Skip to main content

Posts

Showing posts from June 19, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Madiwani Viti Maalum Musoma Mjini Waanika Mafanikio Makubwa...

  Na Shomari Binda-Musoma  MADIWANI wa viti maalum manispaa ya Musoma wamesoma utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ( CCM) ya mwaka 2020,2025 na kuelezea mafanikio waliyoyapata. Utelezaji huo wameusoma leo juni 19,2025 kwenye baraza maalum la UWT lililofanyika kwenye ukumbi wa CCM mkoa wa Mara. Madiwani waliosoma utekelezaji wa ilani hiyo ni Naima Minga,Amina Masisa,Arieth Kumila,Asha Muhamed na Meryciana Masasi. Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa usomaji taarifa wamesema wanajivunia ushirikiano walìupata kutoka kwa viongozi na wanachama wa UWT. Wamesema moja ya mafanikio ni kuhakikisha wanaanzisha vikundi vya wanawake na kuvisajili na baadae kupata mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri. Licha ya eneo hilo madiwani hao wamezungumzia pia namna walivyoshiriki shughuli nyingine za kijamii pamoja na utekelezaji wa miradi. Aidha madiwani hao wamewaomba muda ukifika wajumbe waendelee kuwaamini na kuwachagua tena muda ukifika kutokana na namna wa...

Afrika ipewe Uhuru wa Kuzalisha Nishati Kwa Kutumia Raslimali Zake - Dkt. Biteko

📌 Ahimiza Tanzania na Urusi kuendeleza uhusiano wake wa kuheshimiana 📌 Tanzania kutumia makaa ya mawe kuzalisha umeme wastani wa  megawati 120 📌  Tanzania yapongezwa kwa mafanikio yake sekta ya nishati 📌  Ahimiza mfumo sawa wa uzalishaji nishati kati ya nchi tajiri na masikini  📌  Kampuni za Urusi zaombwa kuwekeza zaidi Afrika  Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ametoa wito kwa nchi za Afrika kupewa uhuru wa kuzalisha nishati kwa kutumia raslimali zilizopo barani humo. Dkt. Biteko ametoa wito huo Juni 19, 2025 wakati akizungumza katika Jukwaa la Kimataifa la Uchumi la St. Petersburg linalofanyika nchini Urusi. Amesema Afrika inahitaji programu itakayosaidia kufikia dhamira yake ya kuondoa idadi kubwa ya watu ambao hawatumii nishati safi huku akitaja baadhi ya athari za matumizi ya nishati isiyo safi ikiwemo uharibifu wa mazingira. Ameongeza kuwa Afrika ina vyanzo  vingi ...

Waendelezaji Miradi ya Nishati Jadidifu Watakiwa Kuchangamkia Fursa za Uwezeshwaji Kutoka REA

📌Ni kwa miradi inayozalisha chini ya Megawati 10 Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhe. Balozi Meja Jenerali Mstaafu, Jacob Kingu ametoa wito kwa waendelezaji wa miradi ya nishati jadidifu kote nchini kuchangamkia fursa za uwezeshwaji zinazotolewa na Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ili kuwa na miradi yenye tija kwa Taifa. Ametoa wito huo Juni 19, 2025 akiwa kwenye ziara ya kutembelea na kukagua mradi wa kuzalisha umeme wa Mwenga wa megawati nne unaomilikiwa na Kampuni ya Mwenga Hydro Limited kwa kutumia maporomoko ya Mto Mwenga katika Kijiji cha Ifwagi, Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa. "Kwenye eneo hili la nishati jadidifu fursa zilizopo ni nyingi, Tanzania  ni kubwa na imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi na bado hazijatumika ipasavyo; tunahitaji waendelezaji wengi wa miradi ya kuzalisha umeme kwa upepo, joto ardhi, jua na maporomoko ya maji kujitokeza ili kuwezeshwa na REA kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa umeme nchini," alisema Mhe. Balozi...

Dimba la Mkapa Mwenyeji Ufunguzi Michuano ya CHAN 2025

 Ufunguzi wa Michuano ya kandanda kwa wachezaji wa ndani barani Afrika(CHAN)Kwa mwaka 2025  utafanyika Jijini Dar-es-laam katika uwanja wa mkapa August 2. kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha mawasiliano serikalini,Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo imeeleza kuwa shirikisho la kandanda barani Afrika(CAF)Tayari imemjulisha Waziri Prof.Palamagamba Kabudi kuhusu uamuzi wa Dimba la Mkapa kuwa mwenyeji wa ufunguzi wa michuano ya CHAN.  Kufuatia uamuzi huo,Waziri Kabudi ametoa wito kwa wadau wote kuchangamkia fursa mbalimbali zinazoambatana na kufanyika kwa mashindano hayo Nchini ikiwemo biashara za bidhaa mbalimbali,huduma za usafiri,utalii na kuvutia uwekezaji. Michuano ya CHAN inatarajiwa kuanza Juni 2 hadi 28 mwaka huu hadi katika vituo vinne ambavyo ni Dar es salaam,Zanzibar,Nairobi(Kenya) pamoja na Kampala(Uganda)  Michuano ya CHAN 2025 yatafuatiwa na michuano ya AFCON 2027 ambapo mataifa ya Tanzania,Kenya na Uganda yatakuwa wenyeji. 

Watano Wahukukumiwa Kunyongwa hadi kufa

 Na Angela Sebastian ;Bukoba MAHAKAMA kuu kanda ya Bukoba imewahukumu watu watano kunyongwa hadi kufa baada ya kukutwa na hatia ya mauji ya kukusudia Wilayani Ngara mkoani Kagera kwa  nyakati tofauti. Wakili wa Serikali Grolia Lugeye akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za mashtaka mjini Bukoba amesema katika tukio la kwanza lilitokea Novemba mosi,2018  majira kati ya saa sita hadi saba usiku kitongoji cha Kukazulu kijiji Mulugalama Wilayani Ngara  ambapo washitakiwa Julius Ngeze (55),Jackson Bwelele (47) na Seleman Lwandindi waliwaua watu wawili mme na mke. “Siku ya tukio majira ya usiku washitakiwa hao walienda nyumbani kwa Amosi Mfumu (80) ambaye ni marehemu na kuvunja mlango na baada ya kuingia ndani walikutana na mgeni ambaye alilala sebureni aliyejulikana kwa jina la Mibulo Benedicto na kumuweka chini ya ulinzi ,wakati huo marehemu Amosi baada ya kusikia purukushani alitoka chumbani ndipo akakutana na wauaji hao na kumkata mapanga sehemu ...

Watano Wahukukiwa Kunyongwa Hadi Kufa

 Na Angela Sebastian ;Bukoba MAHAKAMA kuu kanda ya Bukoba imewahukumu watu watano kunyongwa hadi kufa baada ya kukutwa na hatia ya mauji ya kukusudia Wilayani Ngara mkoani Kagera kwa  nyakati tofauti. Wakili wa Serikali Grolia Lugeye akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za mashtaka mjini Bukoba amesema katika tukio la kwanza lilitokea Novemba mosi,2018  majira kati ya saa sita hadi saba usiku kitongoji cha Kukazulu kijiji Mulugalama Wilayani Ngara  ambapo washitakiwa Julius Ngeze (55),Jackson Bwelele (47) na Seleman Lwandindi waliwaua watu wawili mme na mke. “Siku ya tukio majira ya usiku washitakiwa hao walienda nyumbani kwa Amosi Mfumu (80) ambaye ni marehemu na kuvunja mlango na baada ya kuingia ndani walikutana na mgeni ambaye alilala sebureni aliyejulikana kwa jina la Mibulo Benedicto na kumuweka chini ya ulinzi ,wakati huo marehemu Amosi baada ya kusikia purukushani alitoka chumbani ndipo akakutana na wauaji hao na kumkata mapanga sehemu ...

Madiwani Viti Maalum Musoma Mjini Wasoma Utekelezaji wa Ilani na Mafanikio Waliyoyapata

Na Shomari Binda-Musoma  MADIWANI wa viti maalum manispaa ya Musoma wamesoma utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ( CCM) ya mwaka 2020,2025 na kuelezea mafanikio waliyoyapata. Utelezaji huo wameusoma leo juni 19,2025 kwenye baraza maalum la UWT lililofanyika kwenye ukumbi wa CCM mkoa wa Mara. Madiwani waliosoma utekelezaji wa ilani hiyo ni Naima Minga,Amina Masisa,Arieth Kumila,Asha Muhamed na Meryciana Masasi. Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa usomaji taarifa wamesema wanajivunia ushirikiano walìupata kutoka kwa viongozi na wanachama wa UWT. Wamesema moja ya mafanikio ni kuhakikisha wanaanzisha vikundi vya wanawake na kuvisajili na baadae kupata mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri. Licha ya eneo hilo madiwani hao wamezungumzia pia namna walivyoshiriki shughuli nyingine za kijamii pamoja na utekelezaji wa miradi. Aidha madiwani hao wamewaomba muda ukifika wajumbe waendelee kuwaamini na kuwachagua tena muda ukifika kutokana na namna walivyofa...

Rais Dkt. Samia Amedhamiria Kuiendeleza Sekta ya Madini-Majaliwa

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa uzinduzi wa kiwanda cha kwanza cha kisasa cha kuchenjua shaba ni ishara ya dhamira ya dhati ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuisimamia na kuendeleza sekta ya madini. Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa kiwanda hicho chenye uwezo wa kuchenjua tani 31,200 za mashapo ya shaba kwa mwezi kitaleta manufaa kwa Wana-chunya na Taifa kwa ujumla. Amesema hayo jana (Jumatano Juni 18, 2025) alipomuwakilisha Rais Dkt. Samia katika uzinduzi wa kiwanda cha Mineral Access Systems Tanzania Ltd (MAST), kilichopo katika kata ya Mbugani, Chunya mkoani Mbeya. “Uthubutu na ubunifu wa Rais wetu Dkt. Samia ndio uliochagiza kwa kiasi kikubwa maendeleo katika Sekta ya Madini, wawekezaji hawa wamekuja kwasababu ya mazingira mazuri ya uwekezaji”. Aidha, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa Wizara ya Madini na Taasisi mbalimbali nchini ziendelee kusimamia wawekezaji ili wanapofanya shughuli zao wazingatie Sheria, Kanuni na Taratibu za nchi ikiwemo kulipa kodi stahiki, kutun...