Skip to main content

Posts

Showing posts from October 18, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Glory Aahidi Maendeleo Kawe na Kuondoa Kero za Wavuvi

Mgombea ubunge wa Jimbo la Kawe kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Glory Tausi Shayo, ameahidi kushughulikia changamoto sugu zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo, zikiwemo miundombinu mibovu, elimu yenye michango mingi na kero kwa wavuvi. Katika ziara yake kwenye kata za Msasani na Mikocheni, Glory amezungumza na wavuvi na kueleza kuwa wengi wao wameamua kujiajiri kupitia sekta ya uvuvi, lakini wanakumbana na kero nyingi ikiwemo maafisa uvuvi kudai faini kubwa na kutokutoa risiti. Amesema pia wavuvi wanataka leseni za uvuvi zitolewe kwa muda wa miaka mitano badala ya mwaka mmoja ili kupunguza usumbufu. Glory amesema ameamua kugombea ubunge wa Kawe kwa lengo la kulifanya kuwa jimbo bora lenye huduma bora kwa wananchi. Ameeleza kuwa Kawe ni miongoni mwa majimbo yenye miundombinu mibovu – hakuna barabara nzuri na kwa urahisi, hakuna mitaro, na huduma za afya zimekuwa "mwiba mchungu". Aidha, ameahidi kupambana na changamoto ya elimu kwa kuhakikisha elimu inakuwa bure kwa vitendo n...

Maafisa Usafirishaji Jimbo ka Mtumba Wahamasika Kushiriki Uchaguzi Oktoba 29.2025

Majira ya saa 8 mchana-9 alasiri leo Jumamosi Oktoba 18.2025,waendesha boda boda na bajaji [Maafisa usafirishaji] jimbo la *Mtumba-Dodoma* wapatao *1000* wameungana na Mgombea Ubunge Jimbo la Mtumba *Ndg.Anthony Mavunde*  kuuthibitishia Umma wa Wana Dodoma na Watanzania kwa ujumla kwamba ,wao kama maafisa usafirishaji wako tayari kuitumia haki yao kikatiba kushiriki Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu,huku wakimshukuru *Rais Samia* kwa  kuwajengea *Ofisi yao ya Mkoa iliyopo maeneo ya Makole* Akizungumza nao Mgombea Ubunge kwa tiketi ya *CCM-Jimbo jipya la Mtumba Ndg.Mavunde* amemshukuru Dkt.Samia kwa jitihada madhubuti katika kuiongezea thamani kada hiyo katika sekta binafsi zikiwemo za ujenzi  wa *Ofisi yao ya Mkoa ambayo tayari imekamilika.Ofisi ambayo na yeye pia kama mlezi wa Mkoa wa  Maafisa usafirishaji hao aliwajengea uzio wa ofisi hiyo.* Aidha amewashukuru kwa namna ambavyo wamekuwa karibu naye wakishirikiana katika kuleta ustawi wa kada hi...

Dkt Nchimbi Atoa Ahadi ya Matumizi Ya Ndege Nyuki 'drones' | Ili Kufukuza Wanyama Waharibifu wa Mazao

Mgombea mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kupitia CCM, Balozi Emmanuel Nchimbi amesema Serikali ijayo ya Chama hicho inakusudia Kutumia ndege nyuki 'Drones' kwa ajili ya kufukuza Wanyama waharibifu katika kata ya Mwaya, Kilombero ili mazao ya wakulima yabaki kuwa Salama. Dkt Nchimbi ametoa hakikisho hilo leo Oktoba 18, 2025 akiwa katika mkutano wa Kampeni za Urais, ambao umefanyika katika Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro. Pamoja na mambo mengine ,Dkt.Nchimbi alitumia nafasi hiyo kumuombea kura za ushindi wa kishindo mgombea Urais wa chama hicho,Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na kumnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Kilombero Ndugu Abubakar Damian ASENGA,pamoja na mgombea Ubunge wa jimbo la Mlimba Ndugu Kellen Rose RWAKATARE  na Madiwani. Balozi Nchimbi anafikia mkoa wa 25 sasa tangu kuzinduliwa kwa kampeni hizo Agosti 28,2025 jijini Dar es Salaam,akiendelea kusaka kura za ushindi wa kishindo za mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kwa tiketi...

Wasira: Nchi Ipo Salama, Waambieni Watanzania Wakapige Kura

*Amesisitiza kuchagua viongozi sahihi* *Kura za urais apewe Dk. Samia wa CCM* Na Mwandishi Wetu,  Bariadi  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amesema nchi ipo salama, wananchi wakumbushwe na kuhamasishawa kuwapigia kura wagombea wenye sifa ambapo kwa upande wa urais ni Dk. Samia Suluhu Hassan anayetokana na CCM. Amesema zipo propaganda chafu katika mitandao ya kijamii lakini yanayooelezwa ni upotoshaji, hayana ukweli kwa lengo la kupotosha umma. Makamu Mwenyekiti Wasira alieleza hayo alipokuwa akizungumza na viongozi wa CCM wilayani Bariadi Mkoa wa Simiyu, leo Oktoba 18, 2025. "Wako watu katika nchi yetu ambao wanakerwa na amani na wanashirikiana na watu wa nje kutaka kuwavuruga. "Siku hizi kuna mitandao ya kijamii inapeleka habari za uongo, kutisha na kuwafanya watu wafikiri kuna shida, mimi, nakuja kuwaambia nchi ipo salama kabisa, nchi yetu iko salama na zimebaki siku 10 twende tukapige kura," alisema. Alisisitiza viongozi wa ...