Wadau Wavunja Ukimya, Wafafanua Ukweli wa Mradi Mkakati wa Mahenge** Na Mwandishi Wetu Dar es Salaam Mjadala kuhusu mradi wa kimkakati wa Mahenge Graphite umechukua sura mpya baada ya wachambuzi wa masuala ya uchumi na wadau wa sekta ya madini kumjibu vikali mwanaharakati wa kisiasa, Martin Maranja Masese, wakimtuhumu kusambaza taarifa zisizo sahihi kuhusu mazungumzo ya Rais Samia Suluhu Hassan na Kaimu Balozi wa Marekani, Andrew Lentz. Kwa mujibu wa uchambuzi huo, madai ya Masese yameelezwa kama “propaganda za mtandaoni zilizokosa msingi wa kisheria na kiuchumi.”  *DAI LA “MGODI KUUZWA KWA USD 300 MILIONI” LAVUNJWA VIPANDE VIPANDE* Katika chapisho lake, Masese alidai kuwa Tanzania “imewauzia Wamarekani mgodi wa graphite kwa dola milioni 300”. Lakini taarifa rasmi zinaeleza wazi kuwa: • USD milioni 300 si bei ya mgodi, bali ni makadirio ya uwekezaji (CAPEX) wa kampuni ya ubia Faru Graphite Corporation (FGC) inayomilikiwa kwa pamoja na Serikali ya Tanzania na kampuni ya Austra...
Marato tv - Sauti ya Jamii