Mahakama ya wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza imemuhukumu kifungo cha miezi sita Rajabu Reli (22), mkazi wa Sengerema baada ya kukutwa na hatia ya kuvaa sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) bila ruhusa. Hukumu hiyo imetolewa jana tarehe 07.01.2025 katika shauri la jinai namba 445 la mwaka 2025 na Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo Mhe. Evodius Kisoka mbele ya mwendesha mashtaka wa Serikali Nyamhanga Tissoro. Kwa mujibu wa hati ya mashtaka iliyosomwa na mwendesha mashtaka wa Serikali Nyamhanga Tissoro mbele ya hakimu Evodius Kisoka, mshtakiwa alitenda kosa hilo mnamo tarehe 05.12.2024 huko kijiji cha Kasisa, wilaya ya Sengerema kinyume na kifungu cha 178(1) cha sheria ya kanuni ya Adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022. Mshtakiwa alifikishwa mahakamani januari 07.2025 na kusomewa shitaka la kuvaa sare za Jeshi la wananchi wa Tanzania bila ruhusa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Baada ya kusikiliza pande zote za ushahidi hakimu Evodius Kisoka alijiridhi...
Marato tv - Sauti ya Jamii