Skip to main content

Posts

Showing posts from January 30, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Samia Awasili Nchini Zimbabwe

 Matukio mbalimbali ya kuwasili kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Robert Mugabe, Harare nchini Zimbabwe kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika leo tarehe 31 Januari, 2025.

Tls Mkoa wa Mara Wataka Mahakama Kupewa Uwezo wa Kutoa Amri ya Kukamata Mali za Serikali

Na Ada Ouko, Musoma. CHAMA cha wanasheria wa kujitegemea(TLS) Mkoani Mara kimeiomba Serikali, kufanya Marekebisho ya Sheria inayotoa Hukumu dhidi ya Serikali ili kutengeneza usawa wa haki. Ombi hilo limetolewa na Wakili wa kujitegemea wa Chama hicho wilayani hapa Daud Mahemba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yaliyozinduliwa na Mkuu wa Mkoa huo Evans Mtambi January 25 Mwaka huu. "Ikitokea Mwananchi ameshinda kesi dhidi ya Serikali Mahakama haina mamlaka ya kisheria ya kutoa amri ya kukamata mali ya serikali moja kwa moja kupitia dalali wa Mahakama"alisema. Mahemba alisema utaratibu uliopo ni kuiandikia serikali kupitia hazina ilipe deni ambapo Afisa Masuhuli wa serikali haitekelezi hukumu hiyo kwa madai ya kuwa serikali haina fedha na kwamba mwananchi aliyeshinda kesi hutembea na hukumu isiyotekelezeka kwa muda mrefu. Alisema mdai akimpeleka mahakamani afisa masuhuli kwa lengo la kufikishwa gerezani kwa kosa la kushindwa kutekel...

Balozi Dkt Nchimbi Apokelewa Kwa Heshima Ethiopia

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akipokelewa na Mhe. Dkt. Girma Amente, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Prosperity Party (PP), chama tawala cha Ethiopia na pia Waziri wa Kilimo wa Serikali ya nchi hiyo, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole.  Balozi Nchimbi amewasili nchini Ethiopia kwa ajili ya ziara ya kikazi, kufuatia mwaliko wa PP.

KIKUNDI cha wazaliwa tarafa ya Kiagata wachangia vifaa vya ufundishaji sekondari ya Kiagata

Na Shomari Binda-Butiama KIKUNDI cha wananchi wakazi wa Tarafa ya Kiagata wilayani Butiama wamechangia vifaa vya ufundishaji ikiwemo mashine ya kudurufu karatasi yenye thamani ya shilingi milioni tatu na laki tano kwenye sekondari kongwe ya Kiagata katika tarafa hiyo. Wakazi hao wamechangia vifaa hivyo kupitia michango ya wanakikundi cha WhatsApp cha Kiagata Zone huku wito ukitolewa kwa jamii kurudi nyumbani na kuchangia masuala ya maendeleo. Akizungumza mara  baada ya kukabidhi vifaa hivyo Mwenyekiti wa kikundi hicho Robert Silyvester Maganya amesema jamii haipaswi kuiachia serikali katika kuchangia mambo ya jamii yakiwemo ya maendeleo katika vijiji walivyozaliwa,kupata elimu na kuwafanya watambukike nje ya maeneo ya vijiji hivyo. Amesema kama sehemu ya jamii na wazawa wa tarafa ya Kiagata wameamua kurudi nyumbani na kuchangia sekta ya elimu  na miradi mingine katika jamii ya tarafa hiyo. Amesema baada ya kusikia changamoto ya kudurufu karatasi kwenye shule hiyo walijichangis...

Wasira-hatuko Tayari Chadema Waje na azimio Ya Kuvunja Sheria za Nchi

  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama wa Chamapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amesema Chama na serikali yake haitakubaliana na azimio lolote litakalotolewa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya kukutana kwa faragha kama walivyotangaza viongozi wa chama hicho, juzi. Amesema amesikia chama hicho kikitangaza kwamba kinakwenda kujifungia kisha kije na jambo ambalo halijapata kushuhudiwa nchini, hivyo ametoa angalizo jambo hilo ni lazima lifuate sharia za nchi. Wasira amesema hayo leo alipohutubia wananchi katika mkutano uliotumika kuzindua sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya kuzaliwa kwa Chama kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Stendi ya Zamani mjini Bunda. “Wamesema wanajifungia halafu waje wafanye jambo ambalo halijapata kuonekana, nikasema ni jambo gani, mimi nikaona huko kujifungia ile ni honeymoon maana honeymoon simnaijua, watu wakishaoana wanajifungia mahali…ile ni honemoon. “Tunawaambia tunawatakia heri kwenye honeymoon lakini tu...