Mwanasheria mkuu wa serikali Mh Hamza Johari amewataka Watanzania kutembelea eneo alilozaliwa na kuzikwa Baba wa Taifa hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere, hatua ambayo akesema itawawezesha kujifunza mambo mbalimbali yalifanywa na kiongozi huyo kwa enzi za uhai wake. Akizungumza baada ya kutembelea nyumbani kwa Baba wa Taifa eneo la Mwitongo, kijijini Butiama,Mwanasheria huyo mkuu wa serikali,amesema kufika eneo hilo ni darasa tosha la kufahamu vema historia ya nchi na Baba wa Taifa wa Taifa. "Tumeona nyumba aliyojengewa na jeshi la wananchi,tumeona vitu vingi vya kujifunza kuhusu Mwl Nyerere pia tumefika kwenye kaburi na kumwombea dua,nawaasa watanzania wengine wakipata nafasi kufika Mara, wafike Butiama ili kupata maelezo ya kazi zake alizowahi kuzifanya wakati wa uhui wake" alisema Mh Hamza Johari. Hata hivyo Mwanasheria mkuu wa serikali, amepata nafasi ya kupanda juu ya jiwe ulipo Mwenge wa Mwitongo ambao umeasisiwa na Baba wa taifa na kila mwaka wakati wa mbio...