Skip to main content

Posts

Showing posts from May 14, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Afrika Yahimizwa Kujenga Mustakabali Salama kwa Watoto

Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Neema Mwigulu Nchemba, ametoa wito  kwa viongozi na wadau wa Afrika kuweka kipaumbele katika ulinzi wa watoto dhidi ya ukatili wa kidijitali.  Akizungumza jijini Nairobi, Kenya  Mei 12, 2026, katika  Mkutano wa Wenza wa Mawaziri wakuu wa nchi za Afrika, uliofanyika Pembezoni  mwa Mkutano wa “Africa-Forward Summit” ukilenga kujenga mazingira salama ya kidijitali kwa watoto wa Afrika katika ulimwengu unaoendeshwa na Akili Unde (AI). Bi.Nchemba alisisitiza kuwa mustakabali wa bara la Afrika hautategemea tu vigezo vya kiuchumi, bali uwezo wa watoto kujifunza na kuvumbua katika nafasi ya kidijitali bila hofu ya unyanyasaji. Katika hotuba yake, alibainisha kuwa ingawa teknolojia ya Akili Bandia (AI) inatoa fursa kubwa katika sekta za elimu, afya, na ujasiriamali, imeleta pia hatari mpya na halisi. Alitaja changamoto kama vile uonevu mtandaoni, unyanyasaji wa kijinsia unaochochewa na AI, na ulaghai kama vitisho...

Mhe.Mmuya Aongoza Ujumbe wa Tanzania Katika Mkutano wa Mawaziri Wanaoshughulikia Maafa Nchi za Sadc uliofanyika Zimbabwe

MASVINGO – ZIMBABWE Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Kaspar Mmuya ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Sita (6) wa Kawaida wa Kamati ya Mawaziri Wanaohusika na Usimamizi wa Maafa kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Mheshimiwa Profesa Palamagamba Kabudi unaofanyika Masvingo, Zimbabwe. Aidha, Mkutano huo pamoja na masuala mengine umejadili maendeleo yaliyopatikana katika utekelezaji wa programu za kikanda na masuala ya kimkakati katika utekelezaji wa afua mbalimbali katika Usimamizi wa maafa,pia mkutano huo utatumika kama jukwaa kwa Mawaziri kuimarisha ushirikiano na Washirika wa Maendeleo wa Kimataifa na Jumuiya ya Wafadhili kuhusu uwekezaji katika Usimamizi wa Maafa ili kujenga ustahimilivu wa kikanda. Naibu Waziri Ameongozana na mwenyeji wake ambaye ni Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Mhe. CP-Suzan Kaganda, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anaye...

Mabausa Wanaodaiwa Kumuua Mteja kwa Kipigo Wapandishwa Kizimbani

Na: Dawati la Habari Polisi; Mwanza Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limewafikisha Mahakamani mlinzi (baunsa) pamoja na mfanyakazi wa usafi waliokuwa wakifanya kazi katika baa ya Las Vegas, wakituhumiwa kwa mauaji ya Mkazi wa Mwanza, Mzafuru Faisal Yunusu. ​Washtakiwa hao ni Yohana Paul Peter (22), ambaye ni mlinzi wa eneo lilipotokea tukio hilo na Hamis Juma Mussa (27), mfanyakazi wa usafi.  Wawili hao wamepandishwa kizimbani leo Alhamisi Mei 14, 2026, katika Mahakama ya Wilaya ya Ilemela na kusomewa shtaka la mauaji. ​Akisoma shauri hilo la jinai namba 10492 la mwaka 2026 mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilemela, Mhe. Christian Mwalimu, Wakili wa Serikali Clara Muhando, akisaidiana na Evance Kaiza, aliieleza mahakama kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo mnamo tarehe 05.02.2026 katika baa ya Las Vegas iliyopo eneo la Kona ya Bwiru, mtaa wa Nyamanoro, wilaya ya Ilemela. ​Washtakiwa wote wawili, wakiwa katika baa hiyo ya Las Vegas, wanadaiwa kumshambulia na kumuu...

Wanawake wamiliki asilimia 54 ya biashara ndogo nchini

📍TRA yawawekea mkakati rafiki wa Kodi  Na MASHAKA MHANDO, Tanga MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga, imebainisha kuwa wanawake nchini wanamiliki asilimia 54 ya biashara ndogo, za kati na ndogo (MSMEs), hali inayolazimu kuwepo kwa mifumo rafiki ya kodi itakayochochea ukuaji wa sekta hiyo bila hofu ya vikwazo. Kauli hiyo imetolewa leo Mei 14, 2026, na Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga, John Castro wakati akifungua Kongamano la Jukwaa la Wanawake na Kodi lililofanyika katika ukumbi wa Regal Naivera Hotel jijini hapa. John alisema takwimu za hivi karibuni zinaonyesha mchango mkubwa wa wanawake katika uchumi, ambapo ushiriki wao katika nguvu kazi unakadiriwa kufikia takribani asilimia 80 kwa mwaka wa fedha 2024/2025, jambo linalowafanya kuwa mhimili mkuu wa mapato ya ndani. Jukwaa la Wanawake na Kodi Meneja huyo alifafanua kuwa kuanzishwa kwa jukwaa hilo ni hatua ya kihistoria yenye lengo la kuwapa wanawake elimu sahihi, kusikiliza changamoto zao, na kujenga uaminifu utakaohamasis...

Madalali Wasiosajiliwa Wanaharibu Sekta ya Ardhi Nchini-Arepta

RAIS wa Chama cha Wataalamu wa Milki Tanzania (AREPTA), Boniphace Yumba amesema madalali wasiosajiliwa wameendelea kuwa chanzo kikubwa cha migogoro ya ardhi na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi nchini. Yumba amesema hali hiyo inatokana na baadhi ya watu kujihusisha na shughuli za udalali wa ardhi bila kuwa na usajili, taaluma wala kufuata taratibu rasmi za sekta hiyo. Akizungumza leo Mei 14, 2026 katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Wataalamu wa Milki Tanzania (AREPTA), amesema sekta ya ardhi inahitaji usimamizi wa kitaalamu ili kulinda wananchi dhidi ya utapeli na hasara zisizo za lazima. “Ni kweli kwamba kuna madalali ambao wanaharibu sana sekta ya ardhi. Sisi tuna wataalamu waliosajiliwa, wamesomea na wamebobea katika kazi hizi, lakini bado wapo watu wanaofanya kazi bila usajili na bila kufuata misingi ya kitaalamu,” amesema Yumba. Kwa mujibu wa Yumba, wananchi wengi wanaolalamikia kupoteza fedha au kuingia kwenye migogoro ya ardhi wamekuwa wakifuata madalali wasiotambulika, jambo li...

Waziri wa Ulinzi na Jkt Akiteta na Waziri wa Mifugo na Uvuvi

Waziri wa Ulinzi na JKT Mhe.Dkt.Rhimo Nyansaho, ashiriki katika kikao Cha 28 Cha Mkutano wa 3 wa Bunge la 13 Jijini Dodoma wakati wa Uwasilishaji wa Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi Mei 13, 2026.

Tanzania Yakamilisha Mfumo wa Kurejesha Hali Baada ya Maafa

Na Mwandishi Wetu - Masvingo, Zimbabwe. TANZANIA imekamilisha maandalizi ya Mfumo wa Taifa wa Kurejesha Hali Baada ya Maafa, hatua inayolenga kuimarisha uwezo wa Taifa kukabiliana na athari za majanga yanapotokea. Mfumo huo unatajwa kuwa sehemu ya mkakati mpana wa Tanzania wa kukabiliana na ongezeko la maafa yanayochangiwa na mabadiliko ya tabianchi, huku ukitoa mwongozo wa hatua za haraka za kurejesha huduma za kijamii, miundombinu muhimu pamoja na shughuli za kiuchumi katika maeneo yaliyoathirika. Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Kaspar Mmuya akimwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi katika Mkutano wa Sita wa Kawaida wa Kamati ya Mawaziri wenye dhamana ya Usimamizi wa Maafa katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika Mei 11 hadi 14 mjini Masvingo, Zimbabwe. Alisema mfumo huo umezingatia matumizi ya mifumo ya kisayansi na tek...