Na Mwandishi wetu Jovina Massano Musoma. Chemba ya Taifa ya biashara (TNCC) yamtunuku tuzo maalum waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mwigulu Lameck Nchemba kwa kutambua mchango wake katika kuimarisha mazingira ya biashara, uwekezaji na kukuza ushirikiano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi hapa nchini. Tuzo imetolewa katika hafla iliyowakutanisha viongozi wa serikali, sekta binafsi na wadau wa maendeleo, ambapo TNCC imeweza kueleza kuwa hatua hiyo inalenga kutambua watu na taasisi zilizochangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza uchumi wa Tanzania. Rais wa Chemba ya Taifa ya Biashara (TNCC), Bw. Vicent Minja amemwambia Waziri Mkuu kuwa tuzo hii ni ishara ya kutambua mchango wako mkubwa katika kuimarisha mazingira ya biashara nchini. " Uongozi wako umefungua milango ya ushirikiano imara kati ya serikali na sekta binafsi, jambo ambalo limeongeza imani ya wawekezaji na kuchochea ukuaji wa uchumi hapa nchini", amesema Minja Viongozi na wadau wengine pia wamewez...
Marato tv - Sauti ya Jamii