanzibar,  hii ni baada ya mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe. Tundu Lissu na Makamu Mwenyekiti Bara Mhe. John Heche asubuhi ya leo kwenda katika viwanja vya Karimjee kumuaga Prof. Philemon Sarungi. Baada zoezi hilo watafika Makao Makuu ya Chama kuendelea na kikao.