📍 Igunga, Tabora Tume ya Madini Mkoa wa Tabora imeshiriki rasmi katika hafla ya uzinduzi wa miradi ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) iliyofanyika Wilaya ya Igunga, Mkoa wa Tabora. Hafla hiyo ilifunguliwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Mhe. Sauda S. Mtondoo, na kuhudhuriwa na viongozi wa Serikali, wadau wa sekta ya madini pamoja na wananchi wa maeneo husika. Miradi iliyozinduliwa inajumuisha ujenzi wa darasa moja na ofisi ya walimu katika Shule ya Msingi Mkwabi, pamoja na ujenzi wa vizimba vya maji katika Kijiji cha Nanga. Utekelezaji wa miradi hiyo unalenga kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji shuleni, sambamba na kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi, hivyo kuchangia kuboresha ustawi wa jamii. Miradi hiyo imetekelezwa na Kampuni ya TAUR TANZANIA LTD kwa gharama ya Shilingi milioni 50 katika mwaka wa fedha 2024/2025, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) kwa mujibu wa sheria na miongozo ya sekta ya madini nc...
Marato tv - Sauti ya Jamii