Skip to main content

Posts

Showing posts from May 11, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Majimbo mapya manane ya uchaguzi Hadharani

Tume huru ya  Taifa ya Uchaguzi imetangaza kuanzishwa kwa Majimbo mapya Manane ya uchaguzi nchini.  Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele ameyataja Majimbo mapya kuwa ni Kivule,chamazi,Mtumba,Bariadi Mjini, Chato Kusini,Katoro,Uyole pamoja na Jimbo la Itwangi Jaji Mwambegele amesema kuwa Jimbo Jipya la Kivule limeanzishwa baada ya kugawanywa kwa Jimbo la Ukonga,Chamazi limegawanywa kutoka Jimbo la Mbagala.  Jimbo la Dodoma Mjini Limezaa Jimbo la Mtumba,Bariadi Mjini limetokana na kumegwa kwa Jimbo la Bariadi,Chato Kusini limetokana na Jimbo la chato,Katoro limemegwa kutoka Jimbo la Busanda,Uyole limetoka Jimbo la Mbeya Mjini huku Jimbo la Solwa likizaa Jimbo Jipya la Itwangi.  Mbali na Majimbo mapya manane,Kata mpya Tano pia zimeanzishwa nchini.  Aidha Tume hiyo imetangaza kubadilishwa kwa Majina ya Majimbo 12 ya uchaguzi ikiwemo Jimbo la Chato ambalo sasa litaitwa Chato Kaskazini,Jimbo la Singida Mashariki sasa litajulikana Ikungi ...

Waziri Mkuu Kumwakilisha Dkt. Samia Kwenye Mkutano wa Maafisa Watendaji Wakuu Barani Afrika

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewasili nchini Ivory Coast kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa Siku mbili wa Maafisa Watendaji Wakuu wa Africa unaoanza leo Mei 12, 2025 jijini Abidjan. Mheshimiwa Majaliwa amepokelewa katika uwanja wa ndege wa Félix-Houphouët-Boigny Jijini Abidjan na Waziri Mkuu wa Ivory Coast  Robert Beugre Mambe.

Wachimbaji Geita Wampongeza Rais Samia Kwa Mafanikio Makubwa ya Sekta ya Madini

▪️Wachimbaji Madini wapongeza upatikanaji wa Leseni na mazingira rafiki ya biashara ▪️Waziri Mavunde aainisha mafanikio 16 ya Rais Samia kwenye sekta ya Madini ▪️Aagiza uanzishwaji wa Soko la Dhahabu Katoro ▪️RC Shigela aja na mikakati mizito ya kupaisha sekta ya madini Geita *Katoro,Geita* Wachimbaji na Wafanyabiashara wa Madini wa Mkoa wa Geita wamempongeza Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana kupitia sekta ya madini katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake. Hayo yamesemwa jana kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na wachimbaji hao katika eneo la mnada wa zamani Katoro,Geita kwa lengo la kumpongeza Rais Samia kwa mafanikio yaliyopatikana kupitia sekta ya madini. Akitoa maelezo ya awali,Mwenyekiti wa Chama cha Wachimba Madini Mkoa wa Geita(GEREMA) Ndg. Titus Kabuo amesema dhumuni kubwa la kusanyiko hilo ni kumpongeza Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa kuiboresha sekta ya madini na kuweka mazingira rafiki ya uchimbaji na ufanyaji biashara hali inayopele...

Jeshi la Polisi Mkoani Tanga Laanza Kuchukua Hatua Kwa Madereva wa Serikali

Na MASHAKA MHANDO, Tanga JESHI la polisi mkoani Tanga, limekutana na kuzungumza na madereva wa magari ya serikali, taasisi na mashirika ya umma kuwakumbusha umuhimu wa kuzingatia Sheria za usalama barabarani. Akifungua mkutano baina ya jeshi hilo na madereva hao, Kamanda wa polisi mkoani Tanga ACP Almachius Mchunguzi, alisema kuwa kuna umuhimu mkubwa kwa madereva hao kuendesha magari hayo kwa kufuatia Sheria ili wasiweze kusababisha ajali za kizembe zinazotokana na mwendokasi. Alisema wanawakumbusha Sheria hizo kwakuwa mara nyingi wao ndiyo wanaovunja Sheria hizo kwa kujiona wao hawapaswi kufuata Sheria kwa vile wamewapakia viongozi. "Wakati mwingine mnawasingizia viongozi kwamba wao ndiyo wanawalazimisha mtembee mwendo mkali hapa, nyie ndiyo mliokuwa na dhamana ya kulitoa gari sehemu moja kwenda sehemu nyingine hivyo lazima mfuate Sheria za usalama barabarani," alisema Mchunguzi. Akizungumza kuwaasa zaidi madereva hao, Mkuu wa usalama barabarani mkoani Tanga, SP Willy Mwamas...

Siku ya Wakina Mama Yampa Raha Mbunge Mavunde

 ANAANDIKA MBUNGE ANTHONY MAVUNDE Mwaka Jana nilialikwa kwenye shughuli ya Umoja wa Wafanyabiashara wa Mboga mboga na Matunda wa Masoko (UWAWAMA) wakati wa uzinduzi huo ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mwenyekiti wa UWT Ndg. Mary Chatanda. Nikiwa hapo niliwaahidi wakina mama hawa wa UWAWAMA kuwapatia mradi wa kuinua mfuko wao kwa kuchangia cha Tsh 10,000,000 na kuwanunulia Shamba la Zabibu. Niliwakabidhi shamba lililopo katika eneo la Mpunguzi-Dodoma na wakaanza kulima mara moja pasipo kuchelewa. Leo ninafuraha kubwa kuona zao la kwanza la Zabibu kutoka kwenye shamba la UWAWAMA. Nawatakia heri ya siku ya WAKINAMAMA WOTE DUNIANI

Kanisa Anglikana Lasisitiza Umuhimu Wa Uchaguzi Mkuu Oktoba

📌 Askofu Mkuu Maimbo Mmdolwa ahimiza katiba ifuatwe  ðŸ“Œ Dkt. Biteko asema milango ya Serikali iko wazi kwa mazungumzo 📌 Asema Serikali inathamini mchango wa kanisa kwa jamii Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Mhashamu Maimbo Mmdolwa amewahimiza Watanzania kushiriki katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025 na kuongeza kuwa nchi inaweza kuingia katika mgogoro mbaya wa kikatiba kama watasikiliza watu wanaotaka kuahirisha Uchaguzi Mkuu. Askofu Mmdolwa amesema hayo Mei 11, 2025 jijini Mbeya  katika ibada ya kuwekwa wakfu Canon Jacob William Kahemele kuwa Askofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Nyanda za Juu Kusini - Mbeya ambapo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mgeni rasmi. “ Kwa kuwa Naibu Waziri Mkuu uko hapa na tuliombe Taifa zima kutoahirisha Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 kwa kuwa tutaingia katika ...

Balozi Nchimbi Ateta na Othman Masoud Othman

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akizungumza jambo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Mhe. Othman Masoud Othman, walipokutana Viwanja vya Karimjee, jijini Dar Es Salaam, wakati wa utoaji heshima za mwisho, kumuaga Hayati Mzee Cleopa David Msuya, Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu, katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar Es Salaam, leo Jumapili tarehe 11 Mei 2025. 

Rais Mwinyi Aifariji Familia Ya Marehemu Charles Hillary

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametoa mkono wa pole kwa familia ya marehemu Charles Hillary, aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo, tarehe 11 Mei 2025, jijini Dar es Salaam. Rais Dkt. Mwinyi amefika nyumbani kwa marehemu, Mtaa wa Kibamba CCM, Wilaya ya Ubungo, jijini Dar es Salaam, kutoa mkono wa pole kwa mjane wa marehemu, Bi Sarah Mwakanjuki, pamoja na wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki. Rais Dkt. Mwinyi amewataka wote walioguswa na msiba huo kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. Marehemu Charles Hillary amefariki akiwa na umri wa miaka 66.  Rais Dkt. Mwinyi alimteua kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu tarehe 30 Desemba 2021, na baadaye akamteua tena kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tarehe 6 Februari 2023.