Skip to main content

Posts

Showing posts from May 1, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu akizungumza na wananchi wa Makambako Mkoani Njombe

 WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, akiwasalimia wananchi wa Idofi, wilayani Makambako, mkoani Njombe, ambako amepokea taarifa ya mradi wa umwagiliaji na soko la mbogamboga, pamoja na kusikiliza changamoto mbalimbali za wananchi wa eneo hilo. Waziri Mkuu ameanza ziara yake leo, Mei 2, 2026, katika mikoa ya Iringa na Njombe.

Mzumbe yaunganisha watafiti na Jamii kukabili athari za tabia nchi na changamoto za maji

Farida Mangube Morogoro  Juhudi za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na changamoto za upatikanaji wa maji zimepata msukumo mpya kufuatia kuimarishwa kwa ushirikiano kati ya watafiti na jamii kupitia mradi wa kimataifa wa ICP Connect na Lab to Life. Hatua hiyo imebainishwa wakati wa semina ya kuwasilisha matokeo ya awali ya tafiti za sayansi ya jamii iliyofanyika  Chuo Kikuu Mzumbe Kampas kuu Morogoro, ikiwa ni sehemu ya awamu ya pili ya mradi huo. Mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano wa kimataifa unaojumuisha Chuo Kikuu cha Antwerp (Ubelgiji), Chuo Kikuu Mzumbe, Taasisi ya Sera ya Maendeleo (IOB), Chuo Kikuu cha Kikristo cha Uganda (UCU), pamoja na Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Afrika ya Nelson Mandela (NM-AIST), Arusha. Akifungua semina hiyo, Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Taaluma, Utafiti na Ushauri), Dkt. Proscovia Kamugisha, alisema mradi huo umeongeza uwezo wa kitaifa katika ufuatiliaji na tathmini ya maendeleo kupitia programu ya Shahada ya Uzami...

SUA yasisitiza Mchango wa wafanyakazi,Yaendelea kuborrsha mazingira ya kazi

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimesisitiza kuwa mafanikio yake katika tafiti, ufundishaji na utoaji wa huduma kwa jamii yanategemea kwa kiasi kikubwa mchango wa wafanyakazi wake, huku kikiahidi kuendelea kuboresha mazingira ya kazi ili kuongeza tija na ustawi kazini. Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi), kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Raphael Chibunda, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo upande wa Mipango, Fedha na Utawala, Prof. Amandus Muhairwa, amesema uongozi wa Chuo umejipanga kushughulikia changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi na kuimarisha mazingira rafiki ya utendaji kazi. Akijibu risala ya wafanyakazi, Prof. Muhairwa alieleza kuwa Menejimenti imepokea kwa uzito maoni, changamoto na mapendekezo yaliyowasilishwa, na itaendelea kuyafanyia kazi kupitia mifumo rasmi ya uongozi kwa lengo la kupata suluhisho endelevu. Alibainisha kuwa SUA inaendelea kuboresha upatikanaji wa vitendea kazi kwa kuimarisha mifumo ya manunuzi na kush...

Wazee wa Mkoa wa Mara waunga mkono Tume ya Rais

  WAZEE na baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Mara wameendelea kusisitiza umuhimu wa kulinda amani ya nchi, wakionesha kuunga mkono Tume ya Rais , wakisema ni hatua muhimu inayotokana na mahitaji ya wananchi wenyewe na si Serikali pekee au Rais Samia Suluhu Hassan. Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wamesema kuwepo kwa dalili za mgawanyiko wa kijamii kunahitaji juhudi za makusudi za kurejesha mshikamano, kupitia majukwaa ya kusikilizana, kujenga imani upya na kuimarisha umoja wa taifa. Dkt. Daniel Ouma, mkazi wa Mkoa wa Mara, amesema ni wakati wa Watanzania kuweka tofauti zao pembeni na kuangalia maslahi ya taifa kwa ujumla. “Ni wakati wa Watanzania kuweka tofauti zao pembeni na kujenga maridhiano kwa ajili ya mustakabali wa nchi,” amesema. Mzee Festo Paulo amesema amani ni msingi wa maendeleo ya kweli, akisisitiza kuwa kila Mtanzania ana jukumu la kuilinda. “Nchi isiyo na amani haina maendeleo. Ni wajibu wa viongozi na wananchi kwa pamoja kuhakikisha tunaidumisha amani na kufuata njia sah...

Rais Samia amkabidhi Waziri Nyansaho Kombe la ubingwa

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho Kombe la Ubingwa wa jumla wa Michezo ya Mei Mosi katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi 2026), Mkoani Njombe tarehe 01 Mei, 2026.

Rais Samia aongoza mei mosi Njombe,asisitiza kazi zenye staha na ustawi wa wafanyakazi

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan leo ameshiriki kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) zilizofanyika kitaifa mkoani Njombe, yaliyobeba kaulimbiu: "Kazi zenye Staha ni Nguzo Imara kwa Maendeleo Endelevu katika Utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050." Rais Dkt. Samia ametambua mchango mkubwa na muhimu wa wafanyakazi katika uchumi wa nchi na maendeleo ya Taifa, na kuongeza kuwa Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kazi, maslahi na ustawi wa wafanyakazi nchini kadri uchumi utakavyoimarika. Ameongeza kuwa, mafanikio yaliyopatikana katika sekta mbalimbali ni matokeo ya jitihada za pamoja baina ya Serikali, wafanyakazi, waajiri na wadau wengine wa maendeleo, hususan sekta binafsi, na hivyo kusisitiza wajibu wa kila mmoja kutimiza nafasi yake kwa weledi, uadilifu na uzalendo. Rais Dkt. Samia pia amesema Serikali imeendelea kuweka mazingira bora ya kazi kupitia nyongeza za mishahara, kuimarisha mifumo ya hifadhi ya...

Jamii ni nguzo muhimu katika uhifadhi endelevu

Na Mwandishi wetu Jovina Massano. Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), kupitia Kituo chake cha Mwanza inaendelea kutoa elimu ya uhifadhi kwa jamii ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha uelewa kwa jamii kuhusu umuhimu wa kulinda rasilimali za wanyamapori. Akizungumza  na Mwandishi wetu Mhifadhi wa Wanyamapori kutoka TAWA Kituo cha Mwanza,Bw.Omary Mhando,ameeleza kuwa  elimu hiyo imelenga kuongeza uelewa mpana wa wananchi kuhusu masuala ya uhifadhi. "Jamii ina wajibu wa kushiriki kikamilifu katika kulinda na kuhifadhi wanyamapori na makazi yao ili kuondokana na migogoro",amesema Mhando. Aidha elimu hii inatoa fursa kwa wananchi na viongozi wa maeneo mbalimbali, kuuliza maswali na kupata ufafanuzi wa kina kuhusu masuala ya uhifadhi. Ushirikiano huu umeleta mwitikio chanya kutoka kwa jamii,ambapo wananchi wameipongeza TAWA kwa jitihada hizo na kuomba elimu hiyo iendelee kutolewa mara kwa mara ili kuimarisha uelewa na ushiriki wao katika uhifadhi. Katika hatua ny...

Kabigi awaasa watumishi wa Tume ya Madini kung'ara Kwa weledi kazini

▪️ Watakiwa kuongeza bidii na kudumisha mshikamano 📍 Dodoma Watumishi wa Tume ya Madini wameaswa kuzingatia weledi, uwajibikaji na mshikamano katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuendeleza mafanikio ya Tume pamoja na kuongeza mchango wa sekta ya madini katika ukuaji wa uchumi wa taifa. Akizungumza leo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) yaliyofanyika kimkoa katika Viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Tume ya Madini, Nsajigwa Kabigi, amesema mafanikio yaliyopatikana yanapaswa kulindwa kwa kuongeza bidii, nidhamu na uwajibikaji kazini. Kabigi amesema Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo, amewapongeza watumishi wote wa Tume waliopo Dodoma, wale walioshiriki maadhimisho ya kitaifa mkoani Njombe pamoja na watumishi waliopo katika mikoa mbalimbali ya kimadini nchini kwa juhudi zao katika kutekeleza majukumu ya kazi. “Tumeaswa kuendelea kudumisha mshikamano, upendo na kufanya kazi kwa bidii ili ku...

Rais Samia Awapa Tano wafanyakazi wa Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono Wafanyakazi waliokuwa wakipita mbele ya Jukwaa Kuu katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi 2026), ambayo Kitaifa yamefanyika Mkoani Njombe, tarehe 01 Mei, 2026. Wafanyakazi wa Wizara mbalimbali, Taasisi za umma na binafsi wakipita mbele ya Jukwaa Kuu katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi 2026) ambayo Kitaifa yamefanyika Mkoani Njombe, tarehe 01 Mei, 2026.   Wafanyakazi wa Wizara mbalimbali, Taasisi za umma na binafsi wakipita na magari wanayoyatumia katika shughuli zao za kila siku, mbele ya Jukwaa Kuu kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi 2026) ambayo Kitaifa yamefanyika Mkoani Njombe, tarehe 01 Mei, 2026. Wafanyakazi wa Wizara mbalimbali, Taasisi za umma na binafsi wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi 2026) ambayo Kitaifa yamefanyika Mkoani Njombe, tarehe 01 Mei, 2026.