Skip to main content

Posts

Showing posts from November 15, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mhandisi Seff Aeleza Jitihada za Tarura Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi

Belem, Brazil Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor Seff amesema Serikali ya Tanzania imefanya jitihada kubwa ambayo imeweza kukamilisha miundombinu iliyoathiriwa na mabadiliko ya tabianchi katika maeneo mengi. Mhandisi Seff ameeleza hayo wakati akiwasilisha mada kwenye Mkutano wa Mkutano wa 30 wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP 30) unaoendelea katika Jiji la  Belem nchini Brazil. Aidha, katika wasilisho lake Mtendaji Mkuu huyo aliweza kuonesha Makala fupi ya namna Wakala huo ulivyofanikiwa kurudisha mawasiliano ya miundombinu ya barabara iliyoharibika kwa kujenga miundombinu himilivu ‘resilient’ kwa athari za mabadiliko ya tabianchi na zenye uwezo wa kupitika mwaka mzima. Amesema kupitia programu ya uondoaji vikwazo katika barabara (bottleneck), wameweza kujenga madaraja na barabara na hivyo kufungua mawasiliano katika vijiji na hivyo kuweza kuwasaidia wananchi kusafirisha mazao yao pia kuwarahisishia kupata huduma...

Rais Dkt. Samia: Watanzania Tuendelee Kuliombea Taifa Lidumu Katika Amani

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan anaendelea kuwasisitiza Watanzania waendelee kuliombea Taifa ili amani, upendo, ustahimilivu na mshikamano viendelee kudumu nchini. Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo (Jumapili, Novemba 16, 2025) alipowasilisha salamu za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa waumini na viongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kisasa, Mkoa wa Dodoma. “Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anawasalimu sana. Yuko pamoja nanyi, na rai yake kwa Watanzania wote ni kuendeleza maombi kwa Taifa letu kuwa watulivu na kuiombea amani iendelee kudumu.” Aidha, Waziri Mkuu amesema kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kuhakikisha amani ya nchi inaendelea kulindwa na kuenziwa, kwa sababu pasipo amani, Taifa halitoweza kutekeleza majukumu yake ikiwemo kuendesha ibada na shughuli nyingine za kijamii. “Pasipo amani hatuwezi kutekeleza majukumu mengine yoyote, pasipo amani hatuwezi ku...

Mbunge Mavunde Anuia Kuipaisha Mtumba Kwa Elimu Kidijitali

▪️Agawa Photocopier Machines kubwa kwa kata 20 ▪️Alenga kuwapunguzia michango ya mitihani wazazi wa Mtumba ▪️Maafisa Elimu Kata,Walimu wakuu na Wakuu wa Sekondari wote wapewa Kompyuta Mpakato(𝙇𝙖𝙥𝙩𝙤𝙥𝙨) 110 ▪️Aahidi kuanzisha SACCOS ya Walimu Mtumba na kuchangia 20m ▪️Wadau wa Elimu wampongeza Rais Samia kwa miundombinu bora ya Shule Dodoma Jiji *Mtumba,Dodoma* Mbunge wa Jimbo la Mtumba Mh. Anthony Mavunde leo ametimiza ahadi yake ya kugawa Photocopier Machines 20 kwa kila kata,Kompyuta Mpakato(𝙇𝙖𝙥𝙩𝙤𝙥𝙨) 110 kwa Maafisa Elimu Kata,Walimu wakuu na Wakuu wa Shule zote za Msingi na Sekondari za Jimbo la Mtumba. Mh. Mavunde amesema dhamira kuu ya zoezi hilo ni kuboresha sekta ya elimu Jimbo la Mtumba kidijitali kwa kurahisisha ufundishaji na pia kupunguza adha ya michango ya mitihani kwa wazazi. Na pia ametumia fursa hiyo kuwataka walimu wote wa Jimbo la Mtumba kuunda umoja wao na kutengeneza SACCOS ambayo ameahidi kuchangia kiasi cha *Tsh 20,000,000* kutunisha mfuko wa walimu w...

Hospitali ya Shifaa yazindua kitengo maalum cha kutibu maradhi ya kisukari

Na Mwandishi Wetu HOSPITALI ya Shifaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam imezindua kitengo  maalum kwa ajili ya matibabu ya wenye maradhi ya kisukari. Uzinduzi wa huduma hizo umefanyika leo jijini Dar es Salaam katika hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na wa taasisi binafsi. Mkurugenzi wa Tiba wa hospitali hiyo, Dk Emmanuel Maganga alisema jana kuwa kitengo hicho chenye wataalamu bobezi wa maradhi hayo kitasaidia kupunguza tatizo la ugonjwa huo ambao unaonekana kuendelea kukua kwa kasi nchini. Alisema ongezeko la wagonjwa wa kisukari nchini ndio uliosababisha uongozi wa hospitali hiyo kuona umuhimu wa kuanzisha kitengo hicho kama njia ya kupunguza tatizo hilo. “Miongoni mwa magonjwa yanayosumbua sana kwa sasa hapa nchini ni kisukari ukiangalia miaka ya nyuma utafiti ulionyesha kuwa Dar es Salaam ilikuwa na wagonjwa wasiozidi 600,000 wa kisukari lakini kwa utafiti wa mwaka jana ulionyesha kuwa wagonjwa wa kisukari wamefikia 3,000,000,” alisema “Kwa hiyo unaona ka...

Dkt. Nchimbi Ashiriki Mkutano wa Icglr, Kinshasa

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Emmanuel John Nchimbi ameshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) ukiwa ni mkutano wake wa kwanza kushiriki nje ya mipaka ya Tanzania kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,tangu alipoapishwa kushika wadhifa huo Novemba 03, 2025. Mkutano huo uliofanyika Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Novemba 15, 2025 umefunguliwa na Rais wa DRC, Mhe. Felix Tshisekedi ambaye alipokea uenyekiti wa Jumuiya hiyo kutoka kwa Rais wa Angola, Mhe. João Lourenço. Katika hotuba yake ya ufunguzi Rais Tshisekedi alimpongeza Rais Samia kwa ushindi na kuendesha uchaguzi ulio huru, haki na wazi uliofanyika Oktoba 29, 2025. Aidha, Rais Tshisekedi pamoja na viongozi wengine waliopata fursa ya kuhutubia mkutano huo wakiwemo Katibu Mtendaji wa ICGLR, Balozi João Samuel CAHOLO, Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Afrika, Mhe. Mahamoud Ali Youssouf na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mh...