Skip to main content

Posts

Showing posts from August 31, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

MHASIBU HALMASHAURI YA BUCHOSA APONGEZWA

  Baraza maalumu ya madiwani wa Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza wamepongeza Mhasibu wa Halmashauri hiyo CPA Justice Shemakange kwa kuwasilisha vema Hesabu za Halmashauri hiyo. Pongezi hizo zimetolewa kwenye kikao maalumu cha kupitisha taarifa ya fedha ya Halmashauri hiyo inayoishia Agost 30,2024 mwaka huu Diwani wa Kata ya Kazunzu Boniphace msenyela amesema Mhasibu huyu ameonyesha uwezo wake wa kuandaa na Hesabu kisha kiziwalisha huku adia kuwa baraza hilo halina shaka naye na ni mtu sahihi wa kuisadia Halmashauri hiyo. " Uwezo wake nimkubwa wa kupanga hasebu unaonyesha wazi ni mtu sahihi aliyebobea kwenye kitengo ya fedha wenye cheo Cha CPA ,wamesema madiwani. Kwa upande wake CPA Justice Shemakange Mhasibu wa Halmashauri ya Buchosa amesema jukumu lao kama wataalumu ni kuisadia jamii kupiga hatua kimaendeleo. Diwani wa Kata ya Nyakaliro Paul Kabugwe amesema Mkurunge wa Halmashauri hiyo Benson Mihayo amepata mtu sahihi wa kufanya naye kazi hivyo katika m...

JWTZ YAPONGEZWA KUDUMISHA UTAMADUNI NCHINI

  WAZIRI wa ulinzi na jeshi la Kujenga Taifa JKT Mh Dkt Stergomena Tax,amesema jeshi la ulinzi wa wananchi Tanzania,litaendelea na majukumu yake, lakini pia litashiriki kikamilifu katika kudumisha mila na tamaduni zenye kuleta taifa pamoja. Mh Tax,ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam wakati wa kufunga mashindano ya utamaduni ya mkuu wa majeshi ambayo yamefanyika Msasani Club na kushirikisha vikundi tisa vya ngoma za asili na bendi kumi za muziki wa dansi. Pamoja na kumpongeza mkuu wa majeshi ya ulinzi jenerali Jacob John Mkunda, kuanzisha wazo la kuanzishwa kwa mashindano hayo amesema yatasadia kuleta mabadiliko makubwa ndani ya jamii. Amesema kazi hiyo ambayo imefanywa na jeshi,kupitia mkuu wa majeshi ni sehemu ya kuunga mkono jitihada kubwa zinazofanywa na amri jeshi mkuu Rais Dr Samia Suluhu Hassan,kwa kuweka nguvu kubwa za   kuendelezwa,kudumisha na kuzienzi mila na desturi za kitanzania. Naye mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini jenerali JACOBO JOHN MKUNDA,amesema ...