Skip to main content

Posts

Showing posts from October 3, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Mwinyi:Zanzibar inaendelea na mageuzi kuvutia wawekezaji

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema, Zanzibar inaendelea kuleta mageuzi makubwa ya miundombinu kwa lengo la kuwavutia wawekezaji. Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo  leo tarehe 4 Oktoba 2024, Ikulu Zanzibar alipokutana na Rais wa Kampuni ya Samsung C& T  Corporation Oh Se-Chul kutoka Korea Kusini na ujumbe wake. Aidha Rais Dk. Mwinyi amewahakikishia Wawekezaji hao kuwa Zanzibar ina fursa nyingi na kuwakaribisha Zanzibar kuwekeza. Halikadhalika Dk.Mwinyi ameuelezea ujumbe huo maeneo ya vipaumbele katika uwekezaji hivi sasa kwa Zanzibar ni Utalii, Uchumi wa Buluu, Uvuvi, Usafirishaji na Mafuta na gesi. Rais Dk. Mwinyi ameipongeza kampuni ya Samsung C&T kwa wazo la kushirikiana na nchi za Afrika hasa za Kusini mwa jangwa la Sahara katika nyanja mbalimbali za uwekezaji pamoja na kuanzisha ofisi yao Tanzania.  Naye, Rais wa Kampuni hiyo Bw. Oh Se-Chul amemuelezea Rais Dk. Mwinyi kwamba Kampuni hiyo katika kutanua wigo ...

EMEDO na TMA waja mfumo mpya wa utoaji taarifa ya hali ya hewa kwa wavuvi

Shirika la Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo (EMEDO) na Mamlaka ya Utabiri wa hali ya hewa Mwanza wametambulisha mfumo mpya wa utoaji wa taarifa ya hali ya hewa kwa jamii ya wavuvi walioko katika kisiwa cha Goziba mkoani Mwanza. Uzinduzi huo ulifanyika tarehe 01/10/2024 katika kisiwa cha Goziba na kuhudhuliwa na Wavuvi,Wamiliki wa Mitumbwi,Wafanyabiashara wa Samaki na Vingozi wa Serikali. Utafiti uliofanywa na Shirika la EMEDO mwaka 2021 ulibaini sababu mbalimbali zinazopelekea Wavuvi kuzama maji na wengine kupoteza maisha na sababu moja wapo ilibainika kuwa ni changamoto ya upatikanaji wa taarifa za utabiri wa hali ya hewa kwa wakati na uelewa kuhusu taarifa zenyewe na ili kutatua changamoto hiyo EMEDO na TMA wamefanikiwa kuja na mabango yatakayotoa taarifa za hali ya hewa kwa jamii ya wavuvi kwa njia rahisi na kwa kuanza wameanza na kisiwa cha Goziba. Akizungumza katika uzinduzi rasimi wa mabango hayo Meneja wa Mamlaka ya hali ya hewa kanda ya ziwa Augustino Nduganda amesema nimuhi...

Rc Mtambi atuma salam za shukrani kwa Rais Dkt.Samia kwa kupokea fedha nyingi za miradi mara

Na Shomari Binda-Butiama Mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi amemuomba Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Simbachawene kufikisha salam kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha nyingi kwaajili ya miradi. Shukrani hizo amezitoa leo oktoba 3 kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa shule ya msingi Nyamisisi baada ya kuzindua shule mpya ya msingi Chief Manyori. Amesema mkoa wa Mara chini ya uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan umepokea kiasi cha tilioni 1 na zaidi ya bilioni 200 ambazo zinatekeleza miradi mbalimbali. Kanali Mtambi amesema 280 ikiwa ya shule,maji,afya,miundombinu na mingine ipo iliyokamilishwa na mingine inaendelea kutekelezwa. " Kwa niaba ya wananchi wa mkoa wa Mara tunaomba utufikishie salam kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwa ni mema sliyowanyia wananchi wa mkoa wa Mara. " Miradi inaendelea vizuri na inasimamiwa vizuri na sio shule hii pekee ambayo umeizindua zipo shule mpya zaidi ya 10...

Wanaccm wekeni makundi pembeni"Mnec Hamoud Jumaa

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa anayetokana na Jumuiya ya Wazazi Ndugu.Hamoud Jumaa (MNEC)amewataka viongozi wa CCM kuvunja makundi na badala yake amewasihi kuimarisha umoja na mshikamano katika kukitumikia chama kwa ajili ya ushindi wa CCM katika chaguzi zijazo.  Ameyasema hayo MNEC Hamoud*akiwa  katika Shina namba 13 Tawi la Inyanga Kata ya Mungula Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga, leo "Tunapita kujenga umoja na mshikamano wa wanachama na viongozi kwa kufika katika ngazi za matawi na shina ili kukagua na kuimarisha uhai wa chama kuanzia ngazi ya mabalozi ambao ndiyo msingi mkubwa wa chama cha mapinduzi" alisema MNEC Hamoud Miongoni mwa mambo yanayopewa kipaumbele katika ziara hiyo ni suala la uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji ambao unatarajia kufanyika mwezi ujao ambapo ametumia mikutano hiyo kuhamasisha wananchi na wanachama kujitokeza katika maboresho ya daftari la mkazi ili kuwa na haki ya kushiriki katika uchaguzi ujao, A...

Waziri mkuu asema lishe bora ni kipaumbele cha Rais Samia

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa suala ya lishe ni kipaumbele muhimu kwa Serikali katika kuwezesha utekelezaji wa mipango ya maendeleo na shughuli za kiuchumi kwa jamii jamii zikiwemo za kilimo, uvuvi, ufugaji na biashara. Amesema hayo leo (Alhamisi, Oktoba 03, 2024) wakati alipofunga Mkutano Mkuu wa Kumi wa Wadau wa Lishe kwenye ukumbi wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza.   Amesema kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kutokomeza aina zote za utapiamlo nchini. “Mheshimiwa Rais Dkt. Samia amedhihirisha dhamira yake ya dhati ya kulipa umuhimu wa kipekee suala la lishe. Hatua ambayo imemfanya awe kinara na mmoja wa viongozi wanaotambuliwa na kutolewa mfano ulimwenguni kwa hatua ambazo wameweza kupiga katika mapambano dhidi ya changamoto za utapiamlo” Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa wadau wote wa lishe wahakikishe wanatumia vizuri matokea ya ripoti ya mapitio ya muda wa kati ili kujita...

Wizara ya madini na taasisi zake yaendelea kutoa elimu kwa wadau wa madini

Wizara ya Madini na Taasisi zake leo Oktoba 03, 2024 imeendelea kutoa elimu kwa wadau wa madini katika Maonesho ya Saba ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Bombambili mjini Geita. Kwa upande wa Tume ya Madini elimu imeendelea kutolewa katika maeneo ya usimamizi/udhibiti wa Sekta ya Madini na ukusanyaji wa mapato ya Serikali yatokanayo na tozo mbalimbali zinazotokana na shughuli za madini, utoaji na usimamizi wa leseni za utafutaji wa madini, uchimbaji na biashara ya madini pamoja na namna ya kujisajili katika mfumo wa Online Mining Cadastre Transaction Portal (OMCTP), ukaguzi na usalama wa migodi, afya, mazingira na njia bora ya uzalishaji wa madini kwa migodi midogo, ya kati na mikubwa. Maeneo mengine ni pamoja na usimamizi wa biashara ya madini inayofanyika katika masoko ya madini yaliyoanzishwa nchini, ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta ya Madini na wajibu wa wawekezaji kwa jamii katika uboreshaji wa huduma (Corporate Social Resp...

Waziri chana akutana na machifu na wazee wa kimila wa eneo la lyamba lyamfipa

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Machifu kutoka Misitu ya Miteremko ya Safu za Milima ya Lyamba Lyamfipa kwa lengo la kujadiliana namna ya kuwa na uhifadhi endelevu wa eneo hilo la misitu. Kikao hicho kimefanyika Manispaa ya Sumbawanga, Mkoani Rukwa ambapo pamoja na mambo mengine amewapongeza machifu hao kwa juhudi zao za kuhifadhi eneo hilo muhimu kwa Taifa katika utunzaji wa mazingira. Hifadhi ya Misitu ya Miteremko ya Safu za Milima ya Lyamba Lyamfipa ina vyanzo vingi vya maji ambayo yanatumiwa na wananchi kwa matumizi ya nyumbani na kwenye kilimo cha umwagiliaji na pia ndio chanzo cha mvua kwa eneo la Sumbawanga.