Skip to main content

Posts

Showing posts from August 24, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Majaliwa Mgeni Rasmi Maadhimisho ya Miaka 50 ya Teww

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Agosti 25, 2025 ni mgeni rasmi katika kongamano la kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima inayofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Lengo kuu la kongamano hilo ni kuhakikisha kuwa elimu ya watu wazima inakuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kiteknolojia kwa nchini. Pia ni jukwaa la kubadilishana uzoefu, matokeo ya tafiti na mbinu bora zinazoweza kuendeleza ubunifu katika utoaji wa elimu ya watu wazima. Kongamano hilo linalofanyika kuanzia leo tarehe Agosti 25, 2025 hadi Agosti 27, 2025 lina kaulimbiu isemayo Elimu Bila Ukomo kwa Maendeleo Endelevu."

Tanzania Kuwa Kinara wa Utoaji wa Huduma za Kimaabara Afrika Mashariki na Kati

▪️Waziri Mavunde aweka jiwe la Msingi wa Ujenzi wa Maabara ya kisasa ▪️Ni maabara kubwa ya uchunguzi wa sampuli za madini Afrika Mashariki ▪️Kugharimu Tsh Bilioni 14.3  ▪️Rais Samia atajwa kinara wa mageuzi sekta ya madini Kizota,Dodoma Tanzania imeanza ujenzi wa maabara kubwa na ya kisasa ya uchunguzi wa sampuli za madini ambayo itakuwa ni kubwa kuliko zote kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati na ambayo itatoa huduma ya kimaabara kwa ubora na kwa uharaka kwa wadau wa sekta ya madini nchini. Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa maabara ya kisasa ya uchunguzi wa sampuli za madini katika eneo la Kizota,Jijini Dodoma. “Tunamshukuru Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa kuwa kinara wa mageuzi makubwa ya sekta ya madini na kwa kuandika historia ya ujenzi wa maabara hii ya kisasa miaka 100 baadaye tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa madini(GST) mwaka 1925. Leo tunaandika historia kuanza kwa ujenzi wa maabar...

MAMCU yauza Tani 8295 za mbaazi kwa bei ya juu 850 na Bei ya chini 81 msimu wa kilimo 2025.......

Mnada rasmi wa zao la mbaazi kwa msimu wa mwaka 2025/2026 umezinduliwa katika kijiji cha Lukuledi, Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.  Uzinduzi huo umefanyika kwa usimamizi wa Afisa Biashara na Masoko, Bi Neema Mmavele, ambaye alieleza kuwa jumla ya tani 8,295.197 za mbaazi zinatarajiwa kuuzwa sokoni msimu huu.  Bi Mmavele alisema kuwa ni matarajio yao kuona wanunuzi wa zao hilo wakijitokeza kwa wingi ili kuhakikisha wakulima wanapata soko la uhakika.  Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika (MAMCU), Bakari Ado, alifafanua kuwa mzigo wa mbaazi uliofikishwa mnadani ni tani 8,295, huku baadhi ya shehena (loti) tatu — yaani loti 50, 52 na 58 — zimeshindwa kuingia mnadani.  Ado alibainisha kuwa kulikuwa na jumla ya loti 61 na zote, isipokuwa hizo tatu, hazikufanikiwar kupata wanunuzi.  Aliongeza kuwa bei ya juu katika mnada huo ilikuwa shilingi 850 kwa kilo, huku bei ya chini ikiwa shilingi 810. Katika kuhakikisha uadilifu wa vipimo wakati wa uuz...

Ummy Mwalimu Avishukuru Vikao Vya Chama,Amuombea Kura Rais Samia

  Alhamdulillah ala kulli hal Nimepokea uamuzi wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa moyo wa shukrani. Quran Tukufu inatufundisha kuwa Allah ndie mpangaji na ni bora kwetu. ALHAMDULILLAH Ndugu zangu wanaTanga Mjini, nitumie fursa hii kuwashukuru kwa kuniamini kuwa Mbunge wenu kwa kipindi cha miaka 5 (2020 - 2025) Nafurahi kuona kuwa utumishi wangu kwenu umewagusa wengi na umeacha alama kubwa za kimaendeleo katika Jimbo letu. Asanteni kwa ushirikiano mzuri mlionipatia ktk kipindi chote cha Utumishi wangu. Kwa dhati ya moyo wangu, ninawashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu maalum wa CCM Wilaya ya Tanga kwa kunipa kura nyingi ktk mchakato wa kura za maoni za kutafuta mgombea ubunge wa CCM katika Jimbo letu Tanga Mjini kwa kipindi cha 2025 - 2030. Mlinikopesha imani kubwa sana Nitaienzi na kuithamini imani hii daima.  UAMUZI wa vikao vya Chama ni lazima UHESHIMIWE. Nampongeza Ndugu Kassim Amar Mbaraka (Makubel) kwa kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM Tanga Mjini.  Ninawaomba wanaki...

Global Education Link, TTB kushirikiana kutangaza utalii kimataifa

Na Mwandishi Wetu WAKALA wa Elimu Nje ya Nchi Global Education Link (GEL) inatarajia kusafirisha wanafunzi zaidi ya 1,000 kwenda kusoma kozi mbalimbali nje ya nchi na imeanza kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), kuwatumia wanafunzi wanaosoma nje ya nchi kutangaza utalii. Hayo yalisemwa jana jijjini Dar es Saaalaam na Mkurugenzi Mkuu wa (GEL), Abdulmalik Mollel, wakati wa kuzungumza na wazazi na wanafunzi wanaotarajiwa kusafiri siku za hivi karibuni kwenda masomoni nje ya nchi. Katika hafla hiyo pia wanafunzi hao walipewa elimu ya mambo ya kufanya na ambayo hawapaswi kufanya wakiwa masomoni nje ya nchi na walipewa nyaraka mbalimbali muhimu za kusafiri nazo kama hati ya kusafiria tayari kwa safari hiyo. Mollel alisema kwa kawaida safari kama hizo huwa zinaanza mwezi wa nane hadi wa kumi na siku ya Jumamosi wanafunzi 100 wanaoondika waliwapewa Visa wale wanaotarajia kuondoka tarehe 27 mwezi huu.  “Kwa mwezi wa nane tarehe 27 wataondoka wanafunzi 100, tarehe10 mwezi wa tisa...