Skip to main content

Posts

Showing posts from August 3, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt. Emmanuel Nchimbi Awasili Kigoma Kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Chama

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi amewasili mkoani Kigoma tayari kuanza ziara ya mikoa mitano ya Kigoma, Geita, Kagera, Mara na Mwanza  Balozi Nchimbi amewasili leo asubuhi Agosti 4, 2024 katika Uwanja wa Ndege wa Kigoma akiwa amembatana na Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Ndg. Issa Haji Usi Gavu, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Amos Makalla, Katibu wa NEC-Organaizesheni, pamoja na Katibu wa NEC - Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Rabia Abdallah Hamid.  Baada ya kutua, Katibu Mkuu Balozi Nchimbi pamoja na ujumbe wake amelakiwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali wa mkoa huo,tayari kwa  kuanza ziara ya siku 3 mkoani humo.  Malengo ya ziara hiyo ni pamoja na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020, kuhamasisha uhai wa chama, kusikiliza na kutatua kero za wananchi pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhakiki taarifa zao na kujiandikisha katika Daftari la Wakaazi kwa ajili ya maandalizi ...

Rais Mwinyi Afungua Maonesho ya Nane Nane Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali imedhamiria kuleta mageuzi ya kilimo nchini kwa kukifanya kilimo biashara chenye tija kwa kuimarisha mnyororo wa thamani kutoka shambani hadi kwa mlaji. Dkt.Mwinyi aliyasema hayo leo tarehe 3 Julai 2024 alipofungua maonesho ya saba ya kilimo ya Nane Nane Zanzibar katika viwanja vya Dole , Kizimbani Mkoa wa Mjini. Aidha Rais Dkt.Mwinyi amesema Serikali itaanzisha vituo maalum kila wilaya kuhamasisha upatikanaji wa huduma kwa wakulima na wafugaji nchini.  Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi ameleeza kuwa Serikali inatarajia kutekeleza mradi mkubwa  wa mageuzi wa uzalishaji wa wafugaji wa maziwa kwa wafugaji wadogo wadogo ambao utazingatia mabadiliko ya tabia nchi yenye gharama za  shilingi bilioni 7.5. Rais Dkt.Mwinyi ametoa wito kwa vijana kutumia fursa zilizopo katika sekta ya kilimo na mifugo kwa kujiajiri , pia amewahimiza wajifunze mbinu bora za kilimo na ufugaji kupitia maonesh...

Rais Dkt. Samia Azindua Bwawa la Umwagiliaji Katika Kiwanda Cha Sukari Cha Mtibwa

Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan azindua Bwawa la umwagiliaji lenye mita za ujazo milioni 25 pamoja na Awamu ya tatu ya upanuzi wa mashamba na umwagiliaji katika Kiwanda cha Sukari Mtibwa kwenye muendelezo wa ziara yake ya Kikazi, Mvomero Mkoani Morogoro tarehe 03 Agosti, 2024. Matukio mengine Katika Picha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali pamoja na Wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa mara baada ya kuzindua Bwawa la umwagiliaji lenye mita za ujazo milioni 25 pamoja na Awamu ya tatu ya upanuzi wa mashamba ya Kiwanda hicho, Mvomero Mkoani Morogoro.