Skip to main content

Posts

Showing posts from July 15, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mwenyekiti wa Bawacha Mkoa wa Mara Awahamasisha Wanawake Kugombea Nafasi Za Uongozi

Na Helena Magabe-Tarime Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Mara(BAWACHA) Mhe.Veronica Irecho ametoa Wito Kwa wanawake Mkoani Mara kujitojeza Kwa wingi kujiandisha Kupiga Kura pamoja na Kugombea Nafasi Mbalimbali za Uongozi na hivyo Kushiriki kikamilifu Katika shughuli za maendeleo. Akizungumza katika kikao cha 7 tangu aanze ziara ya  kuhamasisha uhai wa Bawacha Majimboni kilichofanyika katika ofisi ya chadema Tarime mjini Amesema lengo ni kuhamasisha wanawake kujiandikisha kupiga kura,kugombea nafasi mbali mbali sambamba na kukemea vitendo vya rushwa ndani ya Chama hicho  Ikiwa ni mara ya kwanza kukutana na Wajumbe wa Bawacha wa Tarime amekemea vikali vitendo vya rushwa  ambapo amewataka  wanawake kuepuka  ushiriki Vitendo vya rushwa kwani ni mbaya na itapelekea kukosa nafasi mbali mbali kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 pamoja na Serikali kuu 2025. Irecho ambaye ni Diwani Mstaafu wa viti maalumu pia am...

Miradi Mipya 409 ya Uwekezaji Kutoa Ajira 121,209

Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Pascal Maganga amesema, kuanzia Januari hadi Juni 2024 miradi 409 yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 3.09 tayari imesajiliwa katika kituo hicho na kwamba inatarajiwa kutoa ajira 121,209 pindi itakapokamilika.  Maganga amesema hayo wakati TIC ilipotembelea kiwanda cha maziwa cha Kahama Fresh kilichopo Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuhamasisha uwekezaji wa ndani. "Kwa mwaka 2023, miradi 526 ya uwekezaji ilisajiliwa TIC yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 5.72  ikitarajiwa kutoa ajira 137,010," amesema Maganga Katika jitihada za kuhamasisha uwekezaji wa ndani, TIC inatembelea miradi mbalimbali na kutoa elimu kwenye mikoa ya Kagera, Mwanza, Mara, Simiyu, Lindi, Ruvuma, Rukwa, Kigoma na Katavi, na inashirikiana na Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) kwa upande wa Unguja na Pemba. Chanzo: TIC

Waziri Nape Azitaka Vodacom na Ttcl Kukamilisha Ujenzi wa Minara Mitano Kigoma

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) amezitaka Kampuni za Simu zilizopewa miradi ya ujenzi wa Minara 8 ya Mawasiliano ya Simu katika Mkoa wa Kigoma kuhakikisha inakamilika mapema mwaka huu. Waziri Nape amesema kukamilika mapema kwa ujenzi wa minara hiyo kutawezesha wananchi zaidi ya 108,126 wanaopata changamoto ya Mawasiliano kwa sasa katika Kata Nane za Mkoa wa Kigoma kupata huduma hiyo. Amesema hayo tarehe 15 Julai, 2024 wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Kigoma, Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo na watoa huduma za Mawasiliano, mara baada ya kupokea taarifa ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na Mamlaka ya Mawasiliano Tannzania (TCRA) kuhusu hali ya upatikanaji wa Huduma za Mawasiliano na mradi wa ujenzi wa Minara katika mkoa huo. "Vodacom mna minara 4 ambayo bado hamjaanza kujenga, tukubaliane hadi kufikia Oktoba, 2024 iwe imekamilika, nimeshaongea na Mtendaji Mkuu sitaki ifike Oktoba, 2024 tuanze ku...

Waziri Mkuu Aishukuru Serikali ya Denmark Aagana na Balozi Wake

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameishukuru Serikali ya Denmark kwa misaada ambayo imekuwa ikiitoa kwenye miradi ya maendeleo nchini ambapo Krona milioni 1.95 (sh. bilioni 645.86) zilizotolewa katika kipindi cha miaka mitano. Ametoa shukrani hizo leo (Jumatatu, Julai 15, 2024) wakati akizungumza na Balozi wa Denmark anayemaliza muda wake nchini, Bi. Mette N. Dissing-Spandet kwenye ofisi ndogo ya Magogoni, jijini Dar es Salaam. Waziri Mkuu amesema Serikali hiyo ilisaidia sana kwenye miradi mbalimbali hasa katika sekta za afya, masuala ya kikodi, shughuli za utafiti, hifadhi ya mazingira na kuimarisha demokrasia na utawala bora. “Ninakushukuru kwa jitihada zako katika kipindi chote cha miaka mitano uliyokuwepo hapa nchini kwani umesaidia kuimarisha mahusiano yaliyokuwepo baina ya nchi hizi mbili tangu miaka ya 60. Pia tumenufaika na programu za kubadilishana wataalamu baina ya nchi zetu,” amesema Waziri Mkuu. Amesema kutokana na changamoto za kiuchumi zilizokuwepo duniani, mwaka 2020 nchi hi...

Mbunge Ghati Chomete Afanikisha Upatikanaji wa Shilingi Milioni Sita Katika Uzinduzi wa Album ya Nimeelewa Somo

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara Mhe.Ghati Zephania Chomete, Jana tarehe 14 Julai 2024 amefanikisha kupatikana kiasi cha shilingi milioni sita wakati wa uzinduzi wa Album Mpya ya "Nimelielewa Somo" Kanisa la TPC-Tarime.  Mbunge huyo wa viti maalum mkoa wa Mara, amekuwa na mvuto mkubwa katika jamii hasa kutokana ushiriki wake mkubwa katika shughuli mbakimbali za jamii ndani na nje ya mkoani Mara,ikiwa ni pamoja na kuchangia Katika miradi mbali mbali ya maendeleo bila ya ubaguzi. Katika hafla hiyo fupi Mhe. Ghati Chomete na marafiki zake wakichangia Takribani Millioni Tatu (Tsh.3,000,000/=) huku mbunge wa Tarime mjini Mhe.Michael Kembaki akichangia Fedha Taslimu Shillingi Millioni Moja (Tsh.1,000,000/=).  Akizungumza katika hafla hiyo Mhe.Ghati ambaye alikuwa mgeni rasmi, amempongeza Rais Dr Samia Suluhu Hassan kwa jinsi serikali yake inavyoshirikiana na madhehebu ya dini kwa katika Shughuli mbakimbali za maendeleo yakiwemo ya kijamii na kiuchumi.

Waziri Kairuki Awataka Wananchi Katavi Kulinda Maeneo ya Hifadhi

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amewataka wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe, Mkoani Katavi kulinda maeneo ya hifadhi na kuacha kufanya shughuli za kibinadamu katika maeneo hayo. Ameyasema hayo leo Julai 15,2024 wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo Mkoani humo. "Tuyalinde mapori yetu ya akiba, na tusifanye  shughuli za kilimo na ufugaji kwenye maeneo yaliyohifadhiwa" amesisitiza Mhe. Kairuki. Mheshimiwa Kairuki yupo katika ziara ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye yupo mkoani Rukwa kwa ziara ya kikazi.

Waziri Mkuu Azindua Mitambo ya Kisasa ya Kurushia Matangazo

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Julai 15, 2024 amekagua na kuzindua mitambo na vifaa vipya vya kurushia matangazo vya kampuni ya Azam Media Limited. Vifaa hivyo ni pamoja na Magari ya kisasa ya kurushia matangazo (OB Van), kamera za kisasa pamoja na mfumo wa kusaidia maamuzi viwanjani (VAR). Vifaa hivyo vilivyogharimu shilingi bilioni tano vitatumika katika kurushia matangazo ya mpira wa miguu wa ligi Kuu Tanzania bara na Zanzibar pamoja michezo mingine. Akizungumza na wafanyakazi wa Az juuam Media pamoja na wadau wa michezo Mheshimiwa majaliwa amesema manunuzi ya vifaa hivyo ni mapinduzi makubwa katika tasnia ya habari kwani kunaifanya Tanzania kuwa nchi ya kipekee kuwa na vifaa vya kisasa vya aina yake katika ukanda wa Afrika Mashariki. Mheshimiwa Majaliwa pia ameshuhudia uzinduzi wa chaneli mpya ya Azam 4 HD ambayo itatumika kurusha ligi kuu ya Ufaransa (Legue 1) na ligi kuu ya Ujerumani (Bundesliga)

Kundo Mathew Awaagiza Waandisi wa Maji Kukamilisha Miradi Iliyokwama

Na Angela Sebastian-Bukoba  Naibu waziri wa maji mhandisi Kundo Mathew amewaagiza waandisi wa mamlaka za maji nchini kukamilisha miradi iliyokwama  pasipo kuanzisha miradi mipya Mhandisi Mathew amesema hayo alipowasili katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kagera kwa ziara ya siku tatu na kupokea taarifa ya kaimu mkuu wa mkoa wa Kagera Erasto Sima aliyeomba serikali kusaidia wananchi wa wilaya ya Bukoba kukamilishiwa mradi wa maji Kemondo ambayo umekwama kwa muda mrefu Amesema kuwa lengo la Serikali ni kutaka kuahakikisha miradi ya maji ambayo imekwama inakamilika ili kuwaondolea wananchi adha ya upatikanaji wa maji safi hivyo waandisi wa mamlaka za maji nchini wanatakiwa kutekeleza agizo hilo haraka iwezekanavyo kwa maslai mapana ya wananchi. "Hakuna sababu ya kutangaza miradi mingine wakati unao mradi uliofikia asilimia 70 au 80 ukauwezesha kukamilika lakini pia hatutaki tuwe na mchakato mrefu wa manunuzi kwasababu sheri imerekebishwa sisi Wizara na Ruwasa makao makuu tunatoa viba...