Skip to main content

Posts

Showing posts from September 10, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Fahamu Mambo Muhimu ya Kuzingatia Kabla ya Kununua Vifaa Vya Umeme wa Solar

Na Emmanuel Chibasa Umeme wa solar ni aina ya umeme unaozalishwa kwa kutumia mionzi ya jua. Paneli za solar, ambazo hujulikana pia kama photovoltaic (PV) panels, zinakusanya mionzi ya jua na kuibadilisha kuwa umeme wa kutumia nyumbani, ofisini, au kwenye shughuli nyingine za kibiashara. Mfumo wa umeme wa solar unajumuisha paneli za solar, battery za kuhifadhi umeme, na inverter ambazo hubadilisha umeme wa DC (Direct Current) kutoka kwenye paneli kuwa umeme wa AC (Alternating Current) unaotumika katika vifaa vya umeme vya kawaida. Umeme wa solar unafaa kwa shughuli nyingi, hasa katika maeneo ambapo umeme wa gridi ya taifa haupo au unapatikana kwa ukawaida. Mfumo huu ni wa kuaminika na wa gharama nafuu, kwani unategemea chanzo cha nishati kisicho na mipaka—jua. Hivyo, umeme wa solar unafaa kwa matumizi mbalimbali kama vile mwanga wa nyumba, matumizi ya vifaa vya kielektroniki, na hata kwa biashara ndogo na mashamba. Licha ya umeme wa solar kuwa nafuu na uhakika Kwa Matumizi Mbalimbali ha...

Waziri Jafo azindua Maonesho ya 19 ya Afrika Mashariki

Waziri wa viwanda na biashara Dkt. Seleman Jafo amesema kuwa serikali imeendelea kuondoa vikwazo kadhaa vya kibiashara ikiwemo kurahisisha upatikanaji wa vibali ili kuvutia uwekezaji kutoka ndani na nje ya nchi. Akizindua maonesho ya 19 ya biashara ya afrika mashariki yanayofanyika kwenye viwanja wa Furahisha Jijini Mwanza Jafo amewahasa wawekezaji kutumia fursa ya uwepo wa mazingira mazuri kuwekeza kwenye sekta mbalimbali ikiwemo viwanda na kilimo. Amesema kuwa ongezeko la uwekezaji nchini ni muhimu katika kuchochea ukuaji wa Uchumi,kuongeza nafasi za ajira Pamoja na kuongeza pato la Taifa Aidha amezitaka halmashauri nchini kutenga maeneo ya uwekezaji Pamoja na Maeneo maalum ya maonesho ya kibiashara ili kurahisisha upatikanaji wa masoko ya bidhaa zinazozalishwa nchini. Maonesho hayo yameandaliwa na chama cha wafanyabiashara,wenye viwanda na kilimo(TCCIA)Mkoa wa Mwanza ambapo pia waziri Jafo amekitaka chama hicho kuandaa maonesho hayo katika ngazi ya Taifa. Naye mwenyekiti wa TCCIA mk...

WAZIRI MKUU:SUALA LA MAZINGIRA LIWE KITAIFA

 *WAZIRI MKUU: SUALA LA MAZINGIRA LIWE AJENDA YA KITAIFA* WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema suala la uhifadhi wa mazingira liwe ajenda ya Kitaifa na jukumu la kila mmoja kuanzia ngazi ya familia mpaka Taifa.   “Na tunapokwenda kuhifadhi mazingira lazima tuanze na ngazi ya familia na tunapopanda juu tupanue wigo hadi kwa wadau mbalimbali. Viongozi wa dini mnayo nafasi kubwa na hii lazima iwe ajenda maalum, iwe ni ofisi za umma, za binafsi au kwenye taasisi.” Ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Septemba 10, 2024) wakati akifunga mkutano maalum wa viongozi na wadau wa mazingira ulioitishwa ili kujadili mwenendo wa mazingira nchini. Mkutano huo ulifanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.  Amesema kitendo hicho kitakuwa ni kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuendelea kuimarisha uhifadhi na Usimamizi wa mazingira nchini, kazi aliyoifanya kwa weledi, ustadi na mafanikio tangu akiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani...

Wanafunzi 62,214 Kufanya Mtihani wa Darasa la Saba Mkoani Mara

Na Shomari Binda-Musoma WANAFUNZI 62,214 kutoka Mkoa wa Mara wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi utakaoanza kesho Septemba 11. Akizungumza na George Marato Tv leo ofisini kwake Katibu Tawala mkoa wa Mara Gerald Kusaya amesema kati ya wanafunzi hao wavulana ni 29,424 na wasichana ni 32,790. Amesema wanafunzi hao wanatarajiwa kufanya mtihani wa darasa la 7 kwenye shule 876 ambazo zitakuwa ni vituo vya mtihani. Kusaya amesema wanafunzi hao ni wale walioandikishwa darasa la kwanza mwaka 2018 na wanakamilisha mzunguko wao wa kielimu wa miaka 7 mwaka 2024 na watakuwa kwenye mikondo 2,756 Ameongeza kuwa mwaka huu Baraza la Mitihani Tanzania limefanya maboresho mapya kwa mwaka 2024 tofauti na yaliyofanyika 2013 ambapo mtihani wa kuhitimu darasa la 7 utajibiwa kwenye karatasi za maswali. Amesema hiyo imetokana na Baraza la Mitihani kufanya mabadiliko ya utunzi wa mitihani kwa kufuata mtindo mpya ( Format) hivyo hakutakuwa na OMR za kujibia. " Mitihani hii itafanyika kw...

Mhandisi Kundo Methew Awataka Wananchi Bukoba Kulinda na Kutunza Miundombinu ya Miradi ya Maji

  Na Angela Sebastian-Bukoba  Naibu waziri wa maji Mhandisi Kundo Mathew amewataka wananchi katika wilaya ya Bukoba kunakochimbwa visima jumla ya 15 kulinda na kutunza miundo mbinu inayojengwa katika maeneo kunakochimbwa visima hivyo. Amesema hiyo itasaidia  kuhakikisha miundombinu hiyo inadumu na inatoa huduma ya maji kwa muda mrefu kama ilivyokusudiwa. Mhandisi Methew amesema hayo baada ya kushuhudia uchimbaji wa kisima cha maji katika kata ya Kyaitoke   wilaya ya Bukoba ambapo pia aliizungumza na wananchi wa kata hiyo, akawaasa wananchi kunakochimbwa visima 15 kulinda miundombinu ya maji itakayojengwa katika maeneo yao.  Evodius Ishengoma ni mwananchi wa kata hiyo aliishukuru serikali kwa kuona umuwa kuchmbq kisima hicho katika maeneo yao ambapo itasaidia kuepuka adha ambayo wanaipata  ya kutumia maji ya madimbwi ambayo si salama kwa Afya zao maana visima vilivyokuwepo awali vimeharibika. Uchimbaji wa kisima  kimoja unagharimu kati ya shilingi ...