Jumuiya ya Amsha yakabidhi Tuzo maalum ya Ualimu kwa hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Jumuiya wa wahitimu wa Shule ya Sekondari Milambo (AMSHA) imeanzisha tuzo maalum ijulikanayo kama Tuzo ya Mwalimu ili kuenzi mchango wa Mwalimu Nyerere na walimu wengine wanaofanya kazi yao kwa weledi mkubwa. Tuzo hiyo imetolewa kwa Mara ya kwanza kwa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius kambarage nyerere ikiwa ni kutambua mchango wake kwa Taifa pamoja Tasnia ya ualimu ikiwemo kufundisha katika shule ya Sekondari Mirambo kati ya mwaka 1946 na 1948 Akikabidhi Tuzo hiyo nyumbani kwa Mwalimu Nyerere,Mwitongo wilayani Butiama Mkoani Mara ,Mjumbe wa Bodi ya AMSHA Abdul-Razaq Badru amesema kuwa Tuzo ya Mwalimu itakuwa ikitolewa kila mwaka kwa Mwalimu aliyetoa mchango ulioleta matokeo chanya kwenye Jamii. Naye mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Derek Murusuri amesema ujio wa tuzo ya AMSHA utakuwa kichocheo kwa wahitimu wengine kuandaa tuzo kama hizo ili kuwapa motisha walimu wengine na kutambua mchango wao kwenye sekta ya elimu. Mbali na tuzo iliyokabidhiwa kwa familia ya Mwalimu Nyerere, wajumb...