Skip to main content

Posts

Showing posts from July 11, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt Binilith Mahenge Awakaribisha Wawekezaji Kuwekeza Tanzania

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, TIC, Dkt. Binilith Mahenge ametoa wito kwa Wawekezaji kuja kuwekeza Tanzania, kutokana na amani na utulivu pamoja na uwepo ya maeneo ya kutosha kwa ajili ya uwekezaji. Pia Dkt. Mahenge amewakaribisha Wawekezaji wote kuja kuwekeza nchini kutokana na uwepo wa fursa mbalimbali kwenye uwekezaji. Amesema hayo akiwa kama Mgeni rasmi kwenye Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na India (Haryana India), kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Sabasaba, Vile vile, Dkt. Mahenge amesema kuwa nchi za Tanzania na India zimedumisha mwelekeo wa masoko kwenye masuala ya biashara na uwekezaji katika sekta mbalimbali, zikiwemo sekta muhimu za Afya na Elimu.

Wakazi wa Sang'ang'a Tarime Wamshukuru Rais Samia Kwa Mradi wa Visima

Na Shomari Binda-Tarime WANANCHI wa Kitongoji cha Sang'anga Kijiji na Kata ya Nyabisanga wilayani Tarime mkoa wa Mara wameshukuru kupata mradi wa Rais Samia wa kuchimbiwa visima vya maji na sasa wana uhakika wa kupata maji safi na Salama Wakizungumza na Waandishi wa Habari leo julai 11 kijijini hapo wamesema kuyaona magari ya kuchimba visima na kuanza kufanya kazi hiyo ni ishara ya kuondokana na adha ya maji waliyokuwa nayo kwa muda mrefu. Wamesema wamekuwa wakiamka usiku wa manane kwenda kutafuta  maji na kushindwa kujiandaa na shughuli nyingine za kiuchumi ikiwemo kilimo hivyo mradi huo umekuwa mkombozi. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Ghati Marwa amesema wanamshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa mradi huo wa visima vya maji kwaajili ya kuwatua ndoo kichwani. " Tunashukuru sana Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa mradi huu wa kutuletea visima vya maji huku kijijini kwetu. " Kwa namna kazi zinavyoendelea kufanyika hapa tuna uhakika wa kuanza kupata m...