Skip to main content

Posts

Showing posts from November 27, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Naibu Waziri Sangu Apiga Kura, Awaomba Wananchi Kwela Kuendelea Kuwa Watulivu

  Na Mwandishi Wetu-Rukwa WANANCHI wa Jimbo la Kwela wametakiwa kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuchagua viongozi Bora watakao waongoza kwa amani,usala na utulivu. Pia amesisitiza kuwa uchaguzi huo ni fursa kwa wananchi kupata viongozi wa karibu wanaojua changamoto zinazowakabili za moja kwa moja katika maeneo yao. Naibu Waziri, Menejimenti ya Utumishi wa Umma ma Utawala Bora Mhe.Deus Sangu ambaye pia ni Mbunge wa Kwela ametoa kauli hiyo  mapema leo Jumatano Novemba 27, 2024 mara  baada ya kumaliza kupiga kura katika Kitongoji cha Pokopoko Kata ya Laela Mkoani Rukwa  "Niwazi nimeridhika na idadi ya wapiga kura waliojitokeza katika kitongoji hichi na jinsi mchakato wa uchaguzi unavyoendelea, ," Amesema Na kuongeza"Niwaombe Wananchi waliobaki kutimiza haki yao ya kikatiba kwa kujitokeza kupiga kura,"Amesema  Hata hivyo amesisitiza kuwa,ushiriki wa kila raia ni muhimu katika kuhakikisha mchakato wa uchaguzi unafanikiwa kwa haki na uwazi...

Rc Mtambi Awataka Wananchi Mkoa wa Mara Kuendelea Kudumisha Demokrasia

 Ghati Msamba- Musoma MKUU wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, amewataka wananchi wa mkoa huo kuendelea kudumisha demokrasia kama walivyofanya katika zoezi la uandikishaji, na kuhakikisha wanakamilisha zoezi la upigaji kura kwa uangalifu na kwa kufuata sheria. Akizungumza baada ya kupiga kura katika Kituo cha Ofisi ya Kata ya Mukendo, Mtambi alisisitiza umuhimu wa kuepuka vitendo vya kupiga kura mara mbili na kufanya kampeni katika vituo vya kupigia kura. Alisema wananchi wanapaswa kuhakikisha wanarudi nyumbani mara baada ya kupiga kura, na kuepuka kurudi tena kwenye vituo vya kupigia kura, kwani hilo ni kinyume cha sheria. "Kwa sasa tayari mimi nimepiga kura, naomba wananchi wote mliojiandikisha mkaendelee na zoezi hili ili tuweze kupata viongozi wa serikali za mitaa watakaoshirikiana nasi katika kuleta maendeleo," alisema Mtambi. Mkuu huyo wa Mkoa pia aliwapongeza wananchi wa Mara kwa kujitokeza kwa wingi na kudumisha demokrasia, akisisitiza kuwa haki ya kila mmoja ni kum...

Mhe.Mathayo apiga kura Kituo cha Kupigia Kura Sido

Mbunge wa Jimbo la Musoma mjini Mhe Vedastus Mathayo Leo 27/11/2024 amepiga yake katika kituo cha kupigia kura Sido kilichopo mtaa wa Baruti, kata ya Nyakato.  Mhe Mathayo ameongozana na mwenza wake Bi Elizabeth Vedastus Mathayo.  Akizungumzia zoezi zima la upigaji kura, Mhe Mathayo amesema ametembelea baadhi ya maeneo, zoezi hilo linaenda vizuri

Mama Mary Majaliwa akiwa kwenye Foleni ya Kupiga Kura

Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa akiweka Kura yake katika sanduku kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa,Vijiji na Vitongoji kwenye kituo cha Shule ya Msingi Nandagala, Ruangwa Mkoani Lindi,  Novemba 27, 2024.

Balozi Nchimbi akipiga kura Dodoma

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amepiga kura yake katika Kituo cha Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Kilimani, kwa ajili ya kuchagua viongozi wa Serikali ya mtaa anaoishi, eneo la Kilimani, jijini Dodoma, leo tarehe 27 Novemba, 2024.

Dc Misungwi ahimiza amani na Utulivu Wakati na baada ya Uchaguzi

Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza Mhe.Johari Samizi amewongoza wakazi wa Wilaya hiyo katika uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Vijiji na Vitongoji. Mhe, Samizi amepiga kura katika Kituo cha kupigia kura kilichopo ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Misungwi Kitongoji cha Misungwi D Kijiji cha Misungwi na kuwahimiza Wananchi kujitokeza kupiga kura mapema na kutimiza haki ya Msingi na ya kikatiba ya kuwachagua Viongozi. Amewasihi kuendelea na utulivu na Amani wakati wote wa zoezi la upigaji kura na kusubiri matokeo yatakapotangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Misungwi.  Bi. Semeni Juma na Chausiku Mujima wakazi wa Kijiji cha  Misungwi ni miongoni mwa Wananchi waliopiga kura mapema Leo katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi pamoja na mvua kunyesha wamefurahi kutumia haki ya kikatiba ya kuwachagua Viongozi wa Kijiji na Kitongoji na kuhakikisha wametumia Fursa ya kuchagua Viongozi Bora na wabunifu na wanaowataka. Kwa upande wao,Watu wenye ulemavu wilaya ya Misungw...

MBUNGE WA VITI MAALUM MHE. SALOME MAKAMBA APIGA KURA KITUO CHA BUGWETO A JIMBO LA SHINYANGA MJINI KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Salome Makamba, leo amepiga kura katika kituo cha Bugweto A, kilichopo Kata ya Ibadakuli, Jimbo la Shinyanga Mjini, kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa. Mhe. Makamba ameungana na wananchi wengine ikiwemo familia yake kushiriki katika zoezi hilo muhimu ambalo linaendelea kote nchini kwa lengo la kuchagua viongozi watakaowakilisha jamii kwenye ngazi za msingi Uchaguzi wa serikali za mitaa ni miongoni mwa hatua muhimu za kidemokrasia, zinazotoa fursa kwa wananchi kushiriki moja kwa moja katika maamuzi ya maendeleo ya maeneo yao. Kwa sasa, zoezi la upigaji kura linaendelea katika vituo mbalimbali, huku usimamizi wa uchaguzi ukifanyika kwa kuzingatia kanuni na taratibu zilizowekwa na mamlaka husika

Mjumbe wa Baraza Kuu la UWT Taifa Mkoa wa Mara Rhobi Samwelly Amepiga Kula Leo November 27,2024

  MJUMBE wa Baraza Kuu la UWT Taifa Mkoa wa Mara  Ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa huo Rhobi Samwelly ametumia haki yake ya kikatiba ya kupiga   kura Leo Novemba 27, 2024 kuchagua Viongozi wa serikali ya mtaa.