Skip to main content

Posts

Showing posts from October 18, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri mkuu ajiandikisha kijijini kwake nandagala ili aweze kumchagua mwenyekiti wake wa kijiji

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameshiriki zoezi la kujiandikisha kwenye Daftari la Mpigakura kwa ajili ya kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, mwaka huu. Waziri Mkuu ambaye alifuatana na mkewe Mama Mary Majaliwa, alijiandikisha leo (Jumamosi, Oktoba 19, 2024) kwenye shule ya msingi Nandagala iliyopo kitongoji cha Nanguruwe, Kata ya Nandagala, wilayani Ruangwa akiwa na baadhi ya wanakijiji wenzake ambao walifika kituoni hapo. Mapema, akitoa taarifa ya uandikishaji, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Ruangwa, Frank Chonya alisema wilaya ya Ruangwa ina tarafa tatu, kata 22, vijiji 90 na vitongoji 435 ambavyo vitahusika kwenye uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Vijiji. Alisema wilaya hiyo imekadiria kuandikisha wakazi 123,803 ambapo kati yao 60,188 ni wanaume na 63,615 ni wanawake. “Hadi kufikia tarehe 18 Oktoba, 2024, tumefanikiwa kuandikisha jumla ya watu 103,468 ambapo kati yao wanaume ni 47,664 na wanawake ni 55,804.” Alisema zoezi hilo...

Waziri Kikwete aongoza kikao cha wizara na menejiment ya mfuko w Psssf

Kikao cha Wizara na Menejiment ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kimefanyika Oktoba 18 Mwaka huu Bungeni Dodoma,Kikao kimejadili taarifa  ya Utekelezaji wa majukumu ya Mfuko huo kwa Mwaka wa fedha 2023/2024.

Ridhiwani Kikwete ajiandikisha kupiga kura msoga

-Apongeza spidi ya uandikishaji Halmashauri Chalinze na Mkoa wa Pwani. -Ashukuru kuongezwa kwa vituo vya uandikishwaji kutatua tatizo la umbali Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu ambaye pia ni Mbunge wa Chalinze amefika kijijini kwao Msoga, Chalinze kujiandikisha ikiwa ni kutimiza takwa la katiba la kujiandikisha ili apate nafasi ya kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Vijiji unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024.  Akizungumza baada ya kumaliza kujiandikisha , Mh. Kikwete amepongeza sana utulivu katika kipindi hiki cha uandikishaji. “…. Amani ni tunu yetu, na muhimu kujitambulisha nayo kwa vitendo na Watanzania wanathibitisha hili kwa vitendo”, alisema Waziri Kikwete. Pamoja na kuwapongeza Watanzania kwa utulivu pia alishukuru Serikali kwa kuamua kuongeza vituo vya kujiandikisha kutokana na wananchi kulalamika kutembea umba mrefu kufuata kituo cha kujiandikisha. Waziri Kikwete alisema, “…. Naishukuru na kuipongeza Serikali...

Waziri anusuru maelfu ya abiria na magari yaliyokwama baada ya barabara kufungwa

Wananchi wa kijiji cha Magubike wilayani Kilosa  Mkoani Morogoro wamefunga barabara kuu ya Dodoma-Morogoro kwa zaidi ya saa Saba baada ya mtoto Nuru anayesoma elimu ya awali kugongwa na gari inayodaiwa kuwa ya serikali. Kufungwa kwa barabara hiyo kuu ya Morogoro -Dodoma kumesabisha msururi mkubwa wa magari  yakiwemo mabasi ya abiria Uamuzi wa kufunga barabara hiyo umechukuliwa na wananchi ili kushinikiza serikali kuweka matuta kwenye eneo hilo ili kupunguza ajali zinazotokea Mara kwa Mara na kukatisha uhai wa baadhi ya watu na kujeruhi wengine.   Mwenyekiti wa kijiji cha Magubike Salum Chapa wamesema kwa kipindi kifupi tayari watu tisa wamegongwa katika eneo hilo na hakuna hatua ambazo zimechukuliwa Miongoni wa watu waliokwama kufuatia kufungwa kwa barabara hiyo ni pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt.Seleman Jafo na Msafara wake.  Akiwa katika eneo hilo,Dkt.Jafo alilazimika kuzungumza kwa njia ya siku na Waziri wa ujenzi Innocent Bashungwa ambaye am...

Wanu Hafidh Ameir;Kupata elimu ya afya ni Jambo moja,lakini muhimu sana ni kupima kujua afya yako

  Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) imefanikiwa kukuza ufaulu na kupunguza Sifuri katika Mkoa wa Kusini Unguja kwa Asilimia 84 Mwaka 2022/2023 kutoka Asilimia 68 kwa Mwaka 2020/2021. Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Mhe.Wanu Hafidh Ameir amebainisha hayo visiwani Zanzibar wakati wa maadhimisho ya siku ya saratani.  Mhe.Wanu ameongeza kuwa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) pia inajivunia kuweza kuwasomesha Wanafunzi 114 walioshindwa kuendelea na Elimu ya Juu mafunzo ya Amali  takribani Wanafunzi 114 katika Vyuo vya Amali ikiwemo Makunduchi na Mkokoteni.  "Katika suala la Afya, Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) tumekuwa tukishajihisha Vijana, Wanawake na Wanaume kwenye Afya ya Akili kupitia Semina mbalimbali na Michezo kama vile Marathon, Netball, Football na Michezo mingine mbalimbali" Alisema Mhe. Wanu Hafidh Ameir na kuongeza kuwa "MIF kwenye masuala ya Afya, tumeweza kuwabadilisha akina Mama takribani 2,000 kutoka kwenye matumizi ya Nish...

Tbs yaondoa tatizo la choo katika shule ya msingi chamugasa

S hirika la Viwango Tanzania (TBS) limesaidia utatuzi wa changamoto ya upungufu wa vyoo katika shule ya msingi Chamgasa iliyopo Kata ya Kalemela, Wilaya ya Busega mkoani Simiyu baada ya kuchangia kiasi cha shilingi milioni saba. Akizungumza Ijumaa Oktoba 18, 2024 kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TBS- Ashura Katunzi, Meneja wa shirika hilo Kanda ya Ziwa- Happy Kanyeka amesema hatua hiyo ni sehemu ya shirika kuunga mkono jitihada za Serikali kutatua changamoto za kijamii. “Tunarudisha kwa jamii kile tunachokipata, hatua hii ni sehemu ya kuwezesha juhudi na jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kuboresha mazingira ya wanafunzi kujifunza” alisema Kanyeka. Pia Kanyeka alitumia fursa hiyo kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule hiyo kutambua bidhaa zilizothibitishwa na TBS akiwaasa kukagua nembo ya TBS wanapoaizwa mahitaji mbalimbali akisema; “ukitumwa dukani kununua soda, maji, madaftari na bidhaa nyingine haki...

Waziri Mkuu;Serikali yatoa billioni 3.5 kujenga barabara ya lami milola

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imepeleka fedha za ujenzi wa barabara mkoani Lindi na amemwagiza Meneja wa TANROADS wa mkoa huo, Mhandisi Emil Silas Zengo ahakikishe barabara ya Kata ya Milola inawekwa lami mapema iwezekanavyo. Amefikia hatua hiyo baada ya Mhandisi Zengo kukiri kuwa walishapokea fedha kiasi cha sh.bilioni 3.5 ambazo  zililenga kujenga barabara ya Milalo Centre yenye urefu wa kilometa nne, kujenga mitaro na kuweka taa za barabarani.  Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo jioni (Ijumaa, Oktoba 18, 2024) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa kijiji cha Milola, kwenye mkutano uliofanyika kwenye senta ya Milola,  kata ya Milola, wilayani Lindi. Mhandisi huyo amesema Jumatatu ijayo (Oktoba21, 2024), wataalam wataenda kwenye kata hiyo ili waweze kuanza kazi ya usanifu na hatua nyingine za msingi zitaendelea ili baada ya mwezi mmoja, mkandarasi aanze kazi. Wakati huohuo,  Waziri Mkuu amesema Serikali ya Rais Samia imekwishatoa sh. bilioni 1.8 kwa...

Umoja wa mabunge duniani umedhamiria kurejesha amani kwenye maeneo yenye migogoro duniani

 Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 17 Oktoba, 2024, amehitimisha rasmi Mkutano Mkuu wa 149 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (CICG) mjini Geneva, Uswisi. Mkutano huo umejadili mada kuu inayohusu “Matumizi ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kwa ajili ya mustakabali wa Amani na Uendelevu”. Aidha, Mkutano wa 149 umepitisha maazimio kadhaa yanayolenga kurejesha amani katika maeneo yenye migogoro duniani kwa kutumia njia za majadiliano ya kidiplomasia.  Maazimio hayo pia yamejumuisha matumizi ya akili mnemba (AI) katika kuimarisha demokrasia, haki za binadamu na maamuzi ya kisheria, pamoja na rasimu ya mabadiliko ya sheria za uendeshaji wa Baraza la Uongozi na Mkutano Mkuu wa IPU.

Tpa kanda ya ziwa victoria yahamasisha uandikishaji wapiga kura katika daftari la makazi

  Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA)Kanda ya ziwa Victoria imewaasa watanzania kujitokeza kujiandikisha kwenye Daftari la Makazi ili waweze kupata haki ya kuchagua viongozi wanaowataka kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27 Mwaka huu. Meneja wa Mamlaka hiyo Erasto Lugenge ametoa wito huo wakati alipowaongoza baadhi ya wafanyakazi wa Tpa wanaoishi kwenye mtaa wa soko kuu kata ya pamba Jijini Mwanza katika zoezi la uandikishaji kwenye daftari la makazi la wapiga kura. ‘’Tumekuja kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura uchaguzi wa serikali za mitaa na kama unavyofahamu Bandari ni sehemu ambayo inaongozwa na uongozi wa serikali za mitaa,kwa maana ya kwamba tuna wafanyakazi wanaoishi kwenye serikali za mitaa na vitongoji vyake,abiria wanaosafiri kutumia bandari zetu huwa wanatoka serikali za mitaa lakini tuna wateja na wafanyabiashara wanaotoka serikali za mitaa na zaidi ya hapo miundombinu inayoingia na kutoka bandarini inahudumiwa na serikali za mitaa’...