Skip to main content

Posts

Showing posts from March 20, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Shule ya Hazina yampongeza Rais Samia miaka minne kwa kuinua sekta ya elimu

Na Mwandishi Wetu UONGOZI wa Shule ya Hazina  Magomeni jijini Dar es Salaam umempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa miaka minne ya mafanikio kwenye sekta mbalimbali ikiwemo kuipasha sekta ya elimu. Kwa mujibu wa Mkuu wa shule hiyo, Omari Juma Rais Samia amefanya mambo makubwa hususan kwenye elimu ambapo amewezesha wanafunzi wengi kupata elimu ya msingi hadi sekondari. Shule ya Hazina imekuwa kinara kwa kuwa namba moja kwenye matokeo ya darasa la nne na lasaba kwenye Wilaya ya Kinondoni na Mkoa wa Dar es Salaam kwa miaka mingi.  Alisema Rais Samia amefanikiwa kujenga shule za wasichana za sayansi zinazojulikana kwa jina la Mama Samia kwenye mikoa mbalimbali hivyo kuwapa fursa wasichana wa kitanzania kusomea masomo ya sayansi kwa wingi. “Hazina mdau mkubwa wa elimu tumekuwa tukiongoza Wilaya ya Kinondoni na Mkoa wa Dar es Salaam karibu kila mwaka kwa kuwa wakwanza kwenye matokeo ya darasa la saba kwa hiyo tunapoona sekta ya elimu inapewa kipaumbele inatutia moyo sana kamawadau ...

Kikosi cha Taifa Stars Chakabidhiwa Bendera ya Taifa...

 Mashaka Mhando, Tanga NAIBU Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo mhe Hamis Mwinjuma maarufu MwanaFA, amewakabidhi Bendera ya Taifa, timu ya Tanzania 'Taifa Stars' kabla ya mchezo muhimu wa kuwania kufudhu kombe la Dunia 2026 dhidi ya Morocco, mchezo unatarajiwa kuchezwa Machi 26, 2025. Akizungumza Leo Machi 20, 2025 Jiji Tanga kwenye iftar iliyoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), MwanaFA alisema Watanzania wakiongozwa na mwana-Michezo namba moja nchini Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, watakuwa nyuma yao hivyo wakatangulize uzalendo, maarifa na mbinu ili kushinda mchezo huo. Alisema licha ya kwamba, Stars wanakwenda kucheza na timu namba moja Africa, Taifa Stars wana uwezo wa kushinda mchezo huo ikiwa watajituma na kuwa na dhamira ya dhati, uzalendo wa nchi, wanaweza kushinda mchezo huo. Alisema mchezo huo ni muhimu kushinda kutokana na kwamba ushindi utaiweka Tanzania katika nafasi nzuri ya kufudhu kucheza kombe la Dunia mwakani. "Morocco watakuwa...

Uwt Mara yampongeza Rhobi Samwelly Kuwa Kinara wa Kupambana na Ukatili wa Kijinsia

Na Shomari Binda-Musoma  BARAZA la Jumuiya ya Wanawake wa CCM ( UWT) mkoa wa Mara imempongeza Rhobi Samwelly kwa kuwa kinara wa kupambana na matukio ya ukatili wa kijinsia. Pongezi hizo zimetolewa machi 20,2025 na Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Nancy Msafiri kwenye kikao cha baraza hilo. Amesema kupitia kituo chake cha Nyumba Salama kilichopo Serenveti na Butiama kwa kupokea na kuwahifadhi watoto wa kike na wasichana wanaokutana na matukio ya ukatili. Nancy amesema Rhobi amekuwa kinara na kazi yake inaonekana na jumuiya itaendelea kumpa ushitikianl katika jitihada zake za shughuli anayoifanya. " Tunakupongeza sana ndugu yetu Rhobi kwa kazi kubwa unayoifanya katika kupambana na matukio ya ukatili wa kijinsia. " Sisi UWT mkoa wa Mara tutakupa ushirikiano wote na kushirikiana nawe kwa hii kazi njema unayoifanya na Mungu atakulipa",amesema. Awali akitoa taarifa ya masuala ya ukatili kwenye baraza hilo Rhobi Samwelly ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kupinga Ukatili wa UWT mkoa w...

Dc Sima Afanya Ziara Tarafa ya Katerero, Rubale na Bugabo Kukagua Miradi ya Maji

_Aongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama. Asema Rais Samia amedhamiria kumaliza changamoto ya maji kila mahali._ Mkuu wa Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera Mhe. Erasto Sima amesema Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imejipanga kumaliza changamoto ya maji wilayani Bukoba kwa jinsi inavyotekeleza miradi mikubwa kila mahali huku akiwataka wananchi na viongozi kutunza vyanzo vya maji ili miradi hiyo iwe endelevu.  DC Sima ameyasema hayo leo Alhamisi Machi 20, 2025 akiongozana na Kamati nzima ya Ulinzi na Usalama kwenye ukaguzi wa miradi ya maji Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba kwenye Tarafa ya Katerero, Rubale na Bugabo. DC Sima na Kamati wamefanya ukaguzi wa miradi 5 ya maji inavyotekelezwa na mingine ambayo wananchi wameanza kupata huduma ya maji kupitia usimamizi wa RUWASA. Kwenye ziara hii, DC Sima na Kamati ya Ulinzi na Usalama wamekagua mradi wa maji wa Kata ya Katoro na Bujugo kwenye Tarafa ya Katerero, mradi wa Migara na kuzungumza na viongozi wa Jumuia za watumia maji (CBWSO) ka...

Raila Odinga Avuna Matunda ya Handshake na Rais Ruto

  MKATABA wa ushirikiano ambao Kiongozi wa ODM Raila Odinga alitia saini na serikali ya Kenya Kwanza unaendelea kuzaa matunda huku washirika wake wakinufaika na nyadhifa za makatibu wa wizara. Katika mabadiliko ambayo Rais William Ruto alifanyia makatibu wakuu wa wizara Alhamisi, Machi 20, 2025, washirika wa Bwana Odinga waliteuliwa kuhudumu katika Idara za wizara muhimu. Katika mabadiliko hayo, Rais Ruto aliteua makatibu 14 wapya, zaidi ya 10 wakiwa washirika wa Bw Odinga na kuwahamisha sita kupisha wale wa waziri mkuu huyo wa zamani. Katika taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Ikulu, Hussein Mohammed, Rais Ruto amemhamisha Amos Gathecha kutoka wizara ya utumishi wa umma na kumteua kuwa Naibu Mkuu wa Huduma za Umma. Prof Edwin Kisiangani, ambaye alikuwa akihudumu katika Wizara ya ICT, sasa atahudumu kama mshauri na mwanachama wa baraza la washauri wa kiuchumi wa rais. Makatibu wapya 14 wanaohusishwa na Raila ni pamoja na Dkt Jane Kare Imbunya (Idara ya Utumishi wa Umma), Bi Regina Ak...

Waziri Kikwete: Vyama Vya Wafanyakazi ni Nguzo ya Mahusiano Mema ya Kazi Mahali Pa Kazi

Na, Mwandishi Wetu - DODOMA Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Vyama vya Wafanyakazi ni nguzo muhimu katika kujenga mahusiano yenye tija mahali pa kazi. Amebainisha hayo leo Machi 3, 2025 Jijini Dodoma katika mkutano wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli na Shughuli zinazohusiana na Reli (RAWUTA), ambapo amesema kuwa Vyama hivyo vya Wafanyakazi ni vyombo vinavyotetea masuala yote yanayogusa maslahi na haki zao za msingi. “Vyama vya Wafanyakazi nchini vimeendelea kuimarika na kuwa nguzo muhimu katika kusimamia maslahi ya Watumishi na Utatuzi wa migogoro, hivyo mazingira ya kazi yanakuwa bora kwa ustawi wa wafanyakazi na maendeleo ya taifa kwa ujumla,” amesema. Aidha, Mhe. Kikwete amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuweka mazingira ya kukuza ustawi wa vyama vya Wafanyakazi mahali pa kazi sambamba na kuendelea kuhamasisha uanzishwaji wa mabaraza ya Wafanyakazi il...

Rais Dkt. Samia Achangia Sh. Milioni 50 Kumuenzi Padri Shirima

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa shilingi milioni 50 kwa ajili ya maendeleo ya Shule ya Sekondari ya Seminari Uru, mkoani Kilimanjaro. Mchango huo umetolewa ili kuweka alama ya kumbukumbu ya kumuenzi marehemu Padri Canute Mkwe Shirima AJ, aliyewahi kuwa Baba Gombera wa shule hiyo, mojawapo ya seminari maarufu nchini. Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, alitangaza mchango huo kwa niaba ya Rais Dkt. Samia alipokuwa akitoa salaam za pole na rambirambi katika ibada ya mazishi ya Padri Shirima, iliyofanyika Seminari ya Uru, Alhamisi, Machi 20, 2025. “Haya yote niliyoyasema hapa kumhusu Baba Gombera mstaafu Padri Canute Shirima, alivyokuwa mlezi mzuri akifundisha nidhamu na uwajibikaji, nilimwambia Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. “Nilimtaarifu kuwa nakatisha ziara ili kuhudhuria mazishi haya. Mheshimiwa Rais akaniambia anatoa shilingi milioni 50 kwa Seminari ya Uru...