_▪️Awapongeza kuvuka lengo 2024- 2025._ _▪️TRA yarejesha Shilingi Trilioni 1.2 kwa walipa kodi kiwango kikubwa kuwahi kutokea._ WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuongeza usimamizi wa ukusanyaji wa kodi kwa wafanyabiashara ikiwemo wa mataifa ya nje walioamua kuja kufanya shughuli zao nchini. Amesema kuwa TRA inapaswa kuongeza ufanisi zaidi kwenye kuwasimamia wafanyabiashara wote kuhakikisha wanatambua sheria za ulipaji kodi pamoja na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kuhakiki utekelezaji wake. Ametoa agizo hilo leo (Jumanne Julai 08, 2025) alipofungua kikao kazi cha Viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika kituo cha Mikutano cha Arusha (IACC). “Nendeni mkachunguze hawa wanaokuja kufanya biashara nchini, kama wanaondoka na mapato yetu kwa kutolipa kodi yetu, ni lazima tubane eneo hilo kama ambavyo sisi tunabanwa tunapokwenda kwao, yeyote aliyeamua kuja kufanya biashara Tanzania ni lazima ajue Tanzania ina sheria zake ikiwemo za ul...
Marato tv - Sauti ya Jamii