Skip to main content

Posts

Showing posts from March 14, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

JWTZ Yahitimisha Mafunzo ya Soka la Ufukweni

  Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Brigedia Jenerali Simon Pigapiga amefunga rasmi mafunzo ya Mchezo wa Soka la Ufukweni  yaliyoendeshwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa Wanajeshi wa JWTZ Katika Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa Mbweni leo tarehe 14 Machi 25. Akimwakilisha Mkuu wa Utumishi Jeshini Meja Jenerali Marco Gaguti, Brigedia Jenerali Pigapiga amewataka wahitimu wa mchezo huo kutumia mafunzo hayo kwa kuwafunza Maafisa na Askari wengine wa JWTZ ili mchezo huo uwe na tija katika mashindano mbalimbali Jeshini.  Aidha, Brigedia Jenerali Pigapiga ameshukuru Uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini kwa usimamizi wa mafunzo hayo. Akizungumza kwa niaba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu(TFF), Rais wa Shirikisho Bw. Wallace Karia, amesema, Tff inaendelea kushirikiana na JWTZ katika kukuza na kuinua mchezo wa soka nchini, na kuwaomba wahitimu wa mafunzo haya kutumia elimu na maarifa ya mchezo wa Soka la Ufukweni kuw...

Kamati ya Bunge yaridhishwa ujenzi daraja la Pangani

📍 Yaomba barabara ya Tanga Pangani, Bagamoyo ipitie hifadhi ya Saadan  Na MASHAKA MHANDO, Pangani  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeishauri Wakala wa barabara nchini (TANROADS) kufanya uwezekano wa barabara ya Tanga, Pangani Makurunge wilayani Bagamoyo inapita katika hifadhi ya Taifa ya Saadan ili kuongeza watalii na kuitangaza hifadhi hiyo. Akizungumza katika majumuisho baada ya Kamati hiyo kukagua na kutembelea mradi wa barabara ya Tanga Pangani pamoja na daraja la mto Pangani, mwenyekiti wa Kamati alisema kuichepusha barabara hiyo katika eneo jingine, hakuna tija. Alisema Kamati ya Bunge ingependa kuona wataalamu wa Wizara ya ujenzi na Ofisi ya Makamo wa Rais Mazingira wanashirikiana kuona uwezekano wa barabara hiyo kupitia katika hifadhi ya Saadan kuliko sasa inapitia eneo jingine. "Narudi mara ya pili, Bunge lingependa sana barabara ya kutoka Tanga ingeenda kupitia kwenye hifadhi ya Saadan itafungua mkoa kiuchumi na kuongeza idadi ya watalii," alisema na kuo...

Wadau wa Habari Waipongeza Misa Tanzania Kwa Kuwaleta Wadau Pamoja

Mwandishi wetu ;Dodoma Wadau wa habari Tanzania wameipongeza Taasisi ya MISA Tan Kwa kuwa na uthubutu wa kuwaleta wadau wa habari katika kongamano la MISA Wadau Summit 2025 Jijini Dodoma. Mwakilishi toka PSSSF Bwana Valentino Maganga alisema kuwa, Taasisi ya MISA imefanya jambo la kipekee Kwa kuandaa kongamano na kuwa na muda wa kujadili masuala ya kiuchumi. Binafsi yetu kama PSSSF tunaamini kuwa, bila vyombo vya habari ni vigumu wananchi kuelewa wajibu wetu na kazi zetu. Naye Mhandisi Andrew Kisaka amesema kuwa anaishukuru MISA Tan Kwa kutoa nafasi ya TCRA kutoa elimu ya kanuni za uchaguzi. Naye Josephine Joseph toka TASAF alisema kuwa, anaishukuru MISA Tan Kwa kutoa nafasi ya kujadili maendeleo ya kiuchumi kupitia vyombo vya habari, hilo ni jambo zuri sana. Naye Mwenyekiti wa MISA Tanzania Bwana Edwin Soko alisema kuwa, kongamano la MISA hilo ni mwendelezo wa jitihada za MISA kwenye kujenga  mahusiano na wadau wa habari hapa Nchini. MISA Wadau SUMMIT 2025 imefanyika Jijini Dodoma...

Waziri Mkuu Azindua Msikiti wa Nuuril Hikma

_▪️Awataka waumini kuutunza msikiti huo_ _▪️Atoa wito kwa viongozi wa dini kuliombea Taifa na kukemea maovu_   WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Machi 14, 2025 amezindua msikiti wa Masjid Jaami’u Nuuril Hikma uliopo mtaa wa Yombo, Temeke jijini Dar es Salaam ambao umejengwa na Taasisi ya Al-Hikma Akizungumza baada ya kuzindua msikiti huo, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa jamii na Watanzania watakaotumia msikiti huo kuutunza kwani kufanya hivyo ni njia ya kudumisha uhusiano na Mwenyezi Mungu na inahesabika kama sadaka. “Mtume Muhamad S.A.W anatufundisha pia kutunza nyumba za ibada, msikiti ni sehemu ya jamii na ni mahali pa ibada na umoja. Kupitia hadithi ya Bukhari, ni wajibu wa waumini kutunza msikiti, kuhakikisha kwamba ni sehemu safi, na inakidhi mahitaji ya ibada na mafunzo ya kiislamu.” Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa msikiti ni kituo cha kiroho, kijamii, kiutamaduni na nyumba kwa ajili ya ibada na unatoa nafasi kwa waumini kushirikiana katika ibada, kujifunza, n...

Naomba Tumuelewe Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Suala la Degree Twendeni Veta!

  Na Michael  Uled Baada ya kukaa mtaani kwa miaka miwili bila KAZI,sikuwa na Option nyingine!Katika pita pita zangu niliona tangazo la ajira kutoka kampuni ya Uchimbaji Madini ya Shanta Gold Mining Tanzania! Kumbuka nilikuwa mtaani nikiwa na Elimu yangu ya (Masters)lakini sikuwa na KAZI kwa miaka zaidi ya miwili au mitatu hivi Haikuwa rahisi! Tangazo lile la KAZI la Shanta lilikuwa linahitaji watu wa (CCTV Camera Operative),wenye sifa mdogo ndogo kama kupitia kozi za JKT! Lakini pia sifa kuu ilikuwa ni kuwa Elimu angalau ya form four tu!Pamoja na kuwa na Elimu yangu ya Master Of Arts in Communication lakini sikusita kuomba! ILIKUWA HIVI!👇🏿👇🏿 Nafasi ile ilikuwa inahitaji mtu mwenye Elimu ndogo tu ya Form four lakini pia mwenye "skills" za CCTV operation tu! Baada ya kuomba KAZI ile ya "form Four" nilipata!Kwahiyo Degree zangu mbili nikaweka pembeni nikawa natumia cheti cha form four lakini huku nikiwa na Mshahara mzuri sana!Ajira nyingi kwa sasa zipo kwa watu we...