Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya Kichina ya CRJE (East Africa) Limited imesema mradi wa ujenzi ambao upo kwenye hatua za mwisho kabisa wenye thamani ya Tsh10.8 bilioni katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) unatarajiwa kukabidhiwa rasmi kwa Taasisi hiyo iliyo chini ya Wizara ya Uchukuzi mwezi huu. Kampuni ya CRJE (East Africa) Limited imejenga majengo mawili katika Chuo hicho kupitia Mradi wa Eastern Africa Skills for Transformation and Regional Integration (EASTRIP) ambao umefadhiliwa na Benki ya Dunia wenye lengo la kuendeleza Kituo cha Umahiri katika Usafiri wa Anga. Akizungumza katika mahojiano jana jijini Dar es Salaam, Dai Yanwei, Msimamizi wa mradi huo kutoka CRJE (East Africa) Limited alisema: “Tumefanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha mradi huu unakamilika mapema iwezekanavyo. Tuna Mshukuru Mungu tumekamilisha salama na hivi sasa tupo kwenye hatua ndogo ndogo za mwisho ili tuweze kukabidhi mradi huu kwa Chuo.” Mnamo Novemba 2022, NIT imeingia mkataba wa mwaka mmoj...
Marato tv - Sauti ya Jamii