Skip to main content

Posts

Showing posts from December 18, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Serikali kutoa mirahaba ya bil 1 kwa wasanii mwakani

  NA MASHAKA MHANDO WIZARA ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, kupitia Taasisi ya Hakimiliki nchini (COSOTA), inatarajia kuweka historia mpya kwa kugawa zaidi ya shilingi bilioni moja kama mirabaha kwa wasanii wa kampuni mbalimbali nchini ifikapo Januari 23, 2026. Hatua hiyo inakuja baada ya imani ya kimkakati kati ya Naibu Waziri wa sekta hiyo, Mhe. Hamis Mwinjuma (MwanaFA), na uongozi wa COSOTA, yaliyolenga kujibu kiu ya muda mrefu ya wasanii kuhusu malipo ya haki zao. Akizungumza katika mahojiano maalum, MwanaFA alisema kuwa Serikali imejipanga kufanya ugawaji huo kuwa tukio kubwa na kihistoria kutokana na kiwango kikubwa cha fedha kilichopokea. "Kama msanii kama Naibu Waziri, nilipokea maswali mengi kutoka kwa wasanii wenzangu wakitaka kujua hatma ya mirabaha yao. Nimefanya (discussion) nzuri na COSOTA na tumekubaliana kuwa Januari 23 mwakani, tunakwenda kutoa zaidi ya shilingi bilioni moja na ushee. Himekuwa ni kiwango kikubwa ambacho hakijawahi kutokea nchini," alis...

Dkt. Mwigulu Kukagua Miradi ya Maendeleo Mkoani Lindi

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Desemba 19, 2025 amewasili kwenye uwanja wa ndege wa Mtwara akiwa njiani kuelekea mkoani Lindi kwa ajili ya Ziara ya Kikazi. Mheshimiwa Dkt. Mwigulu leo anategemea kukagua Maendeleo ya Ujenzi wa Bandari ya Uvuvi Kilwa pamoja na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Madaraja na Ukarabati wa barabara Kuu ya Marendego-Nangurukuru-Lindi-Mingoyo.

Bilioni 11.3 kuzalisha Vitambulisho vya Watoto

Na Mwandishi Wetu Serikali iko katika  Maandalizi ya Usajili wa watoto wenye umri chini ya miaka 18 ili kutoa namba ya utambulisho ya kipekee ambayo itatolewa tangu mtu anapozaliwa hadi mwisho wa maisha yake ikiwa ni Utekelezaji wa Maelekezo ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyotoa tarehe 10 Agosti,2023. Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene wakati wa ziara ya ukaguzi wa uzalishaji wa vitambulisho katika Kituo cha Kuchakata Taarifa  cha Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA)  ambapo amaetaja kiasi cha Shilingi Bilioni 11.3 kutengwa kwa ajili ya zoezi  huku wilaya za majaribio zikiwa ni Kilolo, Kusini Unguja na Rungwe ambapo pia ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kufika sehemu walizojiandikisha kuchukua vitambulisho vyao. ‘Jamii namba itakayotambua watoto ndio jambo kubwa ambalo linakuja sasa na itaondoa malalamiko mbalimbali kwani mtu atakua anatambulika kuanzia pale anapozaliwa lak...

Papa Alaani Viongozi wa Dini Kuchochea Migogoro ya Nchi.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo, amelaani tabia ya baadhi ya viongozi wa dini kutumia mamlaka na ushawishi wao kwa waumini kuhalalisha migogoro na migawanyiko ndani ya mataifa yao. Leo, ambaye ni Papa wa kwanza kutoka nchini Marekani, ameyasema hayo kupitia ujumbe wa kurasa nne uliotolewa kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani ya Kanisa Katoliki, yanayolenga kusisitiza umuhimu wa kulinda, kuimarisha, na kudumisha amani katika jamii. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Desemba 18, 2025, Papa Leo amesema kumekuwa na baadhi ya viongozi wa dini wanaotumia kigezo cha sera za uzalendo, kama nyenzo ya kupandikiza chuki miongoni mwa waumini kitendo ambacho amekiita ni kufuru, au dhambi kubwa inayomdharau na kumtukana Mungu. "Kwa bahati mbaya, imekuwa jambo la kawaida zaidi kuivuta lugha ya imani katika vita vya kisiasa, kubariki utaifa, na kuhalalisha vurugu na mapambano ya silaha kwa jina la dini," amesema Papa. Amesema waumini lazima wajue kukanusha kikamilif...

Kituo cha urithi wa ukombozi Afrika kujengwa Tanzania-MwanaFA

Na Mwandishi wetu TANZANIA  imeandika historia nyingine kubwa katika nyanja ya kidiplomasia na utamaduni baada ya kufanikiwa kupitisha ajenda ya kuanzishwa kwa Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika (ALHC) kama Taasisi rasmi ya Umoja wa Afrika (AU), kitakachokuwa na makao yake nchini Tanzania. Ushindi huo umepatikana katika Mkutano wa Tano wa Mawaziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Nchi za Afrika (STC–YCS5) uliofanyika Jijini Bujumbura, Burundi. Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo uliongozwa na Mheshimiwa Hamis Mwinjuma (MwanaFA), ambaye amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha nafasi ya Tanzania kama mhimili wa ukombozi wa bara la Afrika inatambulika rasmi kwa kuanzishwa kituo hicho. Katika mkutano huo, MwanaFA alionekana akibadilishana mawazo na kufanya mazungumzo ya kimkakati na Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamaduni wa Afrika Kusini, Mhe. Gayton McKenzie, Viongozi hao wawili wamekubaliana kuendeleza ushirikiano wa karibu kati ya nchi hizo mbili ambazo zina historia ndefu na ya k...

Waziri wa Ulinzi na Jkt Afungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi

 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga, Mheshimiwa Dkt. Rhimo Nyansaho,(Mb) tarehe 18 Desemba 2025 amefungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, katika Ukumbi wa Umwema mkoani Morogoro.  Kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wake ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na JKT, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, kilihudhuriwa na wajumbe kutoka Wizara, Ngome na JKT pamoja na ujumbe wa Tughe Taifa wa Morogoro. Akizungumza kwenye ufunguzi huo, Waziri wa Ulinzi, Dkt Nyansaho, amewaeleza washiriki wa Baraza la Wafanyakazi kuwa Kukusanyika kwao ni sehemu muhimu katika kuboresha mazingira ya kazi na kuongeza ufanisi na tija katika Taasisi yetu.  Akawaambia kuwa uzoefu umeonesha kuwa, Mabaraza ya Wafanyakazi yanapotumika vyema, huleta hali ya maelewano, umoja, ushirikiano na utulivu mahali pa kazi. Aidha, akawaasa kutambua kuwa, ushirikiano wenye tija unahitaji nidhamu, uwajibikaji na moyo wa kujituma. “Tunapofanya kazi kwa umoja, tunapas...

Viongozi wa Dini Mkoani Kagera Wataka Mijadala ya Kutatua Changamoto Katika Kulinda Amani

  Na Angela Sebastian ;Bukoba Viongozi wa dini mkoani Kagera wamewataka viongozi wa Serikali kuandaa mijadala ya mara kwa mara kati yao ili kukutana na kuongea namna ya kuzitatua changamoto zinazoweza kujitokeza na kusababisha uvunjifu wa amani ambayo ni Tunu ya Taifa letu. Viongozi hao wameeleza hayo leo wakati wa Dua na sala ya kuombea Taifa na mkoa huo katika uzinduzi wa kongamano la Ijuka Omuka (Kumbuka nyumbani)lililoandaliwa na mkuu wa mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa kwa lengo la kutangaza fursa za kiuchumi zilizipo mkoani humo. Shekh Abdulshah Abbas ni kiongozi wa Answari Suna amesema viongozi wa dini wamepewa dhamana ya kuhakikisha tunapeleka watu mbinguni na siyo motoni na mwalimu mzuri ni yule anayefundisha wanafunzi wake kulinda amani ya nchi yao pia wazazi wazuri ni wale wasiosahau wajibu wao wa malezi kwa watoto. Alisema vitabu vyote vya dini vinahimiza watu kuwa wamoja,kupenda nchi zao,kutohasi mema tunayojaaliwa na Mungu maana hakuna shetani mbaya kama mtu anayehim...

Tume ya Madini, TRA zaunganisha nguvu kuongeza ufanisi wa ukusanyaji maduhuli

DODOMA TUME  ya Madini kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zimeimarisha ushirikiano wao kwa lengo la kuongeza ufanisi na tija katika utekelezaji wa majukumu ya taasisi hizo, hususan katika ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali yatokanayo na shughuli za madini. Akifungua kikao kazi cha kuhuisha Mkataba wa Makubaliano (MoU) leo Desemba 18, 2025 katika Ukumbi wa Tanzanite uliopo Ofisi za Tume ya Madini jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Tume ya Madini, Nsajigwa Kabigi, amesema ushirikiano huo unatarajiwa kuleta matokeo chanya katika utekelezaji wa majukumu ya taasisi hizo kwa mwaka wa fedha 2025/2026. Amesema MoU hiyo inalenga kuimarisha ushirikiano kupitia ubadilishanaji wa taarifa, mafunzo ya pamoja na utekelezaji wa kaguzi za pamoja, hatua itakayoongeza uwazi, ufanisi na tija katika ukusanyaji wa maduhuli yanayotokana na shughuli za Sekta ya Madini. “Kwa kutambua mchango mkubwa wa TRA katika kufanikisha majukumu ya Serikali, Tume ya Madini ilio...

Viongozi wa Dini Mkoani Kagera Wataka Mijadala ya Kutatua Changamoto Katika Kulinda Amani

Na Angela Sebastian ;Bukoba Viongozi wa dini mkoani Kagera wamewataka viongozi wa Serikali kuandaa mijadala ya mara kwa mara kati yao ili kukutana na kuongea namna ya kuzitatua changamoto zinazoweza kujitokeza na kusababisha uvunjifu wa amani ambayo ni Tunu ya Taifa letu. Viongozi hao wameeleza hayo leo wakati wa Dua na sala ya kuombea Taifa na mkoa huo katika uzinduzi wa kongamano la Ijuka Omuka (Kumbuka nyumbani)lililoandaliwa na mkuu wa mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa kwa lengo la kutangaza fursa za kiuchumi zilizipo mkoani humo. Shekh Abdulshah Abbas ni kiongozi wa Answari Suna amesema viongozi wa dini wamepewa dhamana ya kuhakikisha tunapeleka watu mbinguni na siyo motoni na mwalimu mzuri ni yule anayefundisha wanafunzi wake kulinda amani ya nchi yao pia wazazi wazuri ni wale wasiosahau wajibu wao wa malezi kwa watoto. Alisema vitabu vyote vya dini vinahimiza watu kuwa wamoja,kupenda nchi zao,kutohasi mema tunayojaaliwa na Mungu maana hakuna shetani mbaya kama mtu anayehimiza...

Dkt. Mwigulu: Amani ni Msingi wa Maendeleo

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Desemba 18, 2025 amezungumza na wakazi wa Kiwira mkoani Mbeya ambapo yupo kwenye ziara ya kikazi ya kukagua miundombinu ya umma na mali za watu binafsi ambazo zimeathirika na vurugu zilizotokea Oktoba 29, 2025. Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amewaeleza wananchi hao kuwa kila Mtanzania anapaswa kuilinda amani iliyopo kwani ndio msingi wa maendeleo. “Kila mtanzania anapaswa kuilinda Tanzania” Amesema kuwa Watanzania wanapaswa kuwa makini na watu wenye nia ovu dhidi ya Tanzania na kuhamasisha vurugu zinazoathiri shughuli za kiuchumi na kijamii. “Tunaelewa lengo lao ni rasilimali zetu, Tanzania ina rasilimali adhimu barani Afrika na wanajua ili kuzipata ni lazima kuwavuruga watanzania ambao wameungana, hili msikubali amani yetu ndio kila kitu”