Skip to main content

Posts

Showing posts from November 3, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Bingwa Mathayo Cup 2024 kuondoka na zawadi ya ng'ombe na millioni moja

Na Shomari Binda-Musoma BINGWA wa mashindano ya Mathayo Cup 2024 jimbo la Musoma mjini  ataondoka na zawadi ya ng'ombe  na milioni moja. Jumla ya  timu 16 kutoka Kata za manispaa ya Musoma zinawanio zawadi hiyo na nyingine zitakazlkwa mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo.  Akifungua mashindano hayo baada ya kukabidhi jezi na mixpira kwa timu  shiriki mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma   Chikoka amesema  mbunge Mathayo amefanya  jambo kubwa katika kuinua michezo. Amesema mji wa Musoma unatakiwa kuchangamka kupitia matukio mbalimbali yakiwemo ya kimichezo   kama alivyofanya mbunge Mathayo. Chikoka amesema mashindano hayo yameonekana yatakuwa na ushindani kutokana na hamasa ya zawadi na maandalizi ya timu. " Nimshukuru sana mbunge Mathayo kwa kuanzisha mashindano haya yamekuja kuchangamsha mji wa Musoma. "Zawadi ni kubwa zilizoandaliwa na mbunge tukapambane na kucheza kwa nidhamu   katika kipindi chote cha mashindano",...

Mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini akagua eneo la kuzikwa Musuguri kijijini butiama

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda amewasili nyumbani kwa Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerali David Bugozi Musuguri wilayani Butiama Mkoani Mara tarehe 03 Novemba 2024 kwa ajili ya kutoa salamu za pole kwa wafiwa na kukagua maandalizi ya Mazishi ya Hayati Jenerali Musuguri yatakayofanyika tarehe 04 Novemba 2024. Jenerali Mkunda amesema kuwa maandalizi yote yamekamilika na kuwashukuru wananchi wa Butiama na maeneo ya karibu kwa kushiriki katika kutoa heshima za mwisho kwa marehemu  ikiwa ni heshima kwa kiongozi huyo aliyetoa mchango mkubwa katika Ulinzi wa taifa letu. Jenerali Musuguri aliyefariki tarehe 29 Oktoba 2024 akiwa na umri wa Miaka 104 atazikwa nyumbani kwake kwa heshima zote za kijeshi.

Waziri mkuu ahani msiba wa mzee Tutuba

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo November 03, 2024 amehani msiba wa Mzee John Tutuba ambaye ni baba mzazi wa  Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Emmanuel Tutuba nyumbani kwa Gavana huyo Oysterbay jijini Dar es salaam  Mzee Tutuba alifariki Novemba 01, 2024 katika Hospitali ya Shifaa Pan African ya Kinondoni jijini Dar es salaam alikokuwa akitibiwa.

Mbunge Mavunde akabidhi uwanja wa michezo wa kisasa kwa shule ya sekondari dodoma

▪️Ni wa michezo ya Kikapu,pete na wavu ▪️Wazazi na wanafunzi wamshukuru kwa ujenzi huo ▪️DC Shekimweri ahimiza matumizi ya kiwanja kuimarisha Afya bora na maadili 📍Dodoma Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini *Mh. Anthony Mavunde* amekabidhi kwa uongozi wa Shule ya Sekondari Kiwanja cha Ndege kiwanja cha kisasa cha michezo ya mpira wa kikapu,pete na wavu kama sehemu ya kukuza na kuendeleza vipaji vya wanafunzi wa Jijini Dodoma. Tukio hilo limefanyika jana tarehe 2/11/2024 katika shule ya sekondari ya Kiwanja cha Ndege jijini Dodoma . “Namshukuru sana *Mh.Rais Dkt. Samia S. Hassan* kwa kuboresha miundombinu ya mazingira rafiki ya kusomea kwa shule zetu nyingi ikiwemo Shule ya sekondari Kiwanja cha Ndege. Katika kuunga mkono jitihada hizi kubwa nimeamua kujenga uwanja huu wa kisasa wa michezo hapa shuleni ili kusaidia kuibua na kuendeleza vipaji vya wanafunzi wa Dodoma”Alisema Mavunde Naye Mkuu wa Wilaya ya Dodoma *Mh. Alhaj Jabir Shekimweri* amempongeza Mbunge Mavunde kwa juhudi kubwa ya kul...

Tamasha la Rorya fursa festival 2024 kufanyika novemba 6-10 mwaka huu

Wilaya ya Rorya mkoani mara imeandaa Tamasha la Rorya fursa festival mwaka 2024 kwa ajili ya kutangaza fursa mbalimbali za kiuchumi na kijamii zilizopo wilayani humo. Tamasha hilo litafanyika kuanzia novemba sita hadi kumi mwaka huu mjini shirati. Ofisi ya Mkuu wa wilaya Rorya inakaribisha wananchi wote pamoja wadau mbalimbali kushiriki kwenye tamasha hilo litakalozinduliwa na Mkuu wa wilaya hiyo Dokta Khalfan Haule. Miongoni mwa matukio muhimu yatakayopamba Tamasha la Rorya fursa festival ni pamoja na fursa za kilimo,uvuvi,ufugaji,michezo na utalii pamoja na mbuzi,kondoo,samaki na nyama choma. Tamasha hilo litahimitishwa na mashindano ya mbio za mitumbwi katika eneo la mwalo wa sota,mashindano ya kuchoma nyama,maonesho ya fursa pamoja na kutoa vyeti kwa wawekezaji,wajasiriamali pamoja na idara zote wilayani Rorya. Kauli mbiu ya Tamasha hilo ni  Rorya na Uwekezaji endelevu kwa uchumi wa viwanda  

Katibu muhtasi Maimuna Kanyamala atunukiwa shahada ya heshima ya uzamivu nchini canada

Mwanzilishi wa shirika la kutetea haki za wanawake na watoto la Kivulini Maimuna Kanyamala ametunukiwa shahada ya heshima ya uzamivu(PHD)na Chuo kikuu cha Western cha nchini Canada. Chuo hicho kimemtunuku shahada hiyo oktoba 16 mwaka huu baada ya kutambua mchango wake kwenye nyanja ya Maendeleo ya Jamii ikiwemo mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia. Kanyamala ambaye kitaaluma ni Katibu Muhtasi alilianzisha shirika la kivulini mwaka 1999 kufuatia kushamiri kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia. Miaka 25 tangu kuanzishwa kwa shirika la kivulini,shirika hilo linajivunia mafaniko mengi hususani kuwezesha Jamii kuvunja ukimya dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia.  Hayo yamebainika wakati wa hafla ya kumpongeza Maimuna Kanyamala kwa kutunukiwa shahada ya heshima ya uzamivu na chuo kikuu cha Western cha nchini Canada. Akizungumza kwenye hafla hiyo iliyoandaliwa na shirika la kivulini,Kanyamala amelipongeza shirika hilo kwa kuendeleza vyema ndoto zake za kuhakikisha Jamii in...