Skip to main content

Posts

Showing posts from March 13, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mkutano wa Mawaziri wa Sadc Wamalizika, Wasisitiza Miradi Yenye Tija Kwa Wananchi

Mkutano wa siku mbili wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umehitimishwa jijini Pretoria, Afrika Kusini Machi 13, 2026. Madhumuni ya mkutano huo yalikuwa ni kupanua kasi ya mtangamano wa kikanda kwa ajili ya kuharakisha maendeleo ili kutengeneza ajira, kuimarisha usalama wa chakula na upatikanaji wa nishati kwa wananchi. Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo uliongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe ambaye aliambatana na Naibu Waziri wa Fedha. Mhe. Laurent Luswetula. Katika hotuba yake ya kufunga, Mwenyekiti wa Mkutano huo ambaye ni Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Kusini, Mhe. Ronald Lamola alisisitiza umuhimu wa nchi wanachama kuwa na umoja na mshikamano ili kutekeleza kwa ukamilifu yale yaliyojadiliwa katika mkutano huo. Katika majadiliano hayo, pamoja na mambo mengine, Mawaziri walisisitiza umuhimu wa kuharakisha utekelezaji wa miradi ya kikanda hasa ujenzi wa mi...

CCM yamtimua meneja Machai Mkwakwani

📍Sababu kubwa yaelezwa kushindwa kuiondoa baa ya Thinkers  📍Mwenyekiti Ustadh Rajab ashusha maelekezo mazito *Na Mashaka Mhando, Tanga* Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga, imemuagiza Katibu wa CCM Mkoa kusitisha mkataba wa Meneja wa Uwanja wa Mkwakwani, Akida Machai, kufuatia kusuasua kwa utendaji na usimamizi mbovu wa miundombinu ya uwanja huo wa kihistoria. Maamuzi hayo magumu yamefikiwa Leo Machi 11 2026 na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Komredi Rajab Abdurahman, wakati wa ziara maalum ya Kamati ya Siasa ya Mkoa iliyolenga kukagua maendeleo ya ukarabati na hali ya uwanja huo unaomilikiwa na Chama. Akizungumza kwa uchungu mbele ya wajumbe wa kamati hiyo, Mwenyekiti Rajab alisema Chama hakiwezi kuvumilia uzembe wa mtendaji mmoja unahatarisha hadhi ya uwanja huo, huku CCM ikigharamia mahitaji yote muhimu ikiwemo maji na umeme bila kupata tija inayostahili. “CCM tunatoa fedha kuhakikisha wananchi wanapata burudani, lakini usimamizi ni sifuri. Mimi binafsi...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Aapishwa Kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza S. Johari tarehe 13 Machi, 2026 ameapishwa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama, katika hafla fupi ya uapisho iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Tume ya Utumishi wa Mahakama, Jijini Dodoma. Mhe. Johari ameapa mbele ya Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama na Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George M. Masaju,  kufuatia kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Tume hiyo. Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameteuliwa kuwa mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kufuatia kuteuliwa kwake kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa mara ya pili na Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Novemba,  2026. Aidha, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameapishwa kuwa Kamishna  kutimiza  takwa la Sheria ya Usimamizi wa Mahakama Na. 4  Sura ya 237 inayomtaka kila Kamishna kuapishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yake. Sambamba na Mhe. Johari, Wajumbe wengine ...

Viongozi wa Tanzania na Afrika Kusini Wateta

 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe amefanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Kusini, Mhe. Thandi Moraka pembezoni mwa Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) jijini Pretoria Machi 13, 2026. Mazungumzo hayo ambayo yalihudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Fedha. Mhe. Laurent Luswetula na Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Mhe. James Bwana yalijadili namna bora ya kuimarisha uhusiano na ushiririkiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Afrika Kusini, nchi ambazo zina uhusiano wa kihistoria wa muda mrefu.  Moja ya hatua ambazo viongozi hao wamekubaliana ni kuongeza kasi ya kukamilisha rasimu za Hati za makubaliano katika maeneo mbalimbali ili ziweze kusainiwa na kutekelezwa kwa manufaa ya pande zote mbili.  Mhe. Maghembe alipongeza nchi ya Afrika Kusini kwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa nchi 20 tajiri zaidi duniani (G20) mwaka 2025 na m...

Waziri wa Ulinzi na Jkt,Ashuhudia Jwtz na Jeshi la Marekani Zikisaini Makubaliano ya Ushirikiano Kijeshi

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dk. Rhimo Nyansaho (Mb), tarehe 12 Machi,2026, katika ofisi ndogo za Wizara ya Ulinzi na JKT, Upanga, jijini  Dar es Salaam amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Kikosi cha Ulinzi cha Jimbo la Nebraska nchini Marekani (Nebraska National Guard), Meja Jenerali Craig Strong, aliyeambatana  na Kaimu Balozi wa Marekani hapa nchini, Mhe. Andrew Lentz, pamoja na maafisa jenerali kadhaa kutoka Nebraska.  Baada ya mazungumzo hayo, Waziri wa Ulinzi na JKT pamoja na Kaimu Balozi Lentz walishuhudia utiaji saini wa makubaliano ya ushirikiano kati ya JWTZ na Jeshi la Marekani uliotiwa saini na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda pamoja na Meja Jenerali Strong. Mkataba huo, pamoja na mambo mengine, unalenga kudumisha mahusiano ya muda mrefu kati ya majeshi yetu na nchi zetu kwa ujumla ambayo awali yaliasisiwa mwanzoni mwa miaka ya 1960 na viongozi wetu hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati John Fitzgerald...