Skip to main content

Posts

Showing posts from October 13, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Tanzania yashiriki Kongamano la Afya Duniani jijini Berlin

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Bw. Ismail Rumatila unashiriki Kongamano la Afya la Dunia linalofanyika kwa siku tatu jijini Berlin, Ujerumani kuanzia Oktoba 12 hadi 14, 2025. Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani. Mhe. Hassani Mwamweta anashiriki kongamano hilo linalofanyika chini ya kaulimbiu "Kuchukua Jukumu la Afya katika Ulimwengu unaogawanyika" (Taking Responsibility for Health in a Fragramenting World) limekusanya watu wa kada mbalimbali duniani wakiwemo viongozi wa Serikali, Taasisi za Kimataifa; Asasi za Kiraia; sekta binafsi; wataalam wa Afya; watafiti; wanasayansi; wanaharakati kujadili namna ya kupata ufumbuzi wa changamoto za kiafya zinazoikabili dunia. Washiriki katika siku ya ufunguzi walijadili mada mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano baina ya nchi katika sekta ya afya,; Umuhimu wa kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza kama vile kisukari, moyo, figo na kansa ambayo yamekuwa yakichangia kwa kiasi kikubwa id...

Wanawake Chunya Wachangamkia Uchimbaji, Watoa Uzoefu, Ombi Kwa Serikali, Taasisi Za Fedha

*📍Chunya* Sekta ya Madini nchini Tanzania inaendelea kuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo ya kiuchumi na kijamii na sasa inajulikana kama Sekta jumuishi inayotoa nafasi sawa kwa wote, wanaume, wanawake na vijana kushiriki kikamilifu. Wanawake Wilayani Chunya ni ushahidi wa mabadiliko haya, wakivunja dhana ya zamani kuwa madini ni kazi ya wanaume pekee. Wakizungumza na Madini Diary hivi karibuni, baadhi ya wanawake hao wameeleza jinsi wanavyoshiriki katika kila hatua ya mnyororo wa madini: wapo wanaomiliki leseni za uchimbaji mdogo, wachimbaji mahiri, wapondaji wa mawe na wafanyabiashara. Wanasema shughuli hizo zimewawezesha kupata kipato, kulea familia, kuanzisha miradi ya maendeleo na kujenga makazi bora.Ushuhuda wao unaonesha wazi kuwa sekta ya madini inayoendeshwa kwa usawa wa kijinsia inaweza kuwa chachu ya mabadiliko chanya kwa jamii na taifa kwa ujumla. Mwenyekiti wa Kikundi cha Wachimbaji Wanawake  Itumbi-Chunya Happiness Mabula anasema “Mimi kwenda chini umbali wa mita 200...

Dkt.Nchimbi:Ccm Ndio Chama Kilichojidhihirisha Kinaweza Kuhangaika na Matatizo ya Wananchi Wake

  MGOMBEA Mwenza wa Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema CCM ndiyo chama pekee kilichojidhihirisha kwa Umma, kinachoweza kuhangaika  na matatizo ya wananchi wake. Dkt. Nchimbi ameyasema hayo leo Oktoba 13, 2025 wakati akihitimisha mkutano wake wa mwisho  wa hadhara wa kampeni , uliofanyika kwenye uwanja wa Kazegunga katika Jimbo la Kigoma Kaskazini, ikiwa ni muendelezo wa kampeni zake zinazoendelea katika mikoa mbalimbali nchini. Amesema, vipo vyama vingi duniani havishughuliki na matatizo ya wananchi wake bali kwa maslahi yao binafsi na viongozi. Dkt.Nchimbi amesema, chama hicho ndicho kimeudhihirishia Umma kuwa ndiyo chama kinachoweza kuwaletea miradi ya maendeleo wananchi katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, biashara, kilimo na miundombinu ya barabara. Pia, ameeleza, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kufuata misingi ya CCM ameweza kuendeleza na kukisimamia chama na kuhakikisha kinaendelea kuwa na misingi mizuri n...

Dkt.Nchmbi:Ccm Ndio Chama Kilichojidhihirisha Kinaweza Kuhangaika na Matatizo ya Wananchi Wake

MGOMBEA Mwenza wa Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema CCM ndiyo chama pekee kilichojidhihirisha kwa Umma, kinachoweza kuhangaika  na matatizo ya wananchi wake. Dkt. Nchimbi ameyasema hayo leo Oktoba 13, 2025 wakati akihitimisha mkutano wake wa mwisho  wa hadhara wa kampeni , uliofanyika kwenye uwanja wa Kazegunga katika Jimbo la Kigoma Kaskazini, ikiwa ni muendelezo wa kampeni zake zinazoendelea katika mikoa mbalimbali nchini. Amesema, vipo vyama vingi duniani havishughuliki na matatizo ya wananchi wake bali kwa maslahi yao binafsi na viongozi. Dkt.Nchimbi amesema, chama hicho ndicho kimeudhihirishia Umma kuwa ndiyo chama kinachoweza kuwaletea miradi ya maendeleo wananchi katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, biashara, kilimo na miundombinu ya barabara. Pia, ameeleza, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kufuata misingi ya CCM ameweza kuendeleza na kukisimamia chama na kuhakikisha kinaendelea kuwa na misingi mizuri na chama...

Serikali imeweka Mikakati Dhabiti ya Kukabiliana na Majanga Nchini-Majaliwa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali imeendelea kuchukua hatua madhubuti za kuimarisha ustahimilivu wa Taifa dhidi ya majanga, kupitia utekelezaji wa sera, sheria, mikakati na miradi mbalimbali Amesema kuwa hatua hiyo itasaidia kuendelea katika kujenga ustahimilivu wa jamii dhidi ya maafa, tutaokoa maisha, mali, na rasilimali za taifa letu. Amesema hayo leo Jumatatu (Oktoba 13, 2025) wakati alipotoa tamko katika maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Kupunguza madhara ya maafa, katika ukumbi wa mikutano wa City Park Garden jijini Mbeya. Akitaja baadhi ya hatua zilizochukuliwa, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali imeandaa na kuhuisha nyaraka za kitaifa kuhusu maafa ikiwemo Sera ya Taifa ya Usimamizi wa Maafa (toleo la 2025), Mkakati wa Taifa wa Usimamizi wa Maafa (2022–2027) na Mpango wa Taifa wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa (2022). Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa hatua nyingine ni Kuimarisha usahihi wa utabiri wa hali ya hewa kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa...