Wachimbaji wadogo wa Madini wameipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa ushirikiano mkubwa na Shirikisho la Wachimbaji wa madini FEMATA ambao umewezesha kupatikana kwa zana mbalimbali za kisasa za uchimbaji wa madini. Wakizungumza na GM TV baadhi ya wachimbaji hao wamesema hatua hiyo imetokana kazi nzuri zinazodanywa na FEMATA chini ya Rais wake John Wambura Bina "Hongera sana sana Mh Rais wa Shirikisho la vyama vya wachimbaji Madini Tanzania Ndugu John Wambura Bina kwa namna unavyoweza kushauri Serikali na kukubaliana nao juu ya mambo mengi ya msingi yanayo kwenda kuleta matokeo kwa wachimbaji" walisema wachimbaji wadogo na kuongeza kuwa "Vifaa hivi vinavyoendelea kuletwa nchini kwa ajili ya uchorongaji na utafiti vimetokana na hamasa yako ya kuwaunga wachimbaji wadogo kote nchini na mchango wao katika Pato la Taifa na Taifa limeona" Wachimbaji hao pia wamempongeza kwa dhati Mkurugenzi wa Shirika la Madini Tanzania(Stamico)Dkt.Vernus Mwase kwa kazi kubwa ya kute...
Marato tv - Sauti ya Jamii