Na Ada Ouko, GMTV, Musoma. JAMII imetakiwa kuacha kununua dawa za binadamu na kuzitumia kiholela bila kuzingatia matumizi sahihi ya dawa hizo kutoka kwa wataalamu, kwa kuwa hali hiyo inapelekea usugu wa vimelea vya magonjwa. Mwito huo umetolewa Julai 11, 2025 na Mfamasia mkuu wa Mkoa wa Mara Apolinary Mwakabala wakati akihitimisha mafunzo ya siku mbili kwa watoa huduma za dawa kwenye maduka ya dawa muhimu (ADO) ikiwa lengo ni kupunguza usugu wa vimelea kwenye dawa aina za Antibiotic, na dawa za kuzuia maumivu kwa mtumiaji. "Acheni kuuza dawa kiholela mgonjwa akifika dukani kwako kupata dawa kama anaumwa mnapaswa kumshauri kwenda kupima zahanati au Hospitali kwanza... Ili kubaini ugonjwa unaomsumbua ndipo utaweza kumpa dozi kamili ya dawa kama alivyoandikiwa na daktari, badala ya kumpa dozi nusu jambo ambalo ni hatari kwa afya yake"Anasema Apolinary. Aidha amewataka kuzingatia sheria kanuni, taratibu za uendeshaji wa huduma za maduka ya dawa muhimu (DLDM) sambamba na hilo k...
Marato tv - Sauti ya Jamii