Skip to main content

Posts

Showing posts from January 25, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Serikali Yawezesha Kuanzishwa Kwa Kituo Cha Kisasa Cha Teknolojia ya Madini Muhimu Nchini

● Ni matokeo ya MoU kati ya GST na Taasisi ya KIGAM kutoka Korea ya Kusini, ● Utekelezaji wa mradi huo kugharimu Bilioni 40 za Kitanzania ● Wataalam kutoka GST kujengewa uwezo  ● Wachimbaji wadogo kupatiwa Mafunzo malum *Wizara ya Madini - Mtumba* Ikiwa ni utekelezaji wa Madini Vision 2030, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewezesha kuanzishwa kwa mradi wa ujenzi wa Kituo cha kisasa na kikubwa cha Teknolojia ya Madini Mkakati na muhimu pamoja na ununuzi wa vifaa vya kisasa vya utafiti wa kina wa madini. Hayo yamesemwa leo tarehe 26 Januari, 2026 na Waziri wa Madini, *Mheshimiwa Anthony Mavunde (Mb)* alipokutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe maalum wa Watu 6 kutoka nchini Korea ukiongozwa na *Bw. Seong-Jun Cho* ambaye ni Mtaalam kutoka Taasisi ya Jiosayansi na Rasilimali Madini ya Korea (KIGAM). "*Mheshimiwa Rais* ametuelekeza sisi Wizara ya Madini kuhakikisha tunaongeza eneo la utafiti hadi kufikia asilimia 50 ifikapo mwaka 2030. Mradi huu na wenzetu wa Korea Kusini ...

Dkt. Mwigulu Aelekea Morogoro Kufungua Mkutano wa Mwaka wa Takukuru.

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba akisafiri kwa Treni ya reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) kutoka Dar es Salaam kuelekea Morogoro ambapo atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU, unaofanyika leo Januari 26, 2026.

Rais Samia Atoa Bilioni Kumi Kwa Wafanyabiashara Wadogo Ndani ya Siku Mia

   Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ndani ya siku 100 tayari imetoa shilingi bilioni 10.5 kwa ajili ya kuwawezesha wafanyabiashara ndogondogo zaidi ya 100,000 waliorasimishwa. Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 25 Januari, 2026, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amesema hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kujenga uchumi jumuishi unaowezesha wananchi wengi zaidi kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Taifa. Amesema sekta isiyo rasmi ni mhimili muhimu wa uchumi wa Taifa kwa kuwaajiri mamilioni ya Watanzania hususan wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. Hata hivyo, kwa muda mrefu sekta hiyo imekuwa ikikabiliwa na changamoto za kutotambulika kisheria, kukosa mitaji, masoko pamoja na mifumo ya ulinzi wa kijamii. Kupitia mkakati huo, Serikali imeimarisha zoezi la urasimishaji wa wafanyabiashara ndogondogo ili kuwaing...

Makonda, Lusinde, Halamga Wapitishwa Unec, Dk. Komba Apeta Ubunge Peramiho

Na. Mwandishi wetu, Zanzibar. Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, katika kikao chake kilichofanyika Zanzibar tarehe 25 Januari 2026, imeidhinisha uteuzi wa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa pamoja na viongozi mbalimbali wa chama wanaotokana na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi. Kwa upande wa Tanzania Bara, wajumbe walioteuliwa kuingia Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ni Paul Christian Makonda na Livingstone Joseph Lusinde (wanaume), pamoja na Asia Abdulkarim Halamga (wanawake). Kutoka Zanzibar, Kamati Kuu imeridhia uteuzi wa Khamis Mussa Omar (wanaume) na Tauhida Cassian Galos (wanawake). Aidha, Kamati Kuu imemteua Agnes Elias Hokororo kuwa Katibu wa Wabunge wote wa CCM, huku Najma Murtaza Giga, Deodatus Philippo Mwanyika na Cecilia Daniel Pareso wakiteuliwa kuwa Wenyeviti wa Bunge. Kwa upande wa Baraza la Wawakilishi, Kamati Kuu imeridhia uteuzi wa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambao ni Said Ali Juma na Hamza Ha...

Siku 100 za Dkt. Samia Suluhu Hassan Serikali Imekutana na Wanaume Ili Kuondoa Tatizo la Ukatili wa Kijinsia Nchini

DODOMA. Kutokana na umuhimu wa wanaume katika ustawi na maendeleo ya jamii, Serikali imekutana na kufanya mazungumzo na majukwaa mbalimbali ya wanaume nchini ili kuona namna Bora ya kukabiliana na ukatili wa kijinsia na kuimarisha malezi, makuzi na wajibu wa familia katika jamii. Kauli hiyo ya serikali ameisema waziri wa maendeleo ya Jamii,jinsia, wanawake na Makundi Maalumu Mhe. Dorothy Gwajima Leo jijini Dodoma wakati akieleza mafanikio ya utambuzi,urasimishaji na uwezeshaji wa makundi ya wajasiriamali katika sekta isiyo Rasmi ndani ya siku Mia Moja za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Amesema hatua hiyo ya ushirikishwaji wa wanaume ni hatua muhimu kuelekea kuimarisha majukwaa ya wanaume kwa lengo la kutambua mchango wao katika ustawi na maendeleo ya jamii. "kwa kuelewa umuhimu wa wanaume katika ustawi na maendeleo ya jamii yetu, Serikali imekutana na kufanya mazungumzo na majukwaa mbalimbali ya wanaume nchini ikiwa ni hatua muhimu kuelekea kuimarisha majukwaa ya wanaume ili waisai...

Kanisa la Mlima wa Moto Laja na Kongamano Kuombea Taifa Amani

Na Mwandishi Wetu KANISA la Mlima wa Moto la Mikocheni jijini Dar es Salaam, limezindua kongamano la kuombea nchi amani lijulikanalo kama Anza mwaka na Bwana na miongoni mwa yatakayozungumziwa ni ujasiriamali. Akizungumza leo Kanisani hapo, Askofu wa Kanisa hilo, Rose Mgeta alisema miongoni mwa yatakayofanyika kwenye kongamano hilo la siku nane ni kuombea nchi amani ili isirudi kwenye machafuko ya Oktoba 229 mwaka jana. Alisema kwenye kongamano hilo vijana pia watafundishwa masuala ya ujasiriamali na biashara ili waweze kutambua fursa na kuzitumia kuondokana na umaskini. Alisema vijana watakaohudhuria kongamano hilo mbali na neno la Mungu watafundishwa mbinu mbalimbali za kufafuta fedha kama ujasiriamali na namna ya kutumia fursa mbalimbali za kibiashara zilizopo. Askofu Mgetta alisema maadili kwa sasa yanakwenda kombo hivyo kwenye kongamano hilo watafundisha pia vijana kuzingatia maadili ikiwemo kuheshimu wazazi na watu wanaowazunguka. “Vijana waishi maisha ya heshima kwa wazazi na wa...