Skip to main content

Posts

Showing posts from June 5, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mndolwa amtaka mkandarasi kuzingatia viwango mradi wa Kasoli-Simiyu

Na MWANDISHI WETU Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Raymond Mndolwa, amefanya ziara ya kushtukiza na kukagua mradi  wa Umwagiliaji Mkoani Simiyu ukiwemo mradi wa ujenzi wa bwawa la Umwagiliaji na skimu ya Kasoli, iliyopo Kata ya Kasoli Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu na kutoa maelekezo kwa watendaji na mkandarasi ikiwemo kuzingatia viwango vya ubora wa ujenzi huo. Akizungumza katika ziara hiyo ya ghafla mkoani humo Mndolwa, amesisitiza kuwa Serikali inatumia zaidi ya shilingi  bilioni 8.021 kama thamani ya mradi huo, hivyo hatakubali kuona utekelezaji wake ukiwa wa kusua sua na viwango kuwa vya chini. “Nataka kuona utekelezaji wa mradi unakuwa ndani ya muda tuliokubaliana lakini pia viwango vya ujenzi vizingatie ubora kulingana na thamani iliyopo,”alisema. Mndolwa, alimtaka Mkandarasi anayetekeleza mradi huo Kampuni ya kigeni iitwayo SIETCO Jv JGC, kuongeza kasi ya utekelezaji wa ujenzi, kujenga barabara ya kuingia eneo la ujenzi na kuhakikisha ujenzi unafanyika kwa...

Nssf Mara yawakumbusha Wachimbaji Madini Kujiwekea Akiba

Na Shomari Binda-Musoma  MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii ( NSSF) mkoa wa Mara imewakumbusha wachimbaji wa madini umuhimu wa kujiwekea akiba. Ukumbusho wa umuhimu huo wa kujiwekea akiba umetolewa jana juni 5,2025 na afisa matekelezo wa mfuko huo Athanas Rukuba wakati akitoa mada kwenye siku ya 2 ya kongamano la maonyesho ya madini mkoa wa Mara kwenye ukumbi wa Mwembeni Complex. Amesema mfuko huo umeanzisha Skimu ya Taifa ya Hifadhi ya Jamii kwa Sekta isiyo Rasmi ambayo wachimbaji walioajiliwa na kujiajili na sekta nyingine wanaweza kujiwekea akiba. Athanas amesema uwekaji wa akiba una umuhimu mkubwa katika maisha ya baadae na serikali kupelekea kutazama upande huo. Amesema kwenye kazi kuna Ä·upata ajali na kuumia pamoja na kuzeeka na kushindwa kufanya kazi hivyo akiba uliyojiwekea inasaidia kuendeleza maisha. Afisa huyo wa NSSF mkoa wa Mara amesema kuumia na kuzeeka kutokana na akiba uliyojiwekea itasaidia pia kusomesha watoto na maisha mengine kuendelea. Amesema taratibu za kujiu...

Rais Samia Amlilia Rais Mstaafu wa Zambia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuma salam za rambirambi kwa Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Hakainde Hichilema kufuatia kifo cha Rais mstaafu wa Zambia Marehemu Edga Chagwa Lungu  Taarifa iliyotolewa na mtandao wake wa Instagram imesema “Nimesikitishwa sana kusikia taarifa za kifo cha Rais wa zamani wa Jamhuri ya Zambia, Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu. Kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, natuma salamu za rambirambi za dhati kwa Mheshimiwa Hakainde Hichilema, Rais wa Jamhuri ya Zambia, familia ya Rais Lungu, marafiki na wananchi wote wa Zambia. Roho yake ipumzike kwa amani.”

Makamu wa Rais Awataka Watanzania Kupanda Miti Kwa Wingi

 Na Ada Ouko, GMTV. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa wadau wote wa mazingira kuendeleza mambo yote yaliyofanyika katika maadhimisho ya mazingira ikiwa ni pamoja na upandaji miti na uanzishwaji wa bustani za kijani. Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Mkoani Dodoma. Amewahimiza wadau hao kuhamasisha matumizi ya teknolojia za urejelezaji wa taka ozo na za plastiki, kupunguza ukataji miti holela kwa ajili ya kuni na mkaa na kuongeza matumizi ya nishati safi ya kupikia. Aidha, Makamu wa Rais amesema Serikali imeweka nia ya kupunguza athari za uharibifu wa mazingira kwa kupunguza matumizi ya nishati ya kuni na mkaa kwa shughuli za kupikia. Amesema katika kutekeleza nia hiyo.  Serikali ilitoa katazo la matumizi ya kuni na mkaa kwa taasisi zinazoandaa chakula na kulisha zaidi ya watu mia moja kwa siku na kuzitaka zih...

Madereva Bajaji Watakiwa Kutunza Amani

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limeutaka umoja wa waendesha Bajaji za mizigo (GUTA) mkoani humo, kutunza amani kwa kutafuta njia sahihi ya kutatua changamoto wanazokutana nazo katika kazi yao. Hayo yamejiri leo Juni 5, 2025 katika Uwanja wa Polisi Mabatini, wakati Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Wilbrod Mutafugwa alipokutana na madereva hao pamoja na uongozi wao, kusikiliza na kujadili kero walizonazo kwa lengo la kupata ufumbuzi. Katika mkutano huo, Kamanda Mutafugwa aliwapongeza madereva hao na uongozi kwa mshikamano wao na ushirikiano na Jeshi la Polisi katika kutanzua na kudhibiti uhalifu.  Pia, aliwataka kuzingatia sheria za usalama barabarani, hasa kuheshimu misafara ya viongozi, magari ya dharura na watumiaji wengine wa barabara. Kikao hicho kimetokana na ombi la Umoja wa waendesha Bajaji kuandika barua ya tarehe 03.06.2025 kwa kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza kuomba kufanya maandamano ya amani tarehe 13 Juni,2025 bila kuweka wazi lengo na dh...

Barrick North Mara Yatoa Elimu ya Usalama Kazini

 Mfanyakazi wa Mgodi wa Barrick North Mara akitoa elimu ya usalama kazini kwa wananchi waliotembelea banda lao leo juni 5, 2025 kwenye maonesho ya madini yanayofanyika Uwanja wa shule ya msingi Mukendo mjini Musoma mkoani Mara. Picha na Ada Ouko

Zambia yaomboleza Kifo cha Rais wake wa Zamani Edgar Chagwa Lungu

   RAIS wa zamani wa Zambia Edgar Lungu ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 68; chama chake, Patriotic Front, kimethibitisha. Lungu alikuwa rais wa taifa hilo la Kusini mwa Afrika kati ya mwaka 2015 na 2021 kabla ya kupoteza katika uchaguzi dhidi ya mshindani wake, rais wa sasa Hakainde Hichilema. “Rais wa zamani, ambaye amekuwa akipokea matibabu maalum nchini Afrika Kusini, aliaga dunia Alhamisi Juni 5, 2025,” ikasema taarifa ya chama chake cha Patriotic Front kwenye mtandao wa Facebook. Katika video fupi, binti yake Tasila Lungu alisema kuwa baba yake alikuwa chini ya uangalizi wa madaktari kwa wiki kadhaa, na akaongeza kwa hisia nyingi: “Katika kipindi hiki cha majonzi, tunaiomba roho ya ‘Zambia Moja, Taifa Moja’ – kauli isiyofifia ambayo alitumia Rais Lungu kuhudumia nchi yetu.” Edgar Lungu aliingia madarakani Januari 2015 baada ya kushinda uchaguzi mdogo uliosababishwa na kifo cha aliyekuwa rais, Michael Sata. Baada ya kukamilisha kipindi kilichosalia cha Sata, Lungu alic...

Wachimbaji wa Madini Kufikiwa na Benki ya NMB kwa Kuwezeshwa Mikopo

Na Shomari Binda-Musoma  BENKI ya NMB imesema inazo fedha za kutosha na wanakwenda kuwafikia wachimbaji kuwapa mikopa na kuendesha shughuli zao za uchimbaji. Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Huduma za Wateja wa Mikopo ya Kati wa benki hiyo Dickson Richard wakati akitoa mada kwenye kongamano la maonyesho ya madini mkoa wa Mara kwenye ukumbi wa Mwembeni Complex leo juni 5,2025. Amesema kwa sasa sekta hiyo ya madini inatambulika zaidi ikiwemo shughuli zake na zipo fedha wanazozitoa źa mikopo katika kuboresha kazi zao. Katika kongamano hilo lililowashirikisha wachimbaji,wauzaji,wachenjuaji na wadau wengine meneja huyo amewaita kuchangamkia fursa hiyo kutoka benki ya kizalendo Amesema fedha zipo na kikubwa ni kufuata taratibu zikiwemo taarifa sahihi ambazo zitapelekea kupata mikopo hiyo kwa haraka. " Ndugu zangu benki ya NMB ni benki yenu na inazo fedha za kutosha kwaajili ya kutoa mikopo kwa wachimbaji na wadau wote wa sekta ya madini. " Nimetoka makao makuu na hapa Musoma ni ny...

Rais Samia Akiwa Katika Matukio Tofauti na Askofu Mkuu Wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Alex Malasusa

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuongoza Harambee ya kuchangia ujenzi wa Kituo cha watoto wenye mahitaji maalum cha Bagamoyo Diaconic Lutheran Centre tarehe 05 Juni, 2025.

Simba Terminal kufufua zao la minazi Tanga

# Yagawa miche 5,000 ya minazi kwa wananchi Gombero wilayani Mkinga.  Tanga: KAMPUNI ya Simba Terminal imegawa miche ya zao la minazi kwa wakazi wa vijiji vitano (5) vya Kata ya Gombero Wilayani Mkinga Mkoani Tanga lengo likiwa kufufua Kilimo hicho na kuimarisha Uchumi kwa Wananchi.  Hatua hiyo umekuja ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali katika kusaidia maendeleo ya jamii, ambapo Meneja miradi wa Simha Terminal Innocent Tirya alisema jana kuwa miche hiyo ya minazi itagaiwa kwa awamu mbili. Katika zoezi hilo la ugawaji wa miche hiyo 3000 lililosimamiwa na wenyeviti wa vijiji vya Gombero, Kivuleni, Mgandi, Jirini Bombo na Jirini Mfuduni Wakazi wake walielezea matumaini yao ya kuimarisha Uchumi wa familia zao kupitia minazi. Katika taarifa yake Meneja wa Simba Terminal Innocent Tirya alisema, kampuni yake chini ya Simba Bingwa imekuwa na utaratibu wa kuchangia maendeleo ya kijamii kutokana na faida inayopata ikiwa sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali katika ku...